Waziri Prof. Mkenda dhambi hii ya udahili vyuoni isisubiri tamko la Rais Samia

"like dissolve like" shule za serikali
Umeitumia mahala ambapo sipo hii kanuni. Hata shule za private ni za serikali pia. Diania ya leo serikali haiwezi ikafanya kila kitu ndiyo maana kuna PPP policy.

Private zinaisaidia serikali pahala ambapo haiwezi. Kwahiyo ustake kuhalalisha ubaguzi wa kivipato.
 
Mtoto ambae hakusoma shule za serikali hawezi kuwa kiongozi mzalendo

Watoto waliotoka ktk familia zenye uwezo ndiyo wazalendo na, huongoza mabadikiko ya kweli.

Mwalimu Julius Nyerere mtoto wa chifu, Fidel Castro mtoto wa mkulima mkubwa 'bepari' listi ni ndefu
 
Halafu tunalalamika ndoa hazidumu siku hizi, wakati mama kaanza kudanga toka akiwa anasoma na baba naye kashazoea kulelewa asukume maisha mbele..!! Hali ni mbaya sana kwa kweli sijui tunaelekea wapi...???
 
Binafsi nimeona kwa macho mtoto aliyesoma shule ya serikali ya kata na kupata division 1 points 7 masomo ya sayansi (PCB) lakini amekosa udahiri chuo Cha serikali.
A level alipata ufaulu upi?
 
Weeee!!! nimeitumia kwa kumaanisha kabisa. Vyuo vikuu vya serikali ni vyombo vya serikali vinavyotakiwa kutafsiri kwa vitendo sera ya elimu nchini. Mnyororo wa thamani wa elimu unaanzia chekechea hadi vyuo vikuu vya serikali kwa slogan ya "garbage in garbage out". Ona vyuo vyetu vya serikali havitaki kunasibishwa na dhaifu wa products za shule zao za serikali, hivyo wanatafuta malighafi nje ya serikali,. Hata huko nchi za Magharibi shule na vyuo vya serikali sio vizuri sana kulinganisha na baadhi ya vyuo binafsi.
 
Mtoto wa masikini lazima apambane asome kweli kweli ili apate scholarship maana hii scholarship haijamlenga tajiri au masikini imemlenga mtoto wa mtanzania yeyote atakae faulu vizuri masomo ya sayansi
Watu wenye akili nyingi kama Nyerere alifahamu kuwa elimu ni silaha sawa na silaha nyingine za mass distraction. Ilimfanya achukue uamuzi mgumu sana kama wa kutaifisha shule binafsi na kumsomesha bure kila mtu ili kutengeneza umoja huu unaouona Leo. Watu kama nyinyi wenye mawazo kama haya ni magugu kwenye ustawi wa taifa, mmevaa miwani ya Mbao.

Kama utachunguza Sana Ile hofu ya Mwl Nyerere iliyomfanya azitaifishe zile shule zipo hadi Leo. Leo hii watu wenye uwezo wa kumsomesha mwanawe shule binafsi ni wale wenye ajira, na wafanyabiashara wakubwa na wakati. Ukiziangalia ajira zetu maofisini Zina harufu Fulani.
 
Kuna watoto wengi wapo Muhimbili, UDSM, Mzumbe, UDOM ambao wamesoma St Kayumba!
Suala ni kufaulu tu
Nilikupa thanks, lakini kwa maandishi nasema foolish! Muhimbili imejaa rushwa, nepotism, ukabila, na umwanga mshenzi tu! Kwa ufupi, watoto wa maskini kwa sasa hawataweza tena kusoma medicine.

Hilo jambo aliloandika mleta thrd liangaliwe na watu wenye akili siyo kila mwenye akaunti ya JF. Waziri na rais Samia wote wanajichanganya. Karibuni Waziri alisema kuna Samia Scholarships kwa wanafunzi wa sayansi je, anajua wanafaulu sayansi wanatoka shule gani? Ni aibu kufikia uwaziri lakini huna analytical brain zaidi ya ukorofi tu!

Hakuna mwanafunzi wa shule ya kata ya form 1-4 na 5-6 anayeweza kupata sholarship kama hiyo. Ni uzembe mkubwa kwa waziri anayejiita profesa kusihia kutaja ufauklu kama kigezo pekee cha haki ya kusoma.
 
Kwani hao watoto siyo watanzania? Why wabaguliwe? Msilete siasa kwenye mambo serious, kama ni kutoa elimu bora boresheni elimu kwakutumia kodi za raia na msisingizie watanzania ambao wana haki sawa awe ni tajiri au masikini...Mkose njia bora za kuleta maendeleo kwakukosa innovation na hiyo incapabilities zenu mzi project kwa watanzania? Kama mmeshindwa una resign from where you are and leave those who are capable to do apropriate things...
 
Watu mnaanza kutumia mabavu kuficha incapabilities zenu, watanzania kwanini wawe maskini? With all these resources watu mnawaita masikini, why? Ni wewe unayeshindwa ku translate hizi resources za watanzania kwa kukosa ubunifu na sera bora kuongeza welfare ya raia then you come forward crying like a baby eti watanzania masikini...Masikini ni wewe mwenye mawazo mafupi yasiyoweza kuongeza tija kwenye maisha ya watanzania na kwakua mtu hajui jinsi ya ku create wealth then anataka kila mtu awe victim wa circumstances anayo i create yeye kwakung'ang'ania ku ongoza hata pale asipokuwa na uwezo....hii nchi si mali ya mtu au kundi la watu, kila raia anahaki ya kusoma sehemu anayoiona inafaa ilimradi anakizi vigezo. Umasikini si criteria ya mtu kusoma au kutokusoma, mmelazimisha haya na sasa mambo yameparaganyika you come up with funny proposals za kibaguzi na kunyanyasa raia wasio na hatia.
 
Badala ya kuhoji kwanini mtoto wa masikini aliyesoma shule ya serikali asifaulu kama yule wa shule binafsi huku chini lakini the pattern inageuka elimu ya juu, you come with allegations badala ya facts?

I think you need to stop being naive like this, sorry unani provoke na uandishi wako kwakua unaonekana kupenda kuleta simple answers kwenye serious na critical issues
 
Ahsante kwa mchango wenye tija kwa taifa letu...
 
Hao watoto walijibagua wao wenyewe na wazazi/walezi wao, waliziita shule zote za serikali na zile za kata kuwa ni za kishenzi na kuibeza serikali kwenye mipango yake ya kumsogezea karibu shule kwa kuzijenga kila kata na kuondoa ada. Wazazi hawa wakazipuuza shule na jitihada hizi za serikali na kupeleka watoto wao shule za ghrama kubwa. Nia yao ni uvu sana hawa watu kwani walikuwa wanawakatisha tamaa watoto wa masikini wanaosoma hizi shule za serikali zisizokuwa na mabweni, usafiri, mabweni, chakula shuleni wala madawati. Kinachowashangaza walalahoi ni kuona hawa watoto waliozinyanyapaa shule za serikali wanakwenda kuvikimbilia vyuo vya bei nafuu vya serikali na kuwasukumia watoto maskini kule vyuo binafsi kwenye ada kubwa kwa kisingizio cha ufaulu, nonsense!!!

Kila msiba una mwenyewe, msiba wa watoto waliosoma shule za kata (st. Kayumba) mwenyewe ni vyuo vikuu vya serikali. Watoto hawa wavijaze vyuo hivi vya serikali kwanza kabla ya watoto wengine kupata nafasi huko. Serikali (TCU) wametoa ufafanuzi ni mtoto yupi amefaulu na yupi amefeli, mtoto yupi anaweza kusoma kozi gani na yupi hawezi. Vyuo vya serikali havina hiari kwenye jambo hili la kisera. Vyuo binafsi ndio viwe na hiari ya kuchagua cut-off points zao.
 
Huna unachokifahamu wewe, Mwl. Nyerere alitusomesha bure sisi wote kwa dhana kwamba wako maskini ambao wasingeweza kumudu kusoma na kusomesha. Serikali yetu ya sasa imefuta ada kuanzia chekechea hadil A level kwa sababu hizohizo kubwa hata yule mwenye ajira ujira anaoupata ni mdogo sana, ajira hakuna, masoko ya mazao hakuna, watu wetu bado wanalima kwa kijembe cha mkono na kutegemea mvua, wafugaji wanachunga hawafugi, machinga na wafanyabiashara hawalipi kodi ndio maana wanadhani kuwa wanapata faida, watu wetu wananunua magari makuukuu, wanavaa nguo za mitumba, hawakopesheki na wale wanaokopesheka riba ni kubwa sana.

kama unadhani wewe unazofedha tafadhali mpeleke mwanao vyuo binafsi ndani na nje ya nchi badala ya kubadilisha gia angani na kurudi vyuo vya serikali kuzibia wale wasio na kitu kabisa.
 
What you say may be true, but you do not need to conduct any study in order to know why government schools are weaker in academic performances. Priorities, bad policies, low economic, poor planning, unfair world trade transactions, and climate change are among of the basic cause of this. It is a managerial rather than a research issue.

Ninachosema mimi kwenye uzi huu ni kwambaaa, wakati huu ambao wewe na wenzio mnatafuta kwanini watoto kwenye shule za kata hawapati division I ya point 3 na 4 kama wenzao wa shule za private, hivi vyuo vya serikali viendelee kudahiri watoto wengi kutoka shule za serikali, na vyuo vikuu binafsi na mashirika ya dini viendelee kupokea kwa wingi watoto kutoka shule binafsi. Hii itawapunguzia kadhia ya kukusanya ada zao vyuoni, maana mtoto aliyesoma shule ya kata kwenda kusoma chuo binafsi kama KMC, St. Joseph, Kampala International University, Kairuki, Aga Khan au St. John's ni shida tupu.
 
Ebu jaribu kosoma tena kisha kama unathamini utu wako rudi ndani ya moyo wako na kujiuliza haya uliyoyaandika yanamaana ya kuleta suluhu au kujitetea ili hoja yako ishinde kishabiki?

Kama ni mmoja miongoni mwa watu wenye influence kwenye maamuzi basi inabidi nikubali tu Mungu ndiye awezaye kusaidia watanzania, acha nirudi kwake kwa maombi kuliko kuendeleza mjadala huu na mtu mwenye mtizamo kama wako...Kimtazamo mimi nikiwa kusini wewe utakuwa kaskazini....Sioni tunapokutana kihoja.
 
Huna hoja. Ufaulu hautegemei kama upo private au serikalini. Hilo ndilo Prof. Ndalichako alikosea. Acha wapimwe kwa ufaulu
 
Daaaaah! umeongea kwa hisia kali sana, lakini ukweli lazima tuuseme hata kama unauma. Serikali imefanya jambo zuri kuruhusu kuweko kwa shule na vyuo binafsi nchini, kabla ya mwaka 1998 hakukuwa na vyuo vikuu binafsi nchini, watu wote tulisoma kwenye vyuo vichache vya serikali kwa kusaidiwa na kigezo kimoja tu cha ufaulu wetu, hivyo watoto wengi walikosa nafasi ya kusoma. Leo hii shule za serikali na binafsi zimeongezeka inversely proportional na kuongezeka kwa vyuo vikuu nchini. Hali kama hii inahitaji sera na utaratibu maalumu ili kulifanya taifa lisiinamie upande mmoja, kwakuwa sasa hivi kigezo cha kusoma chuo kikuu sio ufaulu wa mtoto kama zamani, bali nguvu za kiuchumi za familia. shule za serikali zina changamoto nyingi mno, hivyo ili mtoto apate ufaulu mkubwa wa kumuwezesha chuo cha bei nafuu cha serikali lazima akasome shule za private. Fikiria itakuwaje kama shule nzuri za watu binafsi zitaongezeka sana kiasi kwamba wanafunzi wao wote wanapata division I points 3, 4 na 5 hii itamaanisha kuwa watoto wa masikini watakaosoma shule za serikali (zenye changamoto nyingi) hawatapata nafasi ya kusoma vyuo. Maana watoto kutoka shule za private watakuwa na uwezo wa kuvijaza vyuo vya serikali kwa kutumia ufaulu wao mkubwa na kuvijaza vile vya private kwakutumia nguvu zao za kiuchumi za wazazi wao (double deaths na double wins). Watoto wa maskini watapigwa nje ndani, bara na pwani, huku na kule na hivi na vile (onlookers)

vyuo binafsi vinatoa elimu ya chuo kikuu kwa gharama kubwa sana ukilinganisha na vyuo vya serikali. Unachosema wewe unataka iwe "survival of the fittest", yaani
 
Huna hoja. Ufaulu hautegemei kama upo private au serikalini. Hilo ndilo Prof. Ndalichako alikosea. Acha wapimwe kwa ufaulu
Uwanja wa kuwapima lazima uwe sawa kwa watoto wote. Shule za serikali hazina maabara halafu scholarships ni kwa watoto waliofaulu masomo ya sayansi. Hapa ni kumaanisha kuwa automatically scholarships hizi ni kwa watoto waliosoma private kwenye maabara safi za sayansi na walimu Bora.
 
Wasomi wetu wanathamini mtu mwenye uwezo wa kukumbuka na siyo kufikiri
Ndiyo maana wao pia hawana huo uwezo wa kufikiri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…