Kufuatia mjadala wa kupanda kwa gharama za vifurushi kwa watumiaji wa Data kwenye mitandao ya kijamii, Waziri ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye kupitia Ukurasa wake wa Twitter ametoa ufafanuzi kwamba baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuingia madarakani, alichukua hatua ya kushusha gharama za data.
Waziri Nape amesema mwezi Machi 2021 bei ya juu ilikuwa ni Tsh. 40.04 kwa MB 1, lakini ilipungzwa na kufikia Tsh. 9.35 kwa MB 1 mwezi Agosti 2022.
Kumekuwepo na mjadala kupitia mitandao ya kijamii hususani Twitter, JamiiForums na kwenye kurasa nyingine kuhusu kupanda gharama za vifurushi vya mitandao ya simu ikiwemo gharama za Data (Internet) bila utaratibu ambao ni shirikishi wa watumiaji.
Kwa mujibu takwimu Watumiaji wa Internet kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Nchini Tanzania (TCRA) ripoti ya robo ya nne ya mwaka 2021 zinaonesha Watumiaji wa intaneti walifikia milioni 29.8.
=======================