KERO Waziri wa Elimu, tunaomba msaada wako. Shule binafsi bweni hawataki tuone watoto

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
hakuna utaratibu kuwaona kabisa sijui kama unaelewa
Nakuambia huo utaratibu ni mbovu mbaya. Wewe unanihakikishia kuwa hakuna utaratibu wa kuwaona kabisa. Mimi nimekwambia ingetokea wamefanya huo ujinga haraka ninge mwondoa mtoto. Ni haki yangu kumwona mtoto. Ikiwa hata wafungwa huwa wanaonwa itakuwa watoto walio shule. Nyie muanze kutumia akili hata za kuazima.
 
Kama hoja iko sawa na ameshindwa. Kuipangilia msaidie kupangilia, kilaza kwa sababu hakupanga hoja vizur au una kingine? Ebu ipange tuone mpangilio wake kama ni kweli kakosea kupanga.
 
hilo swala limeanza lini? mana hii ni januari hata mwisho wa mwezi hatujafika
Kwani shule si zipo miaka yote tunapambana na uongozi wabadili hayo ? Jan si kitu suala lipo board za shule nyingi sanaaa....wabadilishe utaratibu mbovu
 
Hizo shule za bweni hazina majina?, Zitaje hapa Ili serikali ijue wapi itaanzia.
 
Hizo shule za bweni hazina majina?, Zitaje hapa Ili serikali ijue wapi itaanzia.
Tunataka tamko la serikali kupitia waziri...
Shule karibia zote sasa zinaigana huu ujinga.....
 
Kwani shule si zipo miaka yote tunapambana na uongozi wabadili hayo ? Jan si kitu suala lipo board za shule nyingi sanaaa....wabadilishe utaratibu mbovu
kama mmeongea nahakuna mabadiliko unafikiri utafanya nn? shule zaboarding hasa sec. zina utaratibu flani wa kijinga wao ada mbele mengine wao huamua vile wataamka sku hio, sasa hapo mzazi tafuta mwalim wa karibu jisogeze akuweke karibu na mtoto kuna shule moja matron akitumiwa hela za watoto za pocket money anakula yeye na familia yake mtoto anakaa hata wiki hajui nn kinaendelea anaishi kwa shida madudu n mengi mno au mhamishe ukiona unayiyatakabww hayawi.
 
Zipo shule nyingi za private zenye utaratibu tofauti, zipo ambazo unaweza kwenda kumuona hata kila siku, zingine kila wiki, zingine kila mwezi nk. kuliko kulalamika ni bora kuangalia shule inayokufaa.
Kutaka kila kitu waziri akitolee ufafanuzi ni kupoteza muda.
 
Jioning instructions ilisemaje .. na hadi unampeleka mtoto maana yake masharti yao ulirudhia
 
Jioning instructions ilisemaje .. na hadi unampeleka mtoto maana yake masharti yao ulirudhia
Shule karibia zote wanaigana kwa sasa....hakuna options hapo tunaomba warudishe visiting day.....ina maana sana kwa afya akili ya watoto
 
Hili hata sio swala la kuomba msaada kwa waziri, ni swala la mzazi kumuondoa mwanao kutoka hiyo shule haraka iwezekanavyo.
 
Unajua ni kwanini hizo shule zimezuia utaratibu wa mara kwa mara kwa mzazi kufika kumuona mtoto wake?
Miongoni mwa sababu ni hizi.
1. Usumbufu wa wazazi kwa shule.
2. Mabadiliko ya kifikra na kitabia kwa mtoto baada ya mzazi kumuona mtoto wake.
3. Kuzaliwa kwa malalamiko mengi kutoka kwa wazazi baada ya mzazi kumuona mtoto wake.
 
Wakiweka masaa 3 kumuona mara moja mwezi inatosha sana hasa afya akili watoto hasa wa kike....
 
Shule darasa watoto 8
 
Shule si zimefunguliwa juzi, tayari mnataka kuona watoto hata wiki haijaisha???Au wewe sio wa nchi hii..
Pili kwa nini watoto hasa primary mnapeleka boarding- mtoto chini ya 10 yrs analelewa makambini kama mkimbizi - anakuwa programmed na watu wengine - Trust me hao watoto mnawajengea usugu wa kutokua na hisia na wazazi sio mchezo ..mtapata majibu mbeleni huko, ndo hapo akikua mtoto anasepa miaka 5 - hapigi simu, wala sms, harudi nyumbani, mkiongoea ni kama anaongea na mtu baki tu...
Kumbe kawa trained hivyo
 
Reactions: Cyb
Maana ya kumpeleka bweni ni nini? Kama unataka kumwona mara kwa mara bora akae day tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…