Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Hivi Mbarawa atazungumza mara ngapi kuhusu DP WORLD ?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nani kakwambia Bandari ya Mombasa hakuna mwekezaji?
Ili kuongeza trust ya raia kwa serikali yao na kwakua kuna hisia za kisiasa kwamba hao wameshaji compromise tunaomba waachie ngazi, ili watu wengine waingie na kuanza upya mchakatoKama haachii ngazi angeacha tu kusema chochote
Ewaaaaa hapo sawa kabisa, Mimi ni mpumbavu ninajielewa!Mpumbavu ni wewe
Huu ni ukweli wa wazi, japo kuna sehemu na yeye ana mumunya maneno kwasababu anajua ni wapi penye kigugumizi.Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni
Wanasiass wa CCM na Upinzani vizuri kuachia wataalamu husika jambo husika watoe ufafanuzi kwa wananchi
Kwenye hii Sakata la Press Conference ya kuhusu DP World Kiongozi wa team.ya Tanzania ya kujadiliana na DP World Mkrugenzi mkuu wa mamlaka ya anga mwanasheria Johari kafafanua vizuri mno kipengele kwa kipengele kwa lugha rahisi tofauti na wapiga domo wanasiasa wa CCM na Upinzani
Hongera kwako Mwanasheria Johari nimekuelewa vizuri na maslahi ya nchi yako.salama huko.kwenye mikataba kuandaa uweko kwenye team wasihe kuchemka huko sababu wewe ndie unajua kwa undani kuliko wanasiasa viongozi wa serikali, bunge na Vyama vya siasa ikiwemo CCM na Upinzani Wakiongoe.hili swala wanaishia tu kuchochea moto sababu ya hoja dhaifu mno na hopeless kabisa na kufoka foka tu na kutishia watu
Uko vizuri kichwani na unajua nchi iendeje kiuchumi pamoja na kuwa wewe mwanasheria na unajua kueleza kitu hadi layman aelewe vipengele vinaongelea nini
Hongera sana Johari.Tanzania inahitaji wenye akili kama zako. Kwenye uendeshaji nchi
TICS mmefanikiwa kuuvunja kwa sababu za aina ya mkataba mlioingia nao.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa anazungumza na Waandishi wa Habari, Jijini Dar es Salaam muda huu kuhusu uwekezaji wa Bandari.
Mbarawa:
Pamoja na Serikali kuendeleza juhudi za maboresho ya Bandari zetu, bado ufanisi katika utoaji huduma wa Bandari haujafikia viwango vinavyotakiwa kimataifa.
Hali ya ufanisi wa Bandari ya Dar es Salaam na nyingine nyingi zinazoendeshwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania upo chini sana, udhaifu huo unaonekana katika utendaji wa kila siku wa Bandari zetu pamoja na ukusanyaji wa mapato
Bandari ya Dar imeendelea kuwa nyuma dhidi ya Bandari shindani katika Kanda, mfano wastani wa meli kusubiri nangani ni siku 5 sawa na Saa 120 ikilinganishwa na siku 1 na saa 6 kwa bandari ya Mombasa.
Meli kutumia muda mrefu kupakia shehena kantini kwa wastani wa siku tano wakati kimataifa ni siku moja inayokubalika kimataifa.
Ufanisi mdogo wa Bandari ya Dar es Salaam umetokana na changamoto mbalimbali ikiwemo kukosekana mifumo ya kisasia ya TEHAMA, kutokuwepo kwa maeneo ya kutosha ndani na nje ya Bandari ya kuhifadhia shehena za mizigo pamoja na maegesho ya kutosha ya kuegeshea meli.
Changamoto nyingine ni kukosekana kwa mitambo ya kutosha na ya kisasa inayobadilika mara kwa mara kutokana na teknolojia na hivyo kuwa na gharama kubwa.
Athari za kutokuwa na ufanisi katika Bandari ya Dar es Salaam ni meli kusubiri muda mrefu nangani, mfano gharama ya meli kusubiri nangani kwa siku moja ni takribani Dola 25,000 (Tsh. Milioni 58).
Meli kutumia wastani wa siku tano kupakia na kupakua shehena ukilinganisha na siku 1 inayokubalika kimataifa.
Meli kubwa kutokuja katika Bandari ya Dar es Salaam kutokana na kuchukua muda mrefu kuhudumiwa, hivyo kusababisha bandari yetu kuwa inayolishwa na Bandari nyingine.
Uwezo mdogo wa Bandari ya Dar unaikosesha Nchi mapato makubwa ambayo yangeweza kusaidia katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati inayoendelea kutekelezwa Nchini.
Ili kutoendelea na hali hiyo, Serikali iliingia makubaliano 2000 Serikali ya Awamu ya Tatu iliingia mkataba wa upangaji na uendeshaji na Kampuni ya TICTS, mkataba ambao ulidumu kwa miaka 22 na kuipa haki za kipekee TICTS kuendesha shughuli za gati namba 8 hadi 11 za Bandari ya Dar es Salaam huku maeneo mengine yakihudumiwa na TPA.
Desemba 2022, Serikali ya Awamu ya 6 baada ya kuona mkataba hauendani na maslahi mapana ya Nchi yetu iliamua kusitisha mkataba huo.
Serikali kupitia Mamlaka ya Bandari Tanzania ilipokea mapendekezo ya wawekezaji mbalimbali Duniani, lengo kuu likiwa ni kufungua masoko ya kimkakati katika kufungua eneo la bidhaa na usafirishaji ndani ya Nchi na maeneo yanayotuzunguka.
Baada ya uchambuzi wa kina Serikali ilianzisha majadiliano na Kampuni ya DP World kwa sababu zifuatazo:
Uwezo mkubwa wa uendeshaji wa shughuli za Bandari Afrika, Asia, Ulaya, Marekani ya Kaskazini na Kusini na Australia.
DP World ina uwezo na kuchagiza mnyororo mzima wa usafirishaji kutoka maeneo ambapo bidhaa zinatoka hadi kwa walaji wa bidhaa.
DP World inamiliki zaidi ya meli 400 za mizigo, ina uzoefu wa uendeshaji wa Bandari 6 Afrika na zaidi ya Bandari 30 Duniani kote.
Wawekezaji wengine waliowasilisha mapendekezo yao hayakukidhi sifa kwa mwekezaji ambaye alihitajika.
Kabisa uko sahihiHuu ni ukweli wa wazi, japo kuna sehemu na yeye ana mumunya maneno kwasababu anajua ni wapi penye kigugumizi.
Niseme tu kusema ukweli ni mwelewa na kama hana hidden agenda siyo mbabaishaji kama wale wengine wa mwanzo

Waziri wa uchukuzi Yuko live anaongea na waandishi kuhusu kile kinachoitwa uwekezaji wa DPW, Kwa mtazamo wangu, press hii itazua maswali zaidi.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa anafanya mkutano na Wahariri muda huu jijini Dar es Salaam kuhusu mkataba wa bandari kati ya DP World na Serikali ya Tanzania
Mzee freeman Mbowe nae atakua na press conference Leo kuhusu maazimio ya Kamati kuu......
Wacha tuoneView attachment 2687525
Unataka waanze kulia hadharani Kwa kukosa majibu stahikiTunataka mdaharo wa Waziri Mbarawa na Wanasheria Binafsi waliobobea katika Nyanja ya Mikataba ya Kimataifa.
Hao waandishi wa habari akina Zembwela, na Kitenge hawana uhalari wa kuongelea mambo ya Mikataba ya Kimataifa.
Watanzania tuiamin Serikali
Mkataba una manufaa
Bandari haijauzwa
Na blaaa blaaa mingi.
Sisi tunataka hayo manufaa, tuyaone kupitia Mkataba Kwa mujibu wa Katiba yetu !!.
Wanajua tumepigwaNilitamani kupata maoni ya watu hawa 2. Bashiru na Polepole kuhusu hii kitu
**** mtu aliulizia bei ya Toilet Paper, bado anahitaji?Shida inaanzia kwenye umasikini. Mtu akipata ubunge anaona anakaribia kuuaga umasikini, hivyo hukubali chochote kutoka kwa viongozi Wa juu ilimradi tu awe na uhakika nafasi yake italindwa. Na ndio maana kule Bungeni siyo rahisi kumtofautisha mtu aliye soma na ambaye hajasoma. Wote wanafanana. Huanza kusifia weee ndio aje kwenye hoja.Toilet