Waziri wa Kilimo Hussein Bashe zuieni uuzwaji wa chakula nje ya nchi, mfumuko wa bei unatisha!

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe zuieni uuzwaji wa chakula nje ya nchi, mfumuko wa bei unatisha!

Uk
Huu mjadala tulishaumaliza muda mrefu,ukiona zao lolote liko juu nenda na ww ukalime uje upige faida.


Uko sahihi Sana mkuu!
Watanzania wanataka mahindi yashuke bei ili wale washibe,wazaliane!
Yakipanda mahindi kelele nyingiii mbona mchele bei juu Sana na hakuna mikelele?!
 
Akiuza kwa bei ghali halafu akanunua mahitajit kwa bei kubwa atapata faida Gani!!?

UNAFIKIRI uchumi wetu utakuaje kwa style Hiyo!!?

Maoni yako ni economic oriented au ni politically perspective!?
Na akiuza kwa bei ndogo na akanunua mahitaji kwa bei kubwa atapata faida gani?
 
Acha wakulima nao wapate faida Mana mmewanyinya mda mrefu nyie watu wa mjini. Wakulima ndo wengi kuliko nyie watu wa mjini. Na Samia atapita kwa kishindo 2030 kura kutoka kwa Hawa wakulima. Pia ni strategy ya kuwavutia vijana wakalime siyo zamani unalima halafu hujui ukauze wapi.
Kuna tofauti ya faida na mfumko wa bei bandugu
 
Hapo ndipo unapoambiwa unahitaji kutumia Akili zaidi ya Ushabiki ok mkulima anauza mazao kwa soko la nje then njaa inaingia then huyo huyo na jamii yake wananunua bidhaa zitokanazo na mazao waliyouza kwa bei ya juu
Kuzuia kuuza mazao nje siyo kumsaidia mkulima? Mnafanya wakulima hawana akili hata kidogo!
 
Mkuu

Faida itapatikana kwa kukuza sarafu yetu kwenye soko la Dunia na kudhibiti mfumuko wa Bei!SIO kwa kupaisha mfumuko wa bei kama HIVI!!
Kwahiyo unataka kutuambia, kufunga mipaka kwa kipindi hiki ndio kutaleta mabadiliko na kuipandisha sarafu yetu?

Vipi kuhusu gharama za uwekezaji alizozifanya mkulima tena kwa bei juu ya Mbolea/ Pembejeo?

Kwann usiwe mpango mrefu wa serikali yetu kuanza kuwekeza kwenye kilimo kwa kutoa ruzuku ya Pembejeo, Kuanza kuwekeza kweny kilimo cha kisasa(kisicho cha kutegemea mvua) na kutafuta masoko mazuri ya kuuza nje ya mipaka?

Kwann tusizalishe zaidi kwa gharama nafuu ili ndani nchini tuwe na mazao yakutosha ambayo yataweza kupunguza mfumuko wa bei ya mazao nchini?

Unatambua ni kwann kumekuwa na mfumuko wa bei dhidi ya mazao nchini?...kwa kukukumbusha tu kama hujawaza, sababu kubwa ni kukosekana kwa mazao yakutosha mashambani ambayo imetokana na mabadiliko ya hali ya hewa (upungufu wa mvua).

-Demand imekuwa kubwa kuliko uzalishaji.

Niko tayari kupokea mawazo tofauti ndugu Mwl Athumani Ramadhani
 
Huna akili. Kila mtu aweke akiba ya chakula. Siyo kuzuia chakula kuuzwa. Acheni uzwazwa. Nyambafu!
 
Mkuu

Bei ya debe la mahindi kwenye baadhi ya vijiji nchini ni 25000/= hadi sasa, watu wameshaanza kula kwa kununua unga kwa kilo sh.1700 hadi sasa na hii ni Oktoba hatujui January hali itakuwaje!

Fungeni mipaka hali sio nzuri kabisa, watu wasije kufa njaa, mfuko wa sembe ushafika sh.37000/= tena vijijini kabisa hali sio nzuri!

Naamini utasoma na hatua zitachukuliwa!
Hahahaha sirikali ya bibi imesema tunachakula cha kutosha kufuatia kauli alioitoa Somali boy acha tupike hela baada ya chakula kuisha
 
Wakati Bei ya Mbolea inapaa na gharama za kulima zinaongezeka hamkusema. Tuacheni wakulimq na sisi tufaidi. Kutesa kwa zamu.
 
We we unayejiita mwalima una mawazo ya kijinga sana ,unajua gharama za kuendesha shamba ww,
unajua wakulima ni asilimia 60 na wamekuwa maskini kwa sababu ya sera za kijinga za kuwapangia soko lenye Bei ya chini ya gharama ya uendeshaji, kilimo ni kiwanda na biashara kama zingine,
Wewe na watu wenye mawazo kama ya kwako ni wajinga wenye sera za kipumbavu zilizolemaza sekta ya kilimo na kuzalisha maskini wengi,
Pls stop this nonsense
 
Akiuza kwa bei ghali halafu akanunua mahitajit kwa bei kubwa atapata faida Gani!!?

UNAFIKIRI uchumi wetu utakuaje kwa style Hiyo!!?

Maoni yako ni economic oriented au ni politically perspective!?
Kwanini usishauri na bidhaa zingine zisiuzwe nje kama bidhaa za azam nk kama ndo njia ya kudhibiti mfumko wa bei?
Kwanini tu tuzuie mazao ya wakulima ambazo hutujui gharama za uzalishaji wake?

Unajua faida ya export kwenye uchumi?
Badala tushauri kuboresha sekta ya kilimo ili kuongeza uzalishaji mwingi supply na ili kuongeza export unashauri sera za kijinga,

Kama ni mwalimu kweli unatutaharibia watoto, badala ya kufundisha namna ya kuongeza supply ,unafundisha kudhibiti demand
Achana na hizo fikra za kizamani na na kipumbavu
 
Naona hapa kuna ndezi zinashangilia vyakula kupanda bei, eti wakulima nao wanufaike. Hawa nguruwe [emoji200] hawajui kuwa mkulima huwa hacheleweshi kuuza mazao, na sasa kashauza kila kitu. Na ikitokea taifa au shehemu wanakumbwa na njaa wanaokufa njaa siku zote ni haohao wakulima. Acheni huo upuuzi
Wewe ni mjinga kama sio mpambavu, na mwenye fikra za kizamani sana,
kwa Sasa watu wanalima kilimo biashara na sio ww usubiri wakulima walime Ili uwapangie soko la bei ya chini bila kujua gharama za uzalishaji wao, acha hizo fikra za kipuuzi
 
Wenzetu serikali zao zinawathamini na kuwajali sana Wakulima

Wanahakiiisha fair trade inafanyika tena wamefika mbali mbali duniani wameona Wakulima wanavyotaabika kuanzia wanakolima Ndizi mpaka Cocoa na kahawa bei wanahakikisha wananunua kwa bei inayoridhisha

Waacheni wauze kwa bei zao na wanaopeleka nje watathimini bei kwa kulinganisha na dollars kabisa

Halafu bora kuwatetea wakulima sana maana wao hawapeleki nje bali ni wanunuzi wakubwa ndio wanafaidika zaidi
Tujitafakari na kuzalisha cash crops zaidi maana wanaofaidika ni majirani zaidi wanaonunua kwa bei ya kutupa na bidhaa zinafika Ulaya wakati ni zetu
 
Kila Mtanzania ale matunda ya jasho lake bila ya kuingiliwa na Vizabzabina.
 
Kalime na wewe Ili waje wazuie..

Mwaka huu ndio mwaka wa kufidia hasara zote za awamu ya 5..

Mwisho Waziri amesema hana mpango wa kufunga masoko na hiyo sio njia pekee kwani hakuna mfanyabiashara anaweza kufanya exports bila kupewa Kibali na Serikali..

Waziri amesema watafungia maghala yao Ili kushusha Bei kwenye Mikoa ambayi Bei iko juu zaidi..

Ila huku kwetu gunia la mahindi ni 80,000,tumehifadhi tunasubiria Bei ipande zaidi.
Umehifafhi mahindi Kwa kiuatilifu gani? Actellic ya maji au Shumba dust?! Au airtight bags (agro z)?
 
Mkuu

Bei ya debe la mahindi kwenye baadhi ya vijiji nchini ni 25000/= hadi sasa, watu wameshaanza kula kwa kununua unga kwa kilo sh.1700 hadi sasa na hii ni Oktoba hatujui January hali itakuwaje!

Fungeni mipaka hali sio nzuri kabisa, watu wasije kufa njaa, mfuko wa sembe ushafika sh.37000/= tena vijijini kabisa hali sio nzuri!

Naamini utasoma na hatua zitachukuliwa!
Tulinunuwa mbolea bei ghari sana wacha ipande.Tena mwaka huu tunapanga foleni siku2 kwenye jua ndiyo tunapata mbolea mwakani tena.
 
Back
Top Bottom