kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Elimu ndio chombo pekee kinachoweza kuwakutanisha mtoto wa tajiri na mtoto wa maskini katika ofisi moja na mgahawa mmoja. Takwimu zinaonyesha kuwa shule binafsi za msingi na sekondari nchini ni ghali kuliko za serikali lakini ndizo zenye mazingira mazuri ya kujifunzia na kutoa ufaulu mkubwa kwa wanafunzi wengi.
Na vyuo vikuu vya Serikali ni nafuu kusoma lakini ndivyo vyenye mazingira mazuri na miundombinu ya kufundishia na watoto kupata taaluma ya uhakika. Mpaka hapo hatubishani na hakuna ubishi.
Dhambi inakujaje wakati wa udahiri wa wanafunzi?
1. Vyuo vya serikali vinatoza ada ndogo sana lakini vinadahiri wanafunzi wenye ufaulu mkubwa sana(e.g Muhimbili University), bila shaka wengi wa wanafunzi wenye sifa hizi wengi wao ni wale wanaotoka kwenye shule za binafsi za sekondari kama FEZA, kanosa, etc.
Wazazi wa watoto hawa wengi wao ni wale wenye uchumi wa juu na wakati nchini ambao wanafahamu kuwa vyuo vya serikali vina walimu bora na miundombinu mizuri ya elimu, hivyo pamoja na kuwa na uwezo mkubwa wa kifedha wa kuendelea kuwasomesha watoto vyuo binafsi nchini na nje ya ya nchi lakini hawawapeleki watoto wao kwenye vyuo binafsi nchini kwakuwa wanavijua kuwa hata walimu wao ni wazee waliochoka na vijana wasiokuwa na uwezo mkubwa wa kufundisha.
2. Vyuo vya binafsi havina miundombinu mizuri ya kufundishia (walimu, madarasa, practice, library, office, ect) lakini vinatoza ada kubwa sana ili kumudu kulipa mishahara ya watumishi, majengo, na tozo mbalimbali za serikali. Pamoja na ughali wa vyuo hivi lakini Watoto wa maskini waliosoma shule za serikali wanajikuta wakisukumiwa kwenye aina hii ya vyuo baada ya kukosa nafasi kwenye vyuo vya serikali vyenye ada ambayo wazazi wangeimudu kulipa japo pia kwa tabu.
Kadhia hii inasababisha mambo mabaya sana kwa watoto na wazazi wao zikiwemo za wazazi kuuza kila kitu yaani kila kitu cha familia ili kumudu ada ya mtoto mmoja kwenye chuo binafsi, watoto kukosa mitihani na kuacha shule kwa kukosa ada, wanafunzi kujiingiza kufanya vitendo vibaya vya kuuza mili na madawa au kufanya biashara na wizi ili kusaidia wazazi wao kujaza kile kinachokosekana kwenye gharama za vyuo binafsi.
3. Fedha ya serikali (loans board) inapotea bure kwa watoto hawa kwenye vyuo binafsi. Yaani mtoto anaacha chuo katikati kwa kukosa kulipa kiasi cha ada kujalizia kile cha mkopo alichopewa na loans board. Watoto hawa wanateseka sana vyuoni kwasababu wanalazima kutumia ile meals and accommodations wanayopewa kwa kulipia ada zao. Mtoto akiacha masomo maana yake hata kiasi alichokopeshwa na loans board kimepotea pia.
4. Scholarships na mikopo vinaangalia ufaulu wa mtoto bila kuangalia mtoto kasoma shule gani. Hii inamaanisha kuwa wenye nacho wataongezewa pia hapa. Yaani watoto wa wenye nacho ndio waliosoma shule za private na wengi ndio wenye ufaulu mkubwa kuweza kuwa na sifa za kupata scholarships na mikopo.
5. Mtoto wa Maskini hatakutana na mtoto wa tajiri ofisi moja kama trend itakuwa hiihii.
Hapa ni ama;
Shule za Serikali pia ziongezewe ubora katika kutoa elimu, vyuo vya private vipewe ruzuku na serikali ili ada yao pia iwe himilivu au vyuo vya serikali vihudumie zaidi shule za serikali.
Mifumo ya Serikali lazima isomane, haiwezekani vyuo vya serikali na shule za serikali hiyohiyo havisomani, yaani shule za serikali zinazalisha watoto wasiotakiwa na vyuo vya serikali.