Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Mbarawa azungumza kuhusu uwekezaji wa Bandari

swali la kujiuliza kama hakuna mali asili inayohusika kwanini bunge limepelekewa muswada wa kurekebisha sheria na umiliki wa mali asili yetu ili isiwahusu hao wawekezaji?

Kwanini hawakutoa tenda ili kuruhusu wawekezaji wengine na huyo akapewa upendeleo?

Tutawaaminije leo wakati for almost 40 years uwekezaji ume betray watanzania na kusababisha madhara makubwa kwa uchumi wa nchi yetu?
 
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni
Wanasiasa wa CCM na Upinzani vizuri kuachia wataalamu husika jambo husika watoe ufafanuzi kwa wananchi

Kwenye hii Sakata la Press Conference ya kuhusu DP World Kiongozi wa team.ya Tanzania ya kujadiliana na DP World Mkrugenzi mkuu wa mamlaka ya anga mwanasheria Hamza Johari kafafanua vizuri mno kipengele kwa kipengele kwa lugha rahisi tofauti na wapiga domo wanasiasa wa CCM na Upinzani

Hongera kwako Mwanasheria Hamza Johari nimekuelewa vizuri na maslahi ya nchi yako.salama huko.kwenye mikataba kuandaa uweko kwenye team wasihe kuchemka huko sababu wewe ndie unajua kwa undani kuliko wanasiasa viongozi wa serikali, bunge na Vyama vya siasa ikiwemo CCM na Upinzani Wakiongoe.hili swala wanaishia tu kuchochea moto sababu ya hoja dhaifu mno na hopeless kabisa na kufoka foka tu na kutishia watu

Uko vizuri kichwani na unajua nchi iendeje kiuchumi pamoja na kuwa wewe mwanasheria na unajua kueleza kitu hadi layman aelewe vipengele vinaongelea nini

Hongera sana Hamza Johari.Tanzania inahitaji wenye akili kama zako. Kwenye uendeshaji nchi
 
Huu ni ukweli wa wazi, japo kuna sehemu na yeye ana mumunya maneno kwasababu anajua ni wapi penye kigugumizi.

Niseme tu kusema ukweli ni mwelewa na kama hana hidden agenda siyo mbabaishaji kama wale wengine wa mwanzo
 
TICS mmefanikiwa kuuvunja kwa sababu za aina ya mkataba mlioingia nao.
Shida ya watanzania haipo kwenye uwekezaji bali aina ya mkataba unaowekezwa na DP world.
Kwanza huu hauna ukomo hadi kazi itakapomalizika yaani ni wa milele.
Pili haujaainisha faida tutakazopata tofauti na ile tunayopata kwa sasa.
Tatu hakuna meli iliyowahi kukosa kuleta mzigo unaohitajika nchini kwa sababu za kuchelewa kupakua.
Nne bandari zote haziwezi kukabidhiwa kwa mwekezaji mmoja kwa mujibu wa katiba na ufafanuzi wa sheria zake nk.
Kama huu mkataba hautaandikwa upya na kurudishwa bungeni ili tupate fursa za kuujua hatukubali kamwe kurudishwa kwenye ukoloni wa koloni letu la kale ya waarabu.
 
Ameongea vizuri sana.
 
Sawa,chamsingi leteni updates
 
Watanzania tuiamin Serikali

Mkataba una manufaa

Bandari haijauzwa


Na blaaa blaaa mingi.



Sisi tunataka hayo manufaa, tuyaone kupitia Mkataba Kwa mujibu wa Katiba yetu !!.

Wewe ndio wale wale mbumbumbu tunahitaji majibu ya kisheria na sio kisiasa, ticts mkataba ulisitishwa nchini kwetu hao DP world mkataba na migogoro unawapelekea uingereza, unaenda kubadili sheria ya ulinzi wa rasilimali za taifa ili kunufaisha mafisadi hapana hapana na serikali haitakiwi kuaminiwa
 
**** mtu aliulizia bei ya Toilet Paper, bado anahitaji?
 

Attachments

  • Screenshot_20230714.jpg
    122.2 KB · Views: 1
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…