Waziri Prof. Mkenda dhambi hii ya udahili vyuoni isisubiri tamko la Rais Samia

Waziri Prof. Mkenda dhambi hii ya udahili vyuoni isisubiri tamko la Rais Samia

Huna hoja. Ufaulu hautegemei kama upo private au serikalini. Hilo ndilo Prof. Ndalichako alikosea. Acha wapimwe kwa ufaulu
Ufaulu una vichocheo vyake, vikiwemo:
1. Utayari (readiness) wa mtoto kusoma (akili, afya, mahitaji, usalama)
2. Mazingira ya nyumbani (support system) wazazi malazi chakula mavazi stationery pocket money
3. Mazingira ya shule (walimu, madarasa, madawati, vitabu, library, maabara, usafiri, chakula shuleni, usalama)
4) serikali (mitaala, sera, ukaguzi, motisha kwa walimu, mtihani, usalama)

Hivi vyote ni vitu vya kawaida kwa watoto wa shule za private lakini ni nadra kwa wqtoto wa government schools
 
Ufaulu una vichocheo vyake, vikiwemo:
1. Utayari (readiness) wa mtoto kusoma (akili, afya, mahitaji, usalama)
2. Mazingira ya nyumbani (support system)
3. Mazingira ya shule (walimu, madarasa, madawati, vitabu, maabara, usafiri, chakula shuleni, usalama)
4) serikali (mitaala, sera, ukaguzi, motisha kwa walimu, mtihani, usalama)
Nakataa kabisa, mi mwenyewe nimesoma mazingira magumu ila kote nilipata division one na darasa la saba nilikuwa top 10. Huu ujinga wa kusema mazingira ndiyo tunaharibu watoto tunatengeneza kizazi ambacho hakijitambui kila siku kinalalamika eti mazingira etc.
 
Wasomi wetu wanathamini mtu mwenye uwezo wa kukumbuka na siyo kufikiri
Ndiyo maana wao pia hawana huo uwezo wa kufikiri.
Kaka shule za private wanafanya majaribio (past papers) nyingiiiiiii ili kukariri maswali yaani repeation makes perfect ili siku ya mtihani wa taifa majibu ya maswali yawe kwenye short term memory ili iwe rahisi kwao kuyakumbuka, hii kitaaluma tunaiita rote learning. Sasa huko kwenye shule ya kata hawana muda huo wa kukaririshana bali wanafundishana kama mtaala unavyotaka, isitotoshe wanafunzi wanahangaika na usafiri, kufagia na kufyeka majani, kunyweshea maua, kuchota maji ya walimu, kulima mashamba ya shule, kupikia walimu, nk. Hiyo division 1 ya points 3 watalipata wp? nakuja kuhamaki vyuo vyote vikuu vya serikali na private vizuri vimejaa wanafunzi wa private watoto wa wasure kwakuwa wana ufaulu mkubwa na hela za kulipa ada kubwa pia. Mtoto wa st. Kayumba hana vyote ufaulu wala hela.
 
Shida mitihani imekuwa rahisi mnooo. Na hii ni kuanzia Primary. Hivyo ni mafuriko ya Div 1.
Ktk level ya chuo, hakuna cha kupangiana, isipo kuwa free and fair environment iwepo, iwe maskini au tajiri huenda ni vyuo binsfsi au Govt. Mbona kwa level ya Sec hamuombi hiyo miongozo wakati ADA ni juu na Mazingira ya kujifunzia Private ni bora kuliko Govt?
 
Udahili wa chuo kigezo ni kimoja tu, ufaulu wa mwanafunzi. Hizo nyingine za sijui kipato cha mzazi ni siasa!

Jambo la muhimu ni bodi ya mikopo itoe mikopo kwa wote wanao omba. Mtu mzima anaomba mkopo maana yake anauhitaji, waaache ujinga wao.
Watoto wote ukiwapatia mazingira sawa ya elimu wanafaulu wote. Hata mtoto aliyepata DDD kwenye ufaulu wake wa PCB akipelekwa chuo kikuu chenye walimu safi wenye reaching methodology, maabara, sehemu ya kufanya masomo kwa vitendo watafaulu wote pia.

Kwahiyo serikali ingenge vyuo vikuu vya kata basi
 
06 September 2022
Jarkata, Indonesia 🇮🇩

Maandamano ya wanafunzi, wavuvi, wakulima, waalimu na vibarua Indonesia

b1e506d0-efe6-4726-be9b-1956a9a28d41_16x9_1200x676.JPG


Wafanyakazi na wanafunzi waandamana kutokana na mfumuko wa gharama za maisha inayopelekea hali ngumu ya maisha.


Pia bei ya mafuta imepanda sana hivyo makundi haya ya kijamii yameamua kuingia barabarani kwa maandamano. Serikali ya Indonesia kwa miongo kadhaa ilikuwa inatoa ruzuku kubwa kwa mafuta


Workers and students in Indonesia protest over fuel price hike​

Reuters, Jakarta​

Published: 06 September ,2022: 12:54 PM GSTUpdated: 06 September ,2022: 01:04 PM GST

Thousands of people rallied in Indonesia’s biggest cities on Tuesday, seeking to pile pressure on the government to reverse its first subsidized fuel price hike in eight years amid soaring inflation.

Under pressure to control a ballooning energy subsidy budget, President Joko Widodo on Saturday said he had little choice but to hike subsidized fuel prices by about 30 percent, an unpopular move in the country of 270 million people. Oil prices are about 32 percent higher than a year ago.

By midday on Tuesday, protests were underway in and around the capital Jakarta and in the cities of Surabaya, Makassar, Kendari, Aceh, and Yogyakarta, among a series of demonstrations led by students and labor unions that police say could draw tens of thousands of people this week.

Thousands of police were deployed across Jakarta, many guarding gas stations, fearing those could become targets of mounting anger over a price hike that unions say will hurt workers and the urban poor the most.

“Workers are really, really suffering right now,” said Abdul Aris, a union official.

“The price shouldn’t have been raised,” he said, vowing to keep fighting until the government gives way.

Tuesday’s protests started peacefully, with no early reports of violence or arrests.

Thousands gathered in Jakarta wearing red or orange bandanas, marching and chanting slogans denouncing the government move and calling for an increase in the minimum wage.

One demonstrator was seen shirtless with feet shackled to an empty petrol tank, carrying a sign highlighting hardships of rising costs.

Textiles factory worker Adi Asmadi, 29, said his daily transportation expenses would go up sharply.

“If the fuel price is hiked and wages increase too, that’s ok,” he said. “If it’s not, we object.”

Subsidized fuel is a sensitive issue in Southeast Asia’s biggest economy, but the government has sought to soften the blow through compensation measures, including direct cash transfers.

The hike would cut subsidy spending by about 48 trillion rupiah ($3.22 billion) this year to 650 trillion rupiah, a deputy finance minister said on Monday, but it would also see inflation accelerate.

Small rallies took place at the weekend and on Monday, with tires burned and some roads blocked as demonstrators vented their anger over the decision, which comes amid rising food costs and with the economy still reeling from the impacts of the pandemic
 
Nakataa kabisa, mi mwenyewe nimesoma mazingira magumu ila kote nilipata division one na darasa la saba nilikuwa top 10. Huu ujinga wa kusema mazingira ndiyo tunaharibu watoto tunatengeneza kizazi ambacho hakijitambui kila siku kinalalamika eti mazingira etc.
Bora uwe mjinga kuliko kuwa mpumbavu, huwezi kusoma shule haina maabara, walimu na vitabu halafu useme mazingira hayaathiri. Unasoma kwa kibatari halafu unasema unaweza kushindana na watoto wanaosoma st. Francis ambao wao kila kitu kipo, hawalimi, hawafagii, walimu wenye ari wapo, tuition mjini zipo halafu useme masingira sio kitu katika kufaulu, kama wewe ulifaulu basi kwenu kulikuwa na afadhali, angalau daftari, vitabu, chakula, pocket money, kibaskeli cha kwendea shule na mwanga wa kusomea ulikuwa navyo
 
Unaongea tu kwa sababu una haki ya kuongea ama😬😬
serikali inakwama parefu sana, yaani haimtambui mtoto wa kaya maskini..... what a stupid 😬😬
 
Hebu tuwe na subira, serikali yetu inafahamu kuwa inazo shule na vyuo vyake nchini, siamiini kama Samia scholarships (mkuu wa serikali) zitawaacha nje wanafunzi wake kutoka shule zake hizi pendwa kwa kisingizio chochote. Kama itatokea hivyo basi Rais atakuwa amedanganywa na wasaidizi wake. Kila mama atamnyonyesha mwanawe kwanza kabla ya yule wa ndugu au jirani yake.
 
Kaka ni kweli, lakini mifumo yote ya serikali ni lazima isomane, vyuo vya serikali haiwezekani visisomane na shule za serikali, Hii ina maana kwamba zile 600 Samia scholarships kwa watoto watakaosoma kozi za sayansi zitakwenda kuwanufaisha watoto wa vigogo na kuwaacha watoto wa wakulima na wavuvi nchini.
Mkuu huo ndiyo ukweli wenyewe
 
Lakini hilo haliwezi kuondoa pointi ya msingi kwamba kigezo cha kwanza kabisa cha udahili chuo kiwe ufaulu wako...kwa sababu ile ni taasisi ya elimu...ufaulu ni kipaumbele.
 
Solution ni serikali kuongeza miundombinu na ubora wa shule zake...ili kumuwezesha mwanafunzi kupata ufaulu unaohitajika....na si chuo kushusha kigezo cha ufaulu. Itakuwa ni kitu cha ajabu kwa taasisi ya elimu kuchagua watu wa tabaka mojawapo..hasahasa taasisi ya kiserikali
 
Lakini hilo haliwezi kuondoa pointi ya msingi kwamba kigezo cha kwanza kabisa cha udahili chuo kiwe ufaulu wako...kwa sababu ile ni taasisi ya elimu...ufaulu ni kipaumbele.
hakuna ubishi kwenye hilo la uhusiano kati ya ufaulu na kuingia chuo kikuu. Serikali kupitia TCU, NACTVET na mabaraza ya kitaaluma, Wizara ya Elimu na TAMISEMI wameshatoa muongozo kuhusu ni nani kafaulu na ni nani kafeli na ni nani anaweza kuchaguliwa kwenye mafunzo form I, form II, form V, VETA, Certificate, Diploma, Shahada, Uzamili na Uzamivu (PhD). Hii ina maana kuwa serikali ni moja na sera ya mafunzo ni moja, hivyo taasisi zote hizi za kutoa mafunzo lazima zisomane. Mfano, kama kuongea Kiingereza ni tatizo kwenye shule za msingi na sekondari za serikali tunategemea kuona vyuo vya kati na vyuo vikuu vya serikali kupata wanafunzi wengi sana wasiojua kuongea Kiingereza pia. Kama ufaulu kwenye shule za serikali ni mdogo lazima na vyuo vya serikali wapatikane wanafunzi wenye ufaulu mdogo pia, maana kwa taasisi za serikali inakuwa ni ile ya "garbage in garbage out", yaani hiyo ndiyo hali halisi na taswira ya elimu ya Tanzania, hata ukitaka kufanya utafiti (cohort au comparative studies) kwenye elimu ya tanzania utapata majibu sahihi kabisa. LAKINI kama wanafunzi walioko kwenye vyuo vya serikali wengi wao hawatokani na shule za serikali hapo utapata majibu ambayo siyo ya kuaminika kwenye utafiti wako, na kufanya dhambi hii kunalipasua taifa kati ya walionacho na wasionacho, kutatokea vicious cycle ya kutisha sana kwenye taifa.

Wacha vyuo vya serikali vihudumie zaidi shule za serikali na vyuo kwa private vihudumie zaidi shule za private, vingigine tutaonekana taifa lote halina akili, kwakuwa watoto wa walionacho wanaweza kusoma vyuo vya serikali na vyuo binafsi bila shida, lakini watoto wa masikini hawawezi kusoma vyuo vya private bila shida, hivyo watabakiwa na option moja tu ya vyuo vya serikali ambavyo kwa bahati mbaya navyo vimeshajaza watoto wa wenye nacho, na mbaya zaidi hata scholarships za serikali (samia scholarships) zinakwenda kuwabeba watoto wa wenye nacho ambao ni obvious watakuwa na ufaulu mkubwa kuliko wale wa shule za kayumba.

Ningeshauri hizi scholarships na udahiri kwenye vyuo vya serikali wangeanza kuchukua wanafunzi wenye division One wooooooooote kutoka shule za serikali walioomba kwenye vyuo vyao vya serikali then ndio wachukue watoto wenye division One kutoka shule binafsi na mashirika ya dini. hapo utakuwa angalau umetengeneza dependable and reliable pattern kwenye udahiri.
 
TATIZO siyo hayo;

Tatizo ni kijana anapomaliza kusoma anajiajirije wakati elimu aliyosoma sio ya kujiajiri!!?

Yaani anakuwa mtumwa wa kutafuta ajira!

Nadhani tu focus kwenye anachopata kijana Baada ya learning process kukamilika!

Hicho ndicho watz wanachotaka kusikia na sio udahili kwa elimu ambayo Panya road wanaendelea kuongezeka nchini !

Hofu yangu huko mbeleni ni kuwa na Panya road graduates!!
 
TATIZO siyo hayo;

Tatizo ni kijana anapomaliza kusoma anajiajirije wakati elimu aliyosoma sio ya kujiajiri!!?

Yaani anakuwa mtumwa wa kutafuta ajira!

Nadhani tu focus kwenye anachopata kijana Baada ya learning process kukamilika!

Hicho ndicho watz wanachotaka kusikia na sio udahili kwa elimu ambayo Panya road wanaendelea kuongezeka nchini !

Hofu yangu huko mbeleni ni kuwa na Panya road graduates!!
Lakini kwenye uchaguzi wa nini cha kusoma nani alaumiwe lakini mind set ya mtu imekaaje katika suala la ajira
 
Back
Top Bottom