Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Mbarawa azungumza kuhusu uwekezaji wa Bandari

Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
 

Attachments

  • IMG_1068.MP4
    2.1 MB
  • 3DBA2C45-A50D-4319-8254-A3C1AB24F6F3.jpeg
    32 KB · Views: 1
  • 629E7CA7-9216-4246-AE4C-C6C0AB2EC6CA.jpeg
    140.9 KB · Views: 1
  • 268E9966-3CC4-477F-9F14-7971DA4881BC.jpeg
    37.4 KB · Views: 1
  • 7F1A625B-1DA9-4C8B-A9B0-003C9FF749E0.jpeg
    148.7 KB · Views: 1
  • 9A97A0EE-0405-410D-AB36-1D01351D3153.jpeg
    115.9 KB · Views: 1
  • 2B6F888E-2D50-4163-B694-1D9AD1B00FEE.jpeg
    58 KB · Views: 2
  • 96AC4F70-B2B1-4483-B6EB-59C4C23120B2.jpeg
    55.5 KB · Views: 1
  • 9FD5F3E9-2F97-426B-8B18-EA4727B5A1A7.jpeg
    57 KB · Views: 1
  • 5F9C7745-B184-4CEF-B236-059905C9BB48.jpeg
    57.3 KB · Views: 1
  • 9E2FE5EF-DF92-462B-860C-7F69309901D1.jpeg
    62 KB · Views: 1
  • 66B200BE-D450-44A5-B79C-BCC191D22E79.jpeg
    9.9 KB · Views: 1
  • 15A80DBA-904A-4724-8218-84B6ABCE6004.jpeg
    115 KB · Views: 1
  • FEDD7557-CC0F-4249-BEDB-4090AF55C406.jpeg
    55.3 KB · Views: 3
  • A684B876-BDAB-4823-BE27-2C985FDF8C82.jpeg
    150.5 KB · Views: 2
  • FAE4437F-EE0B-48B8-A44D-D97387AC1004.jpeg
    131.1 KB · Views: 1
  • 002A75F3-6A7E-4FA1-9266-E2CC6D26613C.jpeg
    75.7 KB · Views: 1
  • F4A9A5BF-A2B6-43BD-8834-35658C235242.jpeg
    55.1 KB · Views: 1
  • IMG_1261.MP4
    632.6 KB
Huo uwekezaji na uendeshaji tuna uweza mkishindwa sana kodisheni management toka nchi zingine. Kwa miaka sema 5 . Na kuhusu vifaa mnaweza kununua hata Kwa mkopo au karadha.
Tehema nayo inaweza kununuliwa au kuwakodisha watu wengine.
Mwisho tupate plan ya upanuzi WA bandari yetu toka kampuni tofauti ili tuweze kumiliki wenyewe na kufanya wenyewe siku zijazo.
 
Maswali mazuri
 
 
ITV watakata matangazo ikifika saa Saba Ili kupisha taarifa ya Habari ya Saa Saba
 
Kitenge ni form 4 total failure
FYI: Waandishi wa Habari wengi sana hapa Tz hawana shule ya kutosha kichwani, yaani walio wengi elimu yao ni ya kuunga unga. Wapo wachache sana ambao kimsingi wapo fit kielimu na pia wako competent kwenye taaluma na kazi ya uandishi wa habari, pia wako serious na kazi zao za hanari. Kitu cha kusikitisha zaidi ni kwamba, hata hao waandihi wa habari ambao mnawafahamu kwamba ni watu maarufu hapa nchini, nao uki hunguza kwa umakini sana utaona pia elimu zao ni za kuungaunga, ukanjanja, na wengine wapo katika taasisi za vyombo vy habari maarufu hapa nchini. Very sad indeed!
 
Mkuu mtumisji wa Serikali siku zote anatetea ugali wake na WA bosi wake na Wala siyo akili zake
Binafsi kwenye Hili Hamza kajitahidi sana kueleza kitaalamu kwa asilikia kubwa sijasema asilimia 100

Ila yuko vizuri ukimsikiliza Hamza mtu kama mimi Mkristo nasali kwa Mwamposya sipendi uongo wala unafiki nikipewa taarifa sahihi binafsi naona kabisa Hamza alifanya kazi yake vizuri mno akiwa na dhamiri njema mno kwa maslahi ya nchi kwa asilimia kubwa

Mimi.nimemuelewa hiyo nafasi ya kiofisi aliyonayo kama mkurugenzi wa Anga ni ndogo mno ukilinganisha na uwezo wa akili yake anastahili kuwa na na nafasi kubwa zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…