KERO Waziri wa Elimu, tunaomba msaada wako. Shule binafsi bweni hawataki tuone watoto

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Itengwe jumamosi na jumapili ya mwisho wa mwezi kama visiting day (hii iwe lazima kwa shule zote za bweni).
Waziri/serikali ione hili jambo kwenye yale mafaili ambayo hawalali wanayasoma/bukua.
cc;Profesa Adolph Mkenda kwa ukamilishaji zoezi.
 
Itaneni wazazi wote kaeni na uongozi wa shule mpeane maelekezo namna bora ya malezi ya watoto wenu. Hii nchi watu kama kondoo tu. Nyerere alituharibu sijui.
Hawana uthubutu huo, nani ataanzisha? watapingana wao kwa wao
 
Reactions: Tsh
Waziri aingilie kati vipi wakati umeshasema ni shule binafsi? Kila shule ina utaratibu wake,
Hata JF ni platform ambayo ina private ownership, lakini kuna mamlaka ya serikali inayoiangalia mwenendo wake, kama vile TCRA
 
Mnauhakika hawajawahisi mna kipindupindu?
 
Mkuu hizo shule hazina vikao vya wazazi?? Hizo shule hazina fomu za terms of condition?? Kama fomu haisemi kuhusu kumuona mtoto basi hiyo shule haifai kumpeleka mtoto.

Hakuna mzazi chizi ambae anaweza kukaa miezi 3 au 4 asimwone mtoto wake?? Labda kwa mzazi ambae yupo mbali ila mzazi ambae yupo karibu sioni sababu ya kumzuia kumuona mtoto wake maana hiyo ndo furaha yake kuu.
 
We lijinga sana..kwani hao watoto ni wafungwa?
 
Mbona shule Binafsi zingine wanaruhusu, kipi wanaficha hao 😊
 
Jenga shule ya kwako, chawa sio watu wazuri ,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…