Waziri Prof. Mkenda dhambi hii ya udahili vyuoni isisubiri tamko la Rais Samia

Waziri Prof. Mkenda dhambi hii ya udahili vyuoni isisubiri tamko la Rais Samia

Udahili wa chuo kigezo ni kimoja tu, ufaulu wa mwanafunzi. Hizo nyingine za sijui kipato cha mzazi ni siasa!

Jambo la muhimu ni bodi ya mikopo itoe mikopo kwa wote wanao omba. Mtu mzima anaomba mkopo maana yake anauhitaji, waaache ujinga wao.
Serikali badala ya kutoa mikopo ya kutosha kwa wanavyuo eti wanajificha kwa wanafunzi wa kidato cha 5 na 6 kuwasomesha bure.
 
shule za private zinakaririsha maswali, zinaiba mitihani, zinaonyesha mitihani, wako wachache darasani, nk huko ni rahisi kuwapata watoto wenye ufaulu wa hivyo, je, shule za umma hazitaki watoto kutoka shule za umma? ni watoto wangapi kutoka shule za umma wana ufaulu wa point 3, 4 na 5? bogus
Una ushahidi na hizi tuhuma Ndugu kuwa wanaiba Mitihani na kukaririshana? Mwenyewe umesema wana mazingira mazuri ya kujifunzia

Wapo wengi tu pia wanafunzi wa shule za serikali wanaofaulu vizuri na kuwazidi hao wa Shule za Private

Acha Hasira maana umemaliza kwa Hamaki kubwa sijajua tatizo nini
Binafsi nimeona kwa macho mtoto aliyesoma shule ya serikali ya kata na kupata division 1 points 7 masomo ya sayansi (PCB) lakini amekosa udahiri chuo Cha serikali.
Huyu alama zake za Advance hazikumtosha kuchaguliwa vyuo unavyovitaka. Kumbuka wapo waliopata hayo matokeo O-Level na wakayapata kama hayo A-Level wakaingia Muhimbili kama kawaida

Aliyepunguza speed kwenye Cut-off Points hana pa kupita ndugu maana nafasi yake ina mwingine aliyemzidi
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Una ushahidi na hizi tuhuma Ndugu kuwa wanaiba Mihihani na kukaririshana? Mwenyewe umesema wana mazingira mazuri ya kujifunzia

huwezi kumkataa mwanao eti kwakuwa ana upele, chuo cha umma kumkataa mtoto wa aliyetoka shule ya umma eti kwakuwa hana division I ya point 3, 4 na 5 ni uhujumu uchumi. Hizo shule za serikali za vipaji maalumu zinafahamika, hebu tuzitembelee zote ili tuone ufaulu wao kwa ujumla tuone kama tunaweza kupata wanafunzi 600 wenye ufaulu wa division I ya points 3, 4, na 5 wanaohitakiwa na Muhimbili chuo cha umma. Twende tukaone udahiri wao mwaka huu kwa first year 2022/2023 ili tuone kama watoto wangapi wa wakulima, wamachinga na waoka vitumbua wamo humo kwenye orodha yao. Kaka hapa kuna uhujumu mkubwa wa walalahoi, maana watoto wao waliosomeshwa bure na serikali na kupata ufaulu wa division 1 za points 6, 7, 8, 9 na division II na III watalazimika kwenda kuparangana huko kwenye vyuo ambavyo vinawapokea lakini kwa ada ya sh. 7.0 milioni kwa mwaka.
 
Elimu ndio chombo pekee kinachoweza kuwakutanisha mtoto wa tajiri na mtoto wa maskini katika ofisi moja na mgahawa mmoja. Takwimu zinaonyesha kuwa shule binafsi za msingi na sekondari nchini ni ghali kuliko za serikali lakini ndizo zenye mazingira mazuri ya kujifunzia na kutoa ufaulu mkubwa kwa wanafunzi wengi.

Na vyuo vikuu vya Serikali ni nafuu kusoma lakini ndivyo vyenye mazingira mazuri na miundombinu ya kufundishia na watoto kupata taaluma ya uhakika. Mpaka hapo hatubishani na hakuna ubishi.

Dhambi inakujaje wakati wa udahiri wa wanafunzi?
1. Vyuo vya serikali vinatoza ada ndogo sana lakini vinadahiri wanafunzi wenye ufaulu mkubwa sana(e.g Muhimbili University), bila shaka wengi wa wanafunzi wenye sifa hizi wengi wao ni wale wanaotoka kwenye shule za binafsi za sekondari kama FEZA, kanosa, etc.

Wazazi wa watoto hawa wengi wao ni wale wenye uchumi wa juu na wakati nchini ambao wanafahamu kuwa vyuo vya serikali vina walimu bora na miundombinu mizuri ya elimu, hivyo pamoja na kuwa na uwezo mkubwa wa kifedha wa kuendelea kuwasomesha watoto vyuo binafsi nchini na nje ya ya nchi lakini hawawapeleki watoto wao kwenye vyuo binafsi nchini kwakuwa wanavijua kuwa hata walimu wao ni wazee waliochoka na vijana wasiokuwa na uwezo mkubwa wa kufundisha.

2. Vyuo vya binafsi havina miundombinu mizuri ya kufundishia (walimu, madarasa, practice, library, office, ect) lakini vinatoza ada kubwa sana ili kumudu kulipa mishahara ya watumishi, majengo, na tozo mbalimbali za serikali. Pamoja na ughali wa vyuo hivi lakini Watoto wa maskini waliosoma shule za serikali wanajikuta wakisukumiwa kwenye aina hii ya vyuo baada ya kukosa nafasi kwenye vyuo vya serikali vyenye ada ambayo wazazi wangeimudu kulipa japo pia kwa tabu.

Kadhia hii inasababisha mambo mabaya sana kwa watoto na wazazi wao zikiwemo za wazazi kuuza kila kitu yaani kila kitu cha familia ili kumudu ada ya mtoto mmoja kwenye chuo binafsi, watoto kukosa mitihani na kuacha shule kwa kukosa ada, wanafunzi kujiingiza kufanya vitendo vibaya vya kuuza mili na madawa au kufanya biashara na wizi ili kusaidia wazazi wao kujaza kile kinachokosekana kwenye gharama za vyuo binafsi.

3. Fedha ya serikali (loans board) inapotea bure kwa watoto hawa kwenye vyuo binafsi. Yaani mtoto anaacha chuo katikati kwa kukosa kulipa kiasi cha ada kujalizia kile cha mkopo alichopewa na loans board. Watoto hawa wanateseka sana vyuoni kwasababu wanalazima kutumia ile meals and accommodations wanayopewa kwa kulipia ada zao. Mtoto akiacha masomo maana yake hata kiasi alichokopeshwa na loans board kimepotea pia.

4. Scholarships na mikopo vinaangalia ufaulu wa mtoto bila kuangalia mtoto kasoma shule gani. Hii inamaanisha kuwa wenye nacho wataongezewa pia hapa. Yaani watoto wa wenye nacho ndio waliosoma shule za private na wengi ndio wenye ufaulu mkubwa kuweza kuwa na sifa za kupata scholarships na mikopo.

5. Mtoto wa Maskini hatakutana na mtoto wa tajiri ofisi moja kama trend itakuwa hiihii.

Hapa ni ama;
Shule za Serikali pia ziongezewe ubora katika kutoa elimu, vyuo vya private vipewe ruzuku na serikali ili ada yao pia iwe himilivu au vyuo vya serikali vihudumie zaidi shule za serikali.

Mifumo ya Serikali lazima isomane, haiwezekani vyuo vya serikali na shule za serikali hiyohiyo havisomani, yaani shule za serikali zinazalisha watoto wasiotakiwa na vyuo vya serikali.
Mkuu mwandae mtoto vizuri. Kama atakariri sawa, kama atataka aelewe sawa pia. Ila mtihani watafanya uleule. Udahili chuo kwa Tanzania, kigezo kikubwa na pekee kilichopo ni ufaulu tu wa level yako ya chini. Hawana interview wala kuita kuchunguza hali zenu za kiuchumi.
 
Wazo zuri.

Kikubwa labda kuwe na grants. Ila ada za vyuo vya umma ziendane na vyuo vya Serikali.
 
Sexless serikali imeshaweka ufaulu wa nani aende chuo kikuu na nani hawezi kwenda chuo kikuu. huyo mtoto aliyefeli kwa kula bangi atakosa nafasi chuo kikuu kwakuwa nafasi yake imejazwa na wenzake kutoka shule za serikali ambao waña ufaulu unaotakiwa.

Bodi ya chuo, mkuu wa chuo na makamu mkuu wa chuo wa vyuo vya serikali wanalazimika kuisoma sera ya elimu na ilani ya Chama na kutekeleza yaliomo. Mkuu wa chuo Cha serikali lazima afahamu yanayotokea kwenye ngazi za chini za elimu kuanzia chekechea, msingi na sekondari ili visomane na vyuo vikuu wananavyoviongoza. Huwezi kujaza vyuo vya serikali kwa kudahiri wanafunzi kutoka private schools kwasababu Wana ufaulu mkubwa. Mkuu na makamu wa chuo wa aina hii yafaa kutimuliwa kazi mara moja,
 
Wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu muanzishe harakati za kudai mnayodhani hayafanyiki sawa.

Wenzenu ktk nchi zingine huongoza mabadiliko kwa kujiundia students Union ambazo hazitegemei UVCCM, CCM au chama chochote kinachoongozwa na wanasiasa wawatetee hali zenu ngumu.
Soma hapa chini : source :
 
Matumaini ya kuteuliwa katika kinachoitwa 'mkeka' ukiwa wewe ni mwanachama wa UVCCM imewapofusha vijana wengi.

Muda sasa umefika wajiondoe ktk mfumo huu jinamizi unaowalemaza vijana ambao unawaweka pembeni wasiweze kufanya maamuzi na kubakia watazamaji waimba mapambio na kusifu wazee wa CCM

16 December 2021
Dar es Salaam, Tanzania

Tazama Nguvu Ya UVCCM Kwenye Mkutano Mkuu Wa Umoja Wa Vijana | Tawi La DIT _ Dar es Salaam Tanzania

Kumbe wale waliosoma shule za FEZA, KEMEBOS, BABRO na wale wa kupelekwa na school bus nao wanaishia vyuo hivi hivi vya hapa nchini kama st Kayumba? Nilojua safari yao ni Oxford, Yale, Havard n.k

Oxford, yale, havard hazitaki necta hata uwe umepata 100 masomo yote.

Soma IST fanya vizuri havard , yale , oxford watakupokea ila sio necta
 
Achana naye. Kwahiyo anataka vyuoni waende mateja?
Kwahiyo shule za serikali Zina mateja? Hayo mateja ya serikali Wacha yaende kwenye vyuo vyao vya serikali yakavikaze kwanza. Ni ujinga mama kumnyonyesha mtoto wa jirani na kumwacha mtoto wake afe njaa. Kuwaacha watoto wa maskini wakasome vyuo binafsi kunasigana na sera ya elimu bure.
 
Una ushahidi na hizi tuhuma Ndugu kuwa wanaiba Mihihani na kukaririshana? Mwenyewe umesema wana mazingira mazuri ya kujifunzia

Wapo wengi tu pia wanafunzi wa shule za serikali wanaofaulu vizuri na kuwazidi hao wa Shule za Private

Acha Hasira maana umemaliza kwa Hamaki kubwa sijajua tatizo nini

Huyu alama zake za Advance hazikumtosha kuchaguliwa vyuo unavyovitaka. Kumbuka wapo waliopata hayo matokeo O-Level na wakayapata kama hayo A-Level wakaingia Muhimbili kama kawaida

Aliyepunguza speed kwenye Cut-off Points hana pa kupita ndugu maana nafasi yake ina mwingine aliyemzidi
Wacha urongo wewe, nenda kaangalie MUHAS wamedahiri wanafunzi wenye ufaulu gani mwaka huu 2022/23 halafu ndio uje uchangie Uzi huu. Ulitaka wale wanafunzi wa Kamsamba high high school waende wakasome wapi? Vyuo vya serikali lazima vitafsiri sera na mipango ya serikali kwenye elimu.
 
Vyuo vikuu vya serikali ndiko wanakotayarishwa wazalendo wa nchi hii, huwezi kupata mzalendo nje ya mfumo wa serikali. Usitarijie kumpata mzalendo kindakindki aliyetoka nje ya shule za serikali. Mtoto aliyejisomesha kwa mateso shule na vyuo binafsi kwa ada kubwa kamwe hawezi kuwa mzalendo lialia wa taifa.
 
Jambo la muhimu ni kuifuta loan board ili serikali itumie utaratibu wa awali ambapo ilikuwa inatoa ufadhili kwa wanafunzi waliokuwa wakidahiliwa kwenye vyuo vya umma kupitia wizara ya elimu. Endapo loan board itaendelea kuwepo basi ihusike zaidi na vyuo vya binafsi. Pia mazingira ya utoaji wa elimu ya msingi na sekondari kwa shule za serikali yaendelee kuboreshwa. Hii italeta ushindani sawa kati ya watoto wa matajiri na watoto wa wanyonge kwenye kupambania nafasi za udahili katika vyuo vya umma ambako watakuwa wanapata ufadhili (grants) ambazo zinatokana na kodi za wananchi.​
Umeongea ki facts zaidi...Kama vyuo vya serikali ni bora kuliko binafsi, kwanini shule za serikali zisiwe bora zaidi kuliko binafsi?

Mbona enzi za Mwl JKN shule za serikali zilikuwa bora kuliko za binafsi? Waziri aache kuleta majibu mepesi kwenye mambo complex. Kinachotakiwa ni integration ya mambo mengi na siyo isolations anazotaka kuzileta ambazo zitavuruga zaidi mifumo kama ambavyo waliomtangulia waliivuruga kwakufanya mambo kisiasa badala ya kutumia utaalamu na utawala bora.

Kitu kinachofanya shule za serikali kuwa za hovyo ni mpangilio wa matumizi mabovu ya viongozi wa serikali kwenye fedha za umma, ambazo wanazitumia kufanya luxry wao binafsi na kusahau pesa hizo zilipaswa kutoa service bora kama mishahara ya waalimu, kutengeneza miundombinu bora ya elimu na afya i.e kutoa huduma na kutumia hizo pesa kuwaongoza raia kujiongezea mapato ili uchumi wa taifa uweze kuhimili kutoa huduma hizo za jamii. Viongozi wetu wamepindua mambo upside down, yeye kama mchumi itashangaza sana kama hata hili atalipeleka kisiasa badala ya kuleta suluhu ya kiuchumi.

Mzazi akishapata kipato kinachokidhi basic needs automatically hizo shule zitakuwa bora, huwezi ku penalize mzazi aliyejihimu kupata kipato kizuri kwa nguvu zake ili yule ambaye hana aweze kupata ahueni, this is against pareto efficiency, anachotuletea kama pendekezo ni kitu hatari sana, ni ubaguzi kama mwingine yeyote ule. You cannot decrease the welfare of others and make them worse off to uplift the life of the poor people....Hili hata JPM alilifanya na matokeo ndiyo uchumi ukaelekea kibla, nampenda sana JPM ila kwenye maamuzi haya alivuruga uchumi wa nchi kwa ushauri mbaya wa wachumi wa enzi hiyo yake, na leo watu wale wale wanataka kuleta majanga mengine kwakutafuta majibu mepesi kwenye maswala complex, lets stop this discrimination....Waziri kama mchumi asaidie taifa kuleta majibu ambayo hayata athiri raia yeyote wa nchi hii ili kumwokoa mwingine; la kwanza likiwa kupunguza spending zao zisizo wiana na kasi wala thamani ya mchango wao kwenye kuongeza uchumi wa taifa.
 
shule za private zinakaririsha maswali, zinaiba mitihani, zinaonyesha mitihani, wako wachache darasani, nk huko ni rahisi kuwapata watoto wenye ufaulu wa hivyo, je, shule za umma hazitaki watoto kutoka shule za umma? ni watoto wangapi kutoka shule za umma wana ufaulu wa point 3, 4 na 5? bogus
Tatizo unatatua tatizo kwakuondoa matokeo/matunda na kuacha mizizi inayoizalisha, a very poor way of solving problems
 
Tatizo hapa kubwa kuliko zote ni ku commoditize elimu badala ya kuitoa kama public good...nchi zote za kiberi zimeharibu mifumo ya elimu zao ambapo wamezalisha makundi kama haya na sisi sijui nani alitudanganya tukafanya hicho kituko...Public goods zina tabia ya kuleta externalities kama hizi ndiyo sababu ubaguzi huu huwezi kuukuta nchi nyinhi za Europe ambapo elimu yao inakuwa heavily subsidized...Huu umakundi wa wenye nacho kuongezewa unaukuta nchi zenye ubepari yaani U.K na USA....Hawa ndiyo waluovuruga mifumo ya elimu na kama ambavyo US wametaka kuvuruga na mifumo ya afya kwakuruhusu afya kuhudumiwa na makampuni ya kibepari hadi kupelekea kusababisha conspiracies za hayo kutengeneza magonjwa au kusababisha magonjwa ili kampuni zao za madawa ziweze kuuza sana....Lazima sisi kama mataifa yanayoendelea tukataye kuifanya elimu kuwa commodity na hili haliwezekani kama spending ya government kwenye welfare ya viongozi itaendelea kuwa hii ya ki royal wakati watu wao hawana basics
 
serikali imeshaweka ufaulu wa nani aende chuo kikuu na nani hawezi kwenda chuo kikuu. huyo mtoto aliyefeli kwa kula bangi atakosa nafasi chuo kikuu kwakuwa nafasi yake imejazwa na wenzake kutoka shule za serikali ambao waña ufaulu unaotakiwa.

Bodi ya chuo, mkuu wa chuo na makamu mkuu wa chuo wa vyuo vya serikali wanalazimika kuisoma sera ya elimu na ilani ya Chama na kutekeleza yaliomo. Mkuu wa chuo Cha serikali lazima afahamu yanayotokea kwenye ngazi za chini za elimu kuanzia chekechea, msingi na sekondari ili visomane na vyuo vikuu wananavyoviongoza. Huwezi kujaza vyuo vya serikali kwa kudahiri wanafunzi kutoka private schools kwasababu Wana ufaulu mkubwa. Mkuu na makamu wa chuo wa aina hii yafaa kutimuliwa kazi mara moja,
Haya mambo ya kurejesha siasa kwenye mambo yasiyohitaji siasa ni hatari sana...Mpaka hapa hata hivyo vyuo vya serikali havipo vizuri then mnataka viharibike zaidi ya hapa? Walimu wa vyuo vikuu wanajitolea sana sana pamoja na kuwa wanaanza kudharauliwa na soon tutarudi huko huko kwenye hizo shule za chini kwa ubora; majuzi serikali imeongeza posho kwa viongozi na kumpa mwl wa chuo ambaye amesoma miaka mingi posho ya chini kuliko hata ambao anawazidi kwa vyeo, hilo hatuliangalii...Kinachotoa morale pekee ni mishahara ambayo hata hivyo inaendelea kupungua siku baada ya siku kwasababu hizi hizi za watawala kutochukulia maanani mambo ya msingi...Well haya mambo ya siasa tafadhalini msiyapeleke kwenye vyuo vyetu vikuu
 
Elimu juu ya uombaji wa vyuo ni muhimu sana. Kuwa na ufaulu mkubwa pekee yake haitoshi kukupa nafasi ya kupata chuo na degree program uliyoomba. Kuna vigezo vingi, ikiwa ni pamoja na competativeness ya chuo na degree husika ndani ya chuo. Kuna wakati hadi matokeo ya form four hutumika kuamua nani achukuliwe na nani aachwe. Kuna degree program fulani ndani ya chuo fulani capacity ya chuo kuchukua hao wanafunzi ni 30 tu, sasa ebu niambie, kwa wanafunzi wa form six kuna wenye one ya 7 wangapi? Bila shaka wako maelfu kwa maelfu.
Binafsi nimeona kwa macho mtoto aliyesoma shule ya serikali ya kata na kupata division 1 points 7 masomo ya sayansi (PCB) lakini amekosa udahiri chuo Cha serikali.
 
Mkuu ni bahati mbaya kwamba hiki unachokisema hakipo na hakitakaa kiwepo, siku kikiwepo basi tutakuwa tumefikia pabaya zaidi. Admission za vyuo hazitolewi kama hisani bali kwa merits. Ni bahati mbaya pia kwamba kuwachukua waliofeli kisa wametoka shule za kayumba sio kuwasaidia. Wengi hawa utakuwa unawapeleka kwenye moto bila sababu. Usisahau disco ni jambo la kawaida kwenye hivi vyuo unavyotaka viwape waliofeli nafasi. Ni vema vikaendelea kupokea watu wenye uwezo na kwa hapa hakuna kipimo kingine zaidi ya ufaulu wa mitihani yao ya form four na six.

Back
Top Bottom