Waziri Prof. Mkenda dhambi hii ya udahili vyuoni isisubiri tamko la Rais Samia

ujinga mama kumnyonyesha mtoto wa jirani na kumwacha mtoto wake afe njaa.
Huu ubaguzi ulihubiriwa Sana jiwe. Enzi hizi za mama Samia tunaongelea usawa. Na usawa ktk elimu unaletwa na ufaulu. Vyuoni wanaangalia ufaulu haijalishi ulisomea wapi
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Baada ya kusoma hii thread yote nimekuja na mtazamo huu
1. Shule za private zinafaulisha kuliko za selikali na nadhani hii inatokana na uwekezaji wa kitaaluma na kinidhamu unaofanywa na shule za private ni ngumu kukuta mtoto au mwalimu wa Feza amekosa kipindi.
2. Selikali iwekeze kwenye Elimu ya chini kwa kuajiri waalimu, kuajiri watu wa kuwasimamia waalimu ipasavyo na iweke sheria za kuwasimamia wanafunzi wa shule za selikali, adhabu kali zitolewa kwa wanafunzi wa selikali ambao wataonesha kutofata mienendo inayotakiwa ikiwemo kuwafukuza shule kama wafanyao wenzao wa private (n.b. Hili litaleta wananchi tena kupiga kelele kuwa watoto wa maskini wanaonewa maana siku zote hatujui tunataka nini).
3. Kigezo cha kujiunga na vyuo bora kibaki ufaulu kuendelea kuleta ushindani na kufanya wanafunzi wajitume kupata nafasi.
4. Mwisho selikali ijaribu kutoa ruzuku kwenye Elimu ya juu, hili liendane sambamba na kuregulate ada za vyuo binafsi, ili mwisho wa siku ada zote ziendane na wanafunzi wenye uwezo wa chini waweze kumudu gharama.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Kwenye udahili kinachozingatiwa ni ufaulu tu. Hata hao Watoto wa maskini kama wamefaulu vizuri wanapatag bila shida.

Watoto wa maskini wengi tu wamesoma kwenye hivyo vyuo vya umma. Cha msingi Watoto wa maskini tujitahidi kufaulu vizuri ili tusianze kuomba huruma ya serikali wakati wa udahili.

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Wacha urongo wewe, nenda kaangalie MUHAS wamedahiri wanafunzi wenye ufaulu gani mwaka huu 2022/23 halafu ndio uje uchangie Uzi huu. Ulitaka wale wanafunzi wa Kamsamba high high school waende wakasome wapi? Vyuo vya serikali lazima vitafsiri sera na mipango ya serikali kwenye elimu.
Kamsamba sawa ni shule ya serikali, unataka kusema Kamsamba hawana uwezo kabisa wa kupata Div I za point 3 na 4?

Kama hawana uwezo unashauri nini kifanyike kwenye hizo shule?

Maana Mitihani ya Taifa ni ileile na wanafanya maswali sawa na wale wa Private. Sijaelewa kwa nini unahitaji sana Mtanzania aliyefeli achukue nafasi za Watanzania wengine waliofaulu zaidi yake.

Kama hawana uwezo basi hawataweza kuingia MUHAS, na usipende kutafuta visingizio ili kupata Huruma.

MUHAS imejengwa kusomesha Watanzania na watoto wa Mataifa mengine wenye matokeo mazuri ili tupate wataalam thabiti wa Idara za Afya. Hiki ni Chuo cha Tanzania chenye hadhi yake

Jenga Chuo kingine cha kwako cha Private, ili tusomeshe Madaktari walio na Background hafifu na unaosema ni Maskini

Ushauri wangu,

"Si lazima sana kusoma fani inayokushinda uwezo. Kwa mfano, ukiwa duni wa Chemistry hauwezi kusoma Petroleum, duni wa Mathematics hautasoma Engineering yoyote na usipojua Physics hauwezi kusoma Telecommunications, Water Resources Engineering, Mining Engineering na Mengine kibao"

Mbona wanafunzi wenyewe wanajua kabisa kuwa akitaka kipi asome namna gani!?

Hawataonewa huruma kwa sababu Madai yako yanapanga kudhoofisha hadhi ya Vyuo Vikuu vya Nchi yetu
 
Elimu ndio chombo pekee kinachoweza kuwakutanisha mtoto wa tajiri na mtoto wa maskini katika ofisi moja na mgahawa mmoja. Takwimu zinaonyesha kuwa shule binafsi za msingi na sekondari nchini ni ghali kuliko za serikali lakini ndizo zenye mazingira mazuri ya kujifunzia na kutoa ufaulu mkubwa kwa wanafunzi wengi.

Na vyuo vikuu vya Serikali ni nafuu kusoma lakini ndivyo vyenye mazingira mazuri na miundombinu ya kufundishia na watoto kupata taaluma ya uhakika. Mpaka hapo hatubishani na hakuna ubishi.

Dhambi inakujaje wakati wa udahiri wa wanafunzi?
1. Vyuo vya serikali vinatoza ada ndogo sana lakini vinadahiri wanafunzi wenye ufaulu mkubwa sana(e.g Muhimbili University), bila shaka wengi wa wanafunzi wenye sifa hizi wengi wao ni wale wanaotoka kwenye shule za binafsi za sekondari kama FEZA, kanosa, etc.

Wazazi wa watoto hawa wengi wao ni wale wenye uchumi wa juu na wakati nchini ambao wanafahamu kuwa vyuo vya serikali vina walimu bora na miundombinu mizuri ya elimu, hivyo pamoja na kuwa na uwezo mkubwa wa kifedha wa kuendelea kuwasomesha watoto vyuo binafsi nchini na nje ya ya nchi lakini hawawapeleki watoto wao kwenye vyuo binafsi nchini kwakuwa wanavijua kuwa hata walimu wao ni wazee waliochoka na vijana wasiokuwa na uwezo mkubwa wa kufundisha.

2. Vyuo vya binafsi havina miundombinu mizuri ya kufundishia (walimu, madarasa, practice, library, office, ect) lakini vinatoza ada kubwa sana ili kumudu kulipa mishahara ya watumishi, majengo, na tozo mbalimbali za serikali. Pamoja na ughali wa vyuo hivi lakini Watoto wa maskini waliosoma shule za serikali wanajikuta wakisukumiwa kwenye aina hii ya vyuo baada ya kukosa nafasi kwenye vyuo vya serikali vyenye ada ambayo wazazi wangeimudu kulipa japo pia kwa tabu.

Kadhia hii inasababisha mambo mabaya sana kwa watoto na wazazi wao zikiwemo za wazazi kuuza kila kitu yaani kila kitu cha familia ili kumudu ada ya mtoto mmoja kwenye chuo binafsi, watoto kukosa mitihani na kuacha shule kwa kukosa ada, wanafunzi kujiingiza kufanya vitendo vibaya vya kuuza mili na madawa au kufanya biashara na wizi ili kusaidia wazazi wao kujaza kile kinachokosekana kwenye gharama za vyuo binafsi.

3. Fedha ya serikali (loans board) inapotea bure kwa watoto hawa kwenye vyuo binafsi. Yaani mtoto anaacha chuo katikati kwa kukosa kulipa kiasi cha ada kujalizia kile cha mkopo alichopewa na loans board. Watoto hawa wanateseka sana vyuoni kwasababu wanalazima kutumia ile meals and accommodations wanayopewa kwa kulipia ada zao. Mtoto akiacha masomo maana yake hata kiasi alichokopeshwa na loans board kimepotea pia.

4. Scholarships na mikopo vinaangalia ufaulu wa mtoto bila kuangalia mtoto kasoma shule gani. Hii inamaanisha kuwa wenye nacho wataongezewa pia hapa. Yaani watoto wa wenye nacho ndio waliosoma shule za private na wengi ndio wenye ufaulu mkubwa kuweza kuwa na sifa za kupata scholarships na mikopo.

5. Mtoto wa Maskini hatakutana na mtoto wa tajiri ofisi moja kama trend itakuwa hiihii.

Hapa ni ama;
Shule za Serikali pia ziongezewe ubora katika kutoa elimu, vyuo vya private vipewe ruzuku na serikali ili ada yao pia iwe himilivu au vyuo vya serikali vihudumie zaidi shule za serikali.

Mifumo ya Serikali lazima isomane, haiwezekani vyuo vya serikali na shule za serikali hiyohiyo havisomani, yaani shule za serikali zinazalisha watoto wasiotakiwa na vyuo vya serikali.
Safi sana, Prof kanena vema
 
Ahsante kwa bandiko hili.

Mwanangu anamaliza darasa la saba mwaka huu. Natumaini hili bandiko likipata utatuzi basi hata mwanangu atafaidika huko mbeleni
 
Hebu tulieni.
Unataka kutuzalishia madaktari wa mchongo.
Kama wewe unaamini kuwa shule za serikali zinatoa madakitari wa mchongo huo utakuwa mjadala mwingine, lakini vyuo vya serikali vya nchi yoyote Ile vinajukumu la kutafsiri mipango ya serikali kwenye utoaji wa elimu. Vyuo vikuu hivi vitakuwa vnaitukana serikali kwa kujua au kutokujua kama vitadhani kuwa wanafunzi kutoka shule za serikali hawafai kuweko kwenye vyuo vikuu vya serikali, yaani hawafundishiki, hawachaguliki kuliko wale wa shule za binafsi. Kumbuka kuwa mzazi kuacha kupeleka mwanae kusoma shule ya msingi na sekondari ya serikali na kumpekeka zile za private ni ujumbe tosha kuwa serikali Ina mapungufu. Sasa haiwezekani baniani awe mbaya halafu kiatu (vyuo vya serikali) chake kiwe dawa.

Hapa sisemi kuwa watoto waliosoma shule binafsi wasisome vyuo vikuu vya serikali lahsha, bali wanafunzi kutoka shule za serikali lazima wapewe kipaumbele kwenye vyuo vya serikali, nafasi ikibaki ndio wapewe shule binafsi. Tukifanya hivyo tutakuwa tujuwa kile tunachokifanya kwenye elimu, lakini sio hii ya macho komchuzi mkono kwa ubwabwa inayofanyika Sasa.

Hebu fikiria mzazi kasomesha mtoto shule ya serikali hadi akapata ufaulu mzuri wa division 1 ya point 6 au 7 lakini anakosa nafasi chuo Cha serikali na kuambiwa aende akatafute chuo binafsi akalipe 6m. Huo ni uonevu wa kiwango Cha lami. Inatakiwa akose chuo Cha serikali only if nafasi kwenye vyuo vya serikali zimejazwa na wanafunzi kutoka shule za serikali pia, yaani ufaulu kwenye shule za serikali ni mkubwa pia, lakini sio kwasababu zimejazwa na watoto kutoka feza schools ambako watoto wa viongozi ndiko walikosoma.
 
Mleta mada unaumwa wewe. Kwahiyo unataka vyuo vya serikali vidahili wanafunzi wenye ufaulu mdogo? Mbona umetoa hoja mfu Sana hii?

Kigezo cha ufaulu ndiyo sifa kuu ya mtoto kujiunga na chuo kikuu. Ndiyo maana wazazi maskini kabisa wanajinyima na kumtafutia mtoto shule ya private ili akafaulu.

Sasa wewe endelea kunywa mbege na kukata mauno kwenye mikutano ya ccm halafu utarajie mwanao atadahiliwa na division 3 yake
Serikali kupitia TCU imetoa sifa za mwanafunzi kusoma kozi fulani, ziko wazi, vyuo vya serikali lazima vitekeleze uwamuzi huu wa serikali kwa vitendo. Vyuo vikuu binafsi vinaweza kuhoji na kuchuja sifa hizi lakini sio vyuo vya serikali. Unapoona chuo Cha serikali kinadahiri wanafunzi wenye ufaulu wa division I ya points 3, 4 na 5 TU maana yake imeitukana serikali. Mkuu wa chuo lazima akamatwe na kuhojiwa. Kama anataka wanafunzi wa hivyo lazima iwe ni sera ya kitaifa kwa chuo hicho, la sivyo aende akafungue chuo chake chenye hadhi hiyo.
 
Kamsamba sawa ni shule ya serikali, unataka kusema Kamsamba hawana uwezo kabisa wa kupata Div I za point 3 na 4?

Kama hawana uwezo unashauri nini kifanyike kwenye hizo shule?

Maana Mitihani ya Taifa ni ileile na wanafanya maswali sawa na wale wa Private. Sijaelewa kwa nini unahitaji sana Mtanzania aliyefeli achukue nafasi za Watanzania wengine waliofaulu zaidi yake.

Kama hawana uwezo basi hawataweza kuingia MUHAS, na usipende kutafuta visingizio ili kupata Huruma.

MUHAS imejengwa kusomesha Watanzania na watoto wa Mataifa mengine wenye matokeo mazuri ili tupate wataalam thabiti wa Idara za Afya. Hiki ni Chuo cha Tanzania chenye hadhi yake

Jenga Chuo kingine cha kwako cha Private, ili tusomeshe Madaktari walio na Background hafifu na unaosema ni Maskini

Ushauri wangu,

"Si lazima sana kusoma fani inayokushinda uwezo. Kwa mfano, ukiwa duni wa Chemistry hauwezi kusoma Petroleum, duni wa Mathematics hautasoma Engineering yoyote na usipojua Physics hauwezi kusoma Telecommunications, Water Resources Engineering, Mining Engineering na Mengine kibao"

Mbona wanafunzi wenyewe wanajua kabisa kuwa akitaka kipi asome namna gani!?

Hawataonewa huruma kwa sababu Madai yako yanapanga kudhoofisha hadhi ya Vyuo Vikuu vya Nchi yetu
Kila mtu anazo akili lakini wenye akili timamu sio watu wote. Serikali imefanya utafiti wa kina ikaona kuwa mtoto mwenye ufaulu wa DDD kwenye Physics, Biology na Chemistry anaweza kusoma kozi ya udaktari na yule mwenye ECD anaweza kusoma unesi akafaulu. Chuo kikuu Cha serikali hakiwezi kupingana na ukweli huo kutoka serikalini. Aliyesema MUHAS lazima ichukue watu wenye AAA TU ni nani? Hata hivyo twende tukafanye scrutiny kwenye applicants wote tuone ni watoto wangapi wa watanzania wa kawaida kutoka shule za serikali wenye division I waliokoseshwa nafasi kwenye vyuo vyao vya serikali. Tukaone pia ni watoto wangapi wenye uwezo wa kulipa vyuo vya binafsi lakini wamejibanza kwenye vyuo vya bei nafuu vya serikali na kuwakosesha wenzao maskini nafasi ya kusoma vyuo nafuu vya serikali. Hii ni dhambi kubwa sana kupita dhambi ya kuua mtu na tembo. Mzazi wa mtoto huyu aliyesoma shule za serikali kuanzia chekechea hadi A level na kukosa nafasi kwenye chuo Cha serikali atakwenda kuuza kila kitu ili kumsomesha mtoto huyu chuo binafsi wakati yule mzazi mwenye hela aliyepeleka mwanae chuo Cha bei nafuu Cha serikali atatumia hela yake aliyookoa kwa mambo mengine ya maendeleo au anasa. Hii itaendelea kupanua pengo la kati ya walionacho na wasionacho.
 
Haya mambo ya kurejesha siasa kwenye mambo yasiyohitaji siasa ni hatari sana...Mpaka hapa hata hivyo vyuo vya serikali havipo vizuri then mnataka viharibike zaidi ya hapa? Walimu wa vyuo vikuu wanajitolea sana sana pamoja na kuwa wanaanza kudharauliwa na soon tutarudi huko huko kwenye hizo shule za chini kwa ubora; majuzi serikali imeongeza posho kwa viongozi na kumpa mwl wa chuo ambaye amesoma miaka mingi posho ya chini kuliko hata ambao anawazidi kwa vyeo, hilo hatuliangalii...Kinachotoa morale pekee ni mishahara ambayo hata hivyo inaendelea kupungua siku baada ya siku kwasababu hizi hizi za watawala kutochukulia maanani mambo ya msingi...Well haya mambo ya siasa tafadhalini msiyapeleke kwenye vyuo vyetu vikuu
Hii sio siasa kaka bali ni kufa na kupona, watanzania hali zao ni mbaya sana kiuchumi, ndio maana CCM ikaja na sera ya elimu bure. Huyu aliyesoma bure Sasa vyuo vyao vinakwenda kukaliwa na watoto ambao hawakupenda kusomeshwa bure na serikali kwakuwa Wanazo pesa. Ni heri hawa wa private waendelee na mkondo wao wa private ili wale watoto wa maskini waendelee ku enjoy elimu nafuu vyuoni. Serikali lazima ijieleze ni kwa vipi mtoto aliyesoma bure shule za awali ghafla awe na uwezo wa kusoma chuo Cha 7m kwa mwaka? Are we realistic? Are we mad?
 
Elimu ndio chombo pekee kinachoweza kuwakutanisha mtoto wa tajiri na mtoto wa maskini katika ofisi moja na mgahawa mmoja. Takwimu zinaonyesha kuwa shule binafsi za msingi na sekondari nchini ni ghali kuliko za serikali lakini ndizo zenye mazingira mazuri ya kujifunzia na kutoa ufaulu mkubwa kwa wanafunzi wengi.

Na vyuo vikuu vya Serikali ni nafuu kusoma lakini ndivyo vyenye mazingira mazuri na miundombinu ya kufundishia na watoto kupata taaluma ya uhakika. Mpaka hapo hatubishani na hakuna ubishi.

Dhambi inakujaje wakati wa udahiri wa wanafunzi?
1. Vyuo vya serikali vinatoza ada ndogo sana lakini vinadahiri wanafunzi wenye ufaulu mkubwa sana(e.g Muhimbili University), bila shaka wengi wa wanafunzi wenye sifa hizi wengi wao ni wale wanaotoka kwenye shule za binafsi za sekondari kama FEZA, kanosa, etc.

Wazazi wa watoto hawa wengi wao ni wale wenye uchumi wa juu na wakati nchini ambao wanafahamu kuwa vyuo vya serikali vina walimu bora na miundombinu mizuri ya elimu, hivyo pamoja na kuwa na uwezo mkubwa wa kifedha wa kuendelea kuwasomesha watoto vyuo binafsi nchini na nje ya ya nchi lakini hawawapeleki watoto wao kwenye vyuo binafsi nchini kwakuwa wanavijua kuwa hata walimu wao ni wazee waliochoka na vijana wasiokuwa na uwezo mkubwa wa kufundisha.

2. Vyuo vya binafsi havina miundombinu mizuri ya kufundishia (walimu, madarasa, practice, library, office, ect) lakini vinatoza ada kubwa sana ili kumudu kulipa mishahara ya watumishi, majengo, na tozo mbalimbali za serikali. Pamoja na ughali wa vyuo hivi lakini Watoto wa maskini waliosoma shule za serikali wanajikuta wakisukumiwa kwenye aina hii ya vyuo baada ya kukosa nafasi kwenye vyuo vya serikali vyenye ada ambayo wazazi wangeimudu kulipa japo pia kwa tabu.

Kadhia hii inasababisha mambo mabaya sana kwa watoto na wazazi wao zikiwemo za wazazi kuuza kila kitu yaani kila kitu cha familia ili kumudu ada ya mtoto mmoja kwenye chuo binafsi, watoto kukosa mitihani na kuacha shule kwa kukosa ada, wanafunzi kujiingiza kufanya vitendo vibaya vya kuuza mili na madawa au kufanya biashara na wizi ili kusaidia wazazi wao kujaza kile kinachokosekana kwenye gharama za vyuo binafsi.

3. Fedha ya serikali (loans board) inapotea bure kwa watoto hawa kwenye vyuo binafsi. Yaani mtoto anaacha chuo katikati kwa kukosa kulipa kiasi cha ada kujalizia kile cha mkopo alichopewa na loans board. Watoto hawa wanateseka sana vyuoni kwasababu wanalazima kutumia ile meals and accommodations wanayopewa kwa kulipia ada zao. Mtoto akiacha masomo maana yake hata kiasi alichokopeshwa na loans board kimepotea pia.

4. Scholarships na mikopo vinaangalia ufaulu wa mtoto bila kuangalia mtoto kasoma shule gani. Hii inamaanisha kuwa wenye nacho wataongezewa pia hapa. Yaani watoto wa wenye nacho ndio waliosoma shule za private na wengi ndio wenye ufaulu mkubwa kuweza kuwa na sifa za kupata scholarships na mikopo.

5. Mtoto wa Maskini hatakutana na mtoto wa tajiri ofisi moja kama trend itakuwa hiihii.

Hapa ni ama;
Shule za Serikali pia ziongezewe ubora katika kutoa elimu, vyuo vya private vipewe ruzuku na serikali ili ada yao pia iwe himilivu au vyuo vya serikali vihudumie zaidi shule za serikali.

Mifumo ya Serikali lazima isomane, haiwezekani vyuo vya serikali na shule za serikali hiyohiyo havisomani, yaani shule za serikali zinazalisha watoto wasiotakiwa na vyuo vya serikali.
Bado nchi inahitaji ukombozi wa maskini

Ni Nyerere tu ndiye aliwaza kuwapa elimu maskini.Ndiye alitaka kila familia iwe na mtu mwenye degree.

Hapa ni kazi bure,maskini haangaliwi
 
Dawa ni vijana kuandamana kupiga ubaguzi wa kielimu

Hakuna waziri wala serikali itakayofanya mageuzi kwa hiyari yake yenyewe lazima kuwepo na pressure kutoka kwa wadau wenyewe yaani maelfu ya wanafunzi wawepo mbele ktk maandamano ya kudai mabadiliko ya mfumo wa elimu.

20 May 2022
Kigoma, Tanzania

WANAFUNZI WAANDAMANA HADI KWA MKUU WA WILAYA ''KILA SIKU MAHARAGE,HATUNA MAJI NA HATUSOMI''

Source: millard ayo

NA HUKO NCHI JIRANI :

Beni, Congo DR

Wanafunzi waandamana wamtaka Rais Tshisekedi afike Beni​

23 Aprili, 2021
Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari mjini Beni, Kivu kaskazini, mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia wameandamana na kumtaka Rais Tshisekedi kufika na kulitafutia ufumbuzi suala la amani yao ikiwa siku ya tatu tangu wanafunzi hao kuweka kambi katika ofisi ya Meya wa Beni. Source : Wanafunzi waandamana wamtaka Rais Tshisekedi afike Beni
 
Gabriel Boric on the Chilean student movement 14 June 2017

Gabriel Boric on the Chilean Student Movement

Likes
59,554
Views
2017
14 Jun
In a presentation at the School of Public Policy on June 7, 2017; Gabriel Boric offers a historical perspective and reflects on lessons learned. He focuses especially on the role of social movements in a well-developed democracy and provides insights on how to sustain collective action over an extended period of time. He speaks also about his transition from being a member of a political movement to being a member of Parliament. Gabriel Boric is a Chilean parliamentarian, and a former leader of the national student movement. He was the president of the Student Federation of the Universidad de Chile, one of the most important student unions in the country. Boric currently represents the Magallanes and Antarctic Region in Chile’s Chamber of Deputies. He was elected as an independent candidate and is not associated with either one of the two political coalitions that have traditionally dominated politics in Chile. Source:

Department of Public Policy at CEU​

Mwanafunzi wa chuo kikuu toka familia masikini anazama ktk mkondo wa madeni ya fedha za mkopo wa elimu ya juu huku akiwa na matumaini potofu ya kupata ajira au kuwepo mazingira hewa ya kujiajiri.

Vijana vyuo vikuu na mijini pia vijijini badala ya kumezwa na ukiritimba wa UVCCM na ahadi kuwa ni viongozi wa kesho huku watoto wa vigogo wa CCM wanapewa nafasi sasa na siyo kesho wanatakiwa kuunda chombo chao kipya cha kutambulika kama mdau muhimu anayehitaji kuonekana katika majukwaa ya siasa pia ktk vituo vya redio, televisheni na mitandao ya kijamii kuchagiza mabadiliko na mageuzi ikiwemo pia kupewa nafasi nje ya mfumo wa vyama ili wagombee nafasi za kuchaguliwa na wananchi.

Gabriel Boric - The 100 Most Influential People of 2022 - TIME

time.com › collection › gabriel-boric

gabriel boric presidente from time.com
23 May 2022 · He is making Chile the social, economic, and political laboratory of the world once again. Stiglitz is a Nobel Prize–winning economist
 
Elimu juu ya uombaji wa vyuo ni muhimu sana. Kuwa na ufaulu mkubwa pekee yake haitoshi kukupa nafasi ya kupata chuo na degree program uliyoomba. Kuna vigezo vingi, ikiwa ni pamoja na competativeness ya chuo na degree husika ndani ya chuo. Kuna wakati hadi matokeo ya form four hutumika kuamua nani achukuliwe na nani aachwe. Kuna degree program fulani ndani ya chuo fulani capacity ya chuo kuchukua hao wanafunzi ni 30 tu, sasa ebu niambie, kwa wanafunzi wa form six kuna wenye one ya 7 wangapi? Bila shaka wako maelfu kwa maelfu.
Kwenye vyuo vya serikali akili ya kawaida itakwambia kuwa huko ndiko watakaoishia watoto wa watanzania waliopewa elimu bure kule chekechea, shule za msingi na sekondari na serikali yao sikivu. Hivyo common sense inakwambia kuwa kama watoto 2 wamelingana kwa sifa ya ufaulu aliyesoma shule ya serikali lazima apewe priority kwenye hiyo nafasi, kwakuwa yeye anazo options chache sana za kuendelea na masomo ya elimu ya juu kama hatapata nafasi kwenye chuo cha serikali. Hii sio siasa ni ukweli uliothibitishwa na serikali kwa kuondoa ada kwenye shule za serikali.

Serikali kama inataka kuviacha vyuo vyake vichague kama vinavyotaka basi vitalazimika kutoa ruzuku kwa vyuo binafsi ili ada zao zifanane na vyuo vyake vya serikali. yaani serikali ichukue gharama za kulipa walimu na kusamehe kodi kwenye baadhi ya mambo kwenye vyuo binafsi ili uwanja uwe sawa pande zote.
 
Gabriel Boric on the Chilean student movement 14 June 2017

Mwanafunzi wa chuo kikuu toka familia masikini anazama ktk mkondo wa madeni ya fedha za mkopo wa elimu ya juu huku akiwa na matumaini potofu ya kupata ajira au kuwepo mazingira hewa ya kujiajiri.

Vijana vyuo vikuu na mijini pia vijijini badala ya kumezwa na ukiritimba wa UVCCM na ahadi kuwa ni viongozi wa kesho huku watoto wa vigogo wa CCM wanapewa nafasi sasa na siyo kesho wanatakiwa kuunda chombo chao kipya cha kutambulika kama mdau muhimu anayehitaji kuonekana katika majukwaa ya siasa pia ktk vituo vya redio, televisheni na mitandao ya kijamii kuchagiza mabadiliko na mageuzi ikiwemo pia kupewa nafasi nje ya mfumo wa vyama ili wagombee nafasi za kuchaguliwa na wananchi.

Gabriel Boric - The 100 Most Influential People of 2022 - TIME

time.com › collection › gabriel-boric

gabriel boric presidente from time.com
23 May 2022 · He is making Chile the social, economic, and political laboratory of the world once again. Stiglitz is a Nobel Prize–winning economist

Mtoto ambae hakusoma shule za serikali hawezi kuwa kiongozi mzalendo hata siku moja. Fanya utafiti, viongozi ambao ni mafisadi na vibaraka wa wageni wengi wao hawakusoma shule na vyuo vya serikali.
 
Udahili wa chuo kigezo ni kimoja tu, ufaulu wa mwanafunzi. Hizo nyingine za sijui kipato cha mzazi ni siasa!

Jambo la muhimu ni bodi ya mikopo itoe mikopo kwa wote wanao omba. Mtu mzima anaomba mkopo maana yake anauhitaji, waaache ujinga wao.
kaka mtoto anaesoma chuo binafsi kozi ya miaka 5 atahitaji mko wa sh. 10m x 5 = 50,000 tution fee na stationary tu wakati yule anaesoma shule ya serikali atahitaji mkopo wa shi 3m x 5 = 15,000 tu. Wote hawa wanakwenda kuhudumia watanzania baada ya masomo yao.
 
Huu ubaguzi ulihubiriwa Sana jiwe. Enzi hizi za mama Samia tunaongelea usawa. Na usawa ktk elimu unaletwa na ufaulu. Vyuoni wanaangalia ufaulu haijalishi ulisomea wapi
lengo la elimu ni hatimae akatoe huduma (hands on). Tunataka uje na takwimu hapa zinazoonyesha kuwa watoto waliongia vyuo vikuu wakiwa na division one ya points 3 wako vizuri kazini kuliko walioingia na division I ya points 7 au division II. Lakini watu wanasema "like dissolve like" shule za serikali lazima zitegemee vyuo vya serikali zaidi. Ni pale tu ambapo nafasi serikalini ipo ndio mtoto wa private apate nafasi serikalini
 
Vyuo binafsi vimefikia ada milioni 7 ? Aisee nipo nje ya dunia basi
 
Mkuu ni bahati mbaya kwamba hiki unachokisema hakipo na hakitakaa kiwepo, siku kikiwepo basi tutakuwa tumefikia pabaya zaidi. Admission za vyuo hazitolewi kama hisani bali kwa merits. Ni bahati mbaya pia kwamba kuwachukua waliofeli kisa wametoka shule za kayumba sio kuwasaidia. Wengi hawa utakuwa unawapeleka kwenye moto bila sababu. Usisahau disco ni jambo la kawaida kwenye hivi vyuo unavyotaka viwape waliofeli nafasi. Ni vema vikaendelea kupokea watu wenye uwezo na kwa hapa hakuna kipimo kingine zaidi ya ufaulu wa mitihani yao ya form four na six.
Unapotosha mdau, sifa za kujiunga na vyuo kwa kozi mbalimbali zimewekwa na serikali sio na vyuo wala mtu binafsi, mdau wa kwanza kutekeleza sifa hizo kama zilivyo lazima viwe ni vyuo vikuu vya serikali. Kama watoto wenye sifa hizo hawapo ndio waende wakatafute sehemu nyingine (private na nje ya nchi). Sasa huwezi kusema kuwa nataka vyuo visajili watoto wasio na sifa sijui nini. serikali ina shule zake na vyuo vyake, hivyo shule na vyuo lazima viongee lugha moja. Kinachoonekana vyuo vya serikali havipendi kuongea lunga moja na shule za serikali. Kuna watanzania wenzetu hawataki shule za serikali lakini wanataka vyuo vya serikali, hii haikubaliki kwa mustakabali wa taifa letu wa kujenga uzalendo, umoja na mshikamano. Yaani hii ni sawa na mtu mnapigana halafu yeye anakimbilia korodani zako tu basi, hivyo hata kama wewe una nguvu kiasi gani na umefanya mazoezi kiasi gani ni lazima atakushinda tu maana korodani hazifanyi mazoezi ya aina yoyote. Hawa wanaosomesha watoto wao shule bora kwa pesa nyingi ili wapate nafasi za kwanza kule kwenye shule nafuu za serikali ni sawa na kuwaminya korodani wale waliosota kwenye shule za serikali.
 
Back
Top Bottom