Kilimbatzz
JF-Expert Member
- Feb 11, 2023
- 9,134
- 14,593
Adv Mbula anajenga hoja nzuri ya kumtetea Rais
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hamza ni mzanzibar anadhana na wabara ni kama wazanzibar ni wavivu kusomaNdugu Hamza acha upotoshaji, kwenye IGA ardhi imetajwa itagawiwa kwa mwekezaji, je ardhi si mali asili unaposema hakuna mali asili atakayo pewa? Bandari ina simama hewani? Maji ya bahati si mali asili? Msitumie upotoshaji.
Kama hamtaruhusu ardhi kumilikiwa basi ondoeni article 8 yote kwenye IGA
Anaujua? yeye kasaini tu hajui hata kilichomoAsema kabisa mkataba ni wa muda gani?
Waandishi ndiyo akina Kitenge wanasubiri bahasha maisha yaendeTatizo la wanahabari wetu ni mambumbumbu kwelikweli!
Hawana weledi wowowte ktk tasnia ya habari wala courage ya kuhoji!
Mbarawa ni mwanasheria? alikuwa anafafanua mkataba? vile vipengele OVU amesemea?
Waandishi ndiyo akina Kitenge wanasubiri bahasha maisha yaendeTatizo la wanahabari wetu ni mambumbumbu kwelikweli!
Hawana weledi wowowte ktk tasnia ya habari wala courage ya kuhoji!
Mbarawa ni mwanasheria? alikuwa anafafanua mkataba? vile vipengele OVU amesemea?
Tatizo haliko kwenye mwekezaji, tatizo liko kwenye utata wa mkataba. Kwa muda gani? Bandari zote Tanganyika,au baadhi ya bandari? Kwa Nini iwe bandari za Tanganyika tu na kuziengua za Zanzibar? Waziri afafanue utata wa mkataba, wawekezaji tunawataka.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa anazungumza na Waandishi wa Habari, Jijini Dar es Salaam muda huu kuhusu uwekezaji wa Bandari.
Mbarawa:
Pamoja na Serikali kuendeleza juhudi za maboresho ya Bandari zetu, bado ufanisi katika utoaji huduma wa Bandari haujafikia viwango vinavyotakiwa kimataifa.
Hali ya ufanisi wa Bandari ya Dar es Salaam na nyingine nyingi zinazoendeshwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania upo chini sana, udhaifu huo unaonekana katika utendaji wa kila siku wa Bandari zetu pamoja na ukusanyaji wa mapato
Bandari ya Dar imeendelea kuwa nyuma dhidi ya Bandari shindani katika Kanda, mfano wastani wa meli kusubiri nangani ni siku 5 sawa na Saa 120 ikilinganishwa na siku 1 na saa 6 kwa bandari ya Mombasa.
Meli kutumia muda mrefu kupakia shehena kantini kwa wastani wa siku tano wakati kimataifa ni siku moja inayokubalika kimataifa.
Ufanisi mdogo wa Bandari ya Dar es Salaam umetokana na changamoto mbalimbali ikiwemo kukosekana mifumo ya kisasia ya TEHAMA, kutokuwepo kwa maeneo ya kutosha ndani na nje ya Bandari ya kuhifadhia shehena za mizigo pamoja na maegesho ya kutosha ya kuegeshea meli.
Changamoto nyingine ni kukosekana kwa mitambo ya kutosha na ya kisasa inayobadilika mara kwa mara kutokana na teknolojia na hivyo kuwa na gharama kubwa.
Athari za kutokuwa na ufanisi katika Bandari ya Dar es Salaam ni meli kusubiri muda mrefu nangani, mfano gharama ya meli kusubiri nangani kwa siku moja ni takribani Dola 25,000 (Tsh. Milioni 58).
Meli kutumia wastani wa siku tano kupakia na kupakua shehena ukilinganisha na siku 1 inayokubalika kimataifa.
Meli kubwa kutokuja katika Bandari ya Dar es Salaam kutokana na kuchukua muda mrefu kuhudumiwa, hivyo kusababisha bandari yetu kuwa inayolishwa na Bandari nyingine.
Uwezo mdogo wa Bandari ya Dar unaikosesha Nchi mapato makubwa ambayo yangeweza kusaidia katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati inayoendelea kutekelezwa Nchini.
Ili kutoendelea na hali hiyo, Serikali iliingia makubaliano 2000 Serikali ya Awamu ya Tatu iliingia mkataba wa upangaji na uendeshaji na Kampuni ya TICTS, mkataba ambao ulidumu kwa miaka 22 na kuipa haki za kipekee TICTS kuendesha shughuli za gati namba 8 hadi 11 za Bandari ya Dar es Salaam huku maeneo mengine yakihudumiwa na TPA.
Desemba 2022, Serikali ya Awamu ya 6 baada ya kuona mkataba hauendani na maslahi mapana ya Nchi yetu iliamua kusitisha mkataba huo.
Serikali kupitia Mamlaka ya Bandari Tanzania ilipokea mapendekezo ya wawekezaji mbalimbali Duniani, lengo kuu likiwa ni kufungua masoko ya kimkakati katika kufungua eneo la bidhaa na usafirishaji ndani ya Nchi na maeneo yanayotuzunguka.
Baada ya uchambuzi wa kina Serikali ilianzisha majadiliano na Kampuni ya DP World kwa sababu zifuatazo:
Uwezo mkubwa wa uendeshaji wa shughuli za Bandari Afrika, Asia, Ulaya, Marekani ya Kaskazini na Kusini na Australia.
DP World ina uwezo na kuchagiza mnyororo mzima wa usafirishaji kutoka maeneo ambapo bidhaa zinatoka hadi kwa walaji wa bidhaa.
DP World inamiliki zaidi ya meli 400 za mizigo, ina uzoefu wa uendeshaji wa Bandari 6 Afrika na zaidi ya Bandari 30 Duniani kote.
Wawekezaji wengine waliowasilisha mapendekezo yao hayakukidhi sifa kwa mwekezaji ambaye alihitajika.
Kina Kitenge na Baba Levo? 😂 😂 😂 😂 😂 😂Tatizo la wanahabari wetu ni mambumbumbu kwelikweli!
Hawana weledi wowowte ktk tasnia ya habari wala courage ya kuhoji!
Mbarawa ni mwanasheria? alikuwa anafafanua mkataba? vile vipengele OVU amesemea?
Mtetezi wa Serikali na Mkataba/makubaliano ya uendeshaji wa Bandarihivi huyo hamza anaongea kama nani kwenye suala la bandari
Hiyo kuondoa haiwezekani. Bunge limesharidhiaNaunga mkono bandari kupewa mwekezaji Ila vile vipengele ambavyo wananchi wanapigia kelele viondolewe
Kitenge ni form 4 total failureWaandishi ndiyo akina Kitenge wanasubiri bahasha maisha yaende
Ushirikina unambeba snKitenge ni form 4 total failure
Ibara 63 (3) (e) ya Katiba ya Tanzania mikataba ya kimataifa ya inatamka hatua gani ifuatwe. Na inatakiwa Mchakato wa ndani ufikishwe baraza la mawaziri halafu inakwenda bungeni na bunge linatakiwa kuomba maoni kutoka kwa wananchi kabla ya kutoa Azimio la Kuunga mkono
Watanzania wamechafukwaWatu wamegoma kuwaachia,,Watz wamekuwa ruba,,,Wamekuwa wakali na vya kwao na si dhambi wanastahili sana kuvipagania kwa nguvu na kwa juhudi zote,,,,Viongozi wetu ni vizuri wangekuwa wanasoma alama za nyakati,,Kuishi kwa kujali na kuthamini nyakati ni jambo moja Bora Sana na la msingi mnoo katika kuishi na kuyajenga maisha Yaliyo Bora!!