Akilinjema
JF-Expert Member
- Aug 9, 2016
- 11,430
- 11,813
Kwanini Bandari za zanzibar ziwemo wakati tayari washapewa Makaburu
Kwa miaka 5 tu,
Ila huku Tanganyika mkataba unasema miaka mingapi?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwanini Bandari za zanzibar ziwemo wakati tayari washapewa Makaburu
Kkenge ww,tuwasikilize wanasheria vilaza
Leo kwa maelezo yao wenyewe wanasema ni mkatabaJamani ni mejitahidi kusogea karibu na tv lakini sijaelewa huko uliopelekwa bugeni ulikuwa mkataba au makubaliano?
Sent from my ZTE T1002 using JamiiForums mobile app
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa anazungumza na Waandishi wa Habari, Jijini Dar es Salaam muda huu kuhusu uwekezaji wa Bandari.
Mbarawa:
Pamoja na Serikali kuendeleza juhudi za maboresho ya Bandari zetu, bado ufanisi katika utoaji huduma wa Bandari haujafikia viwango vinavyotakiwa kimataifa.
Hali ya ufanisi wa Bandari ya Dar es Salaam na nyingine nyingi zinazoendeshwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania upo chini sana, udhaifu huo unaonekana katika utendaji wa kila siku wa Bandari zetu pamoja na ukusanyaji wa mapato
Bandari ya Dar imeendelea kuwa nyuma dhidi ya Bandari shindani katika Kanda, mfano wastani wa meli kusubiri nangani ni siku 5 sawa na Saa 120 ikilinganishwa na siku 1 na saa 6 kwa bandari ya Mombasa.
Meli kutumia muda mrefu kupakia shehena kantini kwa wastani wa siku tano wakati kimataifa ni siku moja inayokubalika kimataifa.
Ufanisi mdogo wa Bandari ya Dar es Salaam umetokana na changamoto mbalimbali ikiwemo kukosekana mifumo ya kisasia ya TEHAMA, kutokuwepo kwa maeneo ya kutosha ndani na nje ya Bandari ya kuhifadhia shehena za mizigo pamoja na maegesho ya kutosha ya kuegeshea meli.
Changamoto nyingine ni kukosekana kwa mitambo ya kutosha na ya kisasa inayobadilika mara kwa mara kutokana na teknolojia na hivyo kuwa na gharama kubwa.
Athari za kutokuwa na ufanisi katika Bandari ya Dar es Salaam ni meli kusubiri muda mrefu nangani, mfano gharama ya meli kusubiri nangani kwa siku moja ni takribani Dola 25,000 (Tsh. Milioni 58).
Meli kutumia wastani wa siku tano kupakia na kupakua shehena ukilinganisha na siku 1 inayokubalika kimataifa.
Meli kubwa kutokuja katika Bandari ya Dar es Salaam kutokana na kuchukua muda mrefu kuhudumiwa, hivyo kusababisha bandari yetu kuwa inayolishwa na Bandari nyingine.
Uwezo mdogo wa Bandari ya Dar unaikosesha Nchi mapato makubwa ambayo yangeweza kusaidia katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati inayoendelea kutekelezwa Nchini.
Ili kutoendelea na hali hiyo, Serikali iliingia makubaliano 2000 Serikali ya Awamu ya Tatu iliingia mkataba wa upangaji na uendeshaji na Kampuni ya TICTS, mkataba ambao ulidumu kwa miaka 22 na kuipa haki za kipekee TICTS kuendesha shughuli za gati namba 8 hadi 11 za Bandari ya Dar es Salaam huku maeneo mengine yakihudumiwa na TPA.
Desemba 2022, Serikali ya Awamu ya 6 baada ya kuona mkataba hauendani na maslahi mapana ya Nchi yetu iliamua kusitisha mkataba huo.
Serikali kupitia Mamlaka ya Bandari Tanzania ilipokea mapendekezo ya wawekezaji mbalimbali Duniani, lengo kuu likiwa ni kufungua masoko ya kimkakati katika kufungua eneo la bidhaa na usafirishaji ndani ya Nchi na maeneo yanayotuzunguka.
Baada ya uchambuzi wa kina Serikali ilianzisha majadiliano na Kampuni ya DP World kwa sababu zifuatazo:
Uwezo mkubwa wa uendeshaji wa shughuli za Bandari Afrika, Asia, Ulaya, Marekani ya Kaskazini na Kusini na Australia.
DP World ina uwezo na kuchagiza mnyororo mzima wa usafirishaji kutoka maeneo ambapo bidhaa zinatoka hadi kwa walaji wa bidhaa.
DP World inamiliki zaidi ya meli 400 za mizigo, ina uzoefu wa uendeshaji wa Bandari 6 Afrika na zaidi ya Bandari 30 Duniani kote.
Wawekezaji wengine waliowasilisha mapendekezo yao hayakukidhi sifa kwa mwekezaji ambaye alihitajika.
Mkurugenzi TCCA: Hakuna ardhi ya Tanzania ambayo itauzwa
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini, Hamza Johari amewatoa hofu Watanzania kuhusu tarifa za kuwa nchi imeuzwa kutokana na mkataba wa makubaliano ya ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai akisema kuwa taarifa hizo hazina ukweli wowote.
Kauli hiyo ameitoa leo Julai 14, 2023 alipokuwa akizungumza katika mkutano na wahariri jijini Dar es Salaam huku akiwataka watu kutoingiza siasa kwenye masuala yahusuyo uchumi wa nchi na kusisitiza kuwa mkataba huo ni mzuri.
Mbona hiyo zanzibar tayari ishachomoka Bandari yake tayari kashampa mkaburuTibaijuka anauliza:Bila ya marekebisho ya Mkataba article 4 Zanzibar haichomoki Wala Kemondo haichomoki
Maswali mazuriHoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa
1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)
2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?
3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?
4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!
6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
Unateseka ukiwa wapi?hivi huyo hamza anaongea kama nani kwenye suala la bandari
Nashukuru kwa ufafanuziMbona hiyo zanzibar tayari ishachomoka Bandari yake tayari kashampa mkaburu
Kivipi? Au unajifariji tu?Ama kweli wameshikwa pabaya.
Huo mfumo wa Muungano ni pasua kichwa ni ngumu kuufasiriIla mipaka yake ya kiutendaji ni bara tuu maana zanzibar hawahusiki kwenye hayo mambo
Maswali mazuri
FYI: Waandishi wa Habari wengi sana hapa Tz hawana shule ya kutosha kichwani, yaani walio wengi elimu yao ni ya kuunga unga. Wapo wachache sana ambao kimsingi wapo fit kielimu na pia wako competent kwenye taaluma na kazi ya uandishi wa habari, pia wako serious na kazi zao za hanari. Kitu cha kusikitisha zaidi ni kwamba, hata hao waandihi wa habari ambao mnawafahamu kwamba ni watu maarufu hapa nchini, nao uki hunguza kwa umakini sana utaona pia elimu zao ni za kuungaunga, ukanjanja, na wengine wapo katika taasisi za vyombo vy habari maarufu hapa nchini. Very sad indeed!Kitenge ni form 4 total failure
Wapi duniani Jeshi ndo lina utaalamu wa kuendesha bandari?Hamza anahema sana daa pesa ni balaa tupu Mimi naona Bora jeshi lihamie pale Kwa ajili ya kuopalete shughuli zote bandalini kama shida ni uaminifu jeshi likafanye KAZI hapo
Sent from my ZTE T1002 using JamiiForums mobile app
Binafsi kwenye Hili Hamza kajitahidi sana kueleza kitaalamu kwa asilikia kubwa sijasema asilimia 100Mkuu mtumisji wa Serikali siku zote anatetea ugali wake na WA bosi wake na Wala siyo akili zake
Wenyewe wanasema sio Mkataba ni Makubaliano utapokuja huo mkataba ndio wataweka huo mudaKwa miaka 5 tu,
Ila huku Tanganyika mkataba unasema miaka mingapi?