WAZO: kwanini serikali isipunguze muda wa kustaafu kwa watumishi wa umma

Mtu anafanya kazi miaka ishirini alichowekeza ni kukata viuno wake wanne ,michepuko saba watoto timu ya mpira alafu astaafu🀣🀣
 
Serikali Haina pesa za kulipa wastaafu.
Fikiria hata Hawa wanao staafu sasa wakiwa na miaka 60,wanalipwa pension baada ya miaka miwili.

Je wakisema walio fikia 45-60 wastaafu wataweza kuwalipa kwa mkupuo?
Pia kustaafu mapema sio suluhisho la ajira.
Serikali ina pesa sana haijaamua tu.....hizo milions anazopewa mbunge kila mwezi na hazina kodi? Hizo milioni mia kadhaa wanazojichotea kila baada ya miaka mitano?? Hizo vieite??

Serikali inazo pesa ni vile tu wastaafu na wasio na ajira sio kipaumbele
 
Hii inaweza saidia kupunguza tatizo la ajira nchini ikibidi kutoka miaka 60 mpka 45 au 50 ili vijana nao wapate nafasi kwani hii itatoa nafasi nyingi katika kada mbalimbali .
Nchi zote Duniani zinaongeza mda wa watu kustaafu sio kupunguza.

Lengo la Ajira sio kila mtu apite Bali ufanisi upatikane
 
Nchi zote Duniani zinaongeza mda wa watu kustaafu sio kupunguza.

Lengo la Ajira sio kila mtu apite Bali ufanisi upatikane
Hebu Mchumi waambie Hao wanaong'ang'ania hoja zao za Ajabu..
Mimi Nina miaka 53 Kwa sasa Nimebakiza Miaka 12 Nistaafu Kazini Halafu Mtu ananiambia Nistaafu sasa Hivi..
Anataka Kunikatisha Maisha Yangu au πŸ˜‚πŸ˜‚
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Huyu jamaa anataka Vizee Vimroge Kizee kina Miaka 50 na Kitu Bado kinahisi Kina Uhalali wa Kukalia Ofisi wakati kuna Vijana wana Nguvu wapo mtaani..

Kizee hata Kusoma tu mafaili kinaita Mtu akisomee ila kuachia Ofisi hakitaki πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Kwahio kwa kuacha nguvu kazi ya miaka 25 na kukumbatia wazee wa above 45 years ndio kutaongeza productivity?
 
Hii inaweza saidia kupunguza tatizo la ajira nchini ikibidi kutoka miaka 60 mpka 45 au 50 ili vijana nao wapate nafasi kwani hii itatoa nafasi nyingi katika kada mbalimbali .
Umaskini ni mbaya sana.
Kama kijana ametoka fresh chuoni akiwa hana majukumu zaidi ya kujikimu yeye mwenyewe tu ameshindwa kujiajiri, Amini akistaafu akiwa na miaka 45 akiwa na majukumu ya kifamilia ndio hatoweza kabisa kujiajiri
 
Kwahio kwa kuacha nguvu kazi ya miaka 25 na kukumbatia wazee wa above 45 years ndio kutaongeza productivity?
Hujawahi Kusikia Kuwa Experience Makes Better?

kipindi Naanza Kazi Miaka ya 2000..
Nakumbuka Ilikuwa ni mwaka 2002 kama Sikosei au 2003 hivi Nilikuwa nfanya kazi na Mzee Mmoja alikuwa anasifika Hospitali Nzima alikuwa kafanya kazi Maabara kwa Miaka 38 alikuwa ukimpelekea Choo (kinyesi) apime alikuwa Akisikia Harufu tu anakuambia Wadudu wote waliopo kwenye Choo kabla ya Kupima Na Akienda Kupima unakuta Kweli..

Ukiacha Hiyo daktari Mwenye Experience Kubwa anaweza Kujua shida ya Mgonjwa Kutokana na Experience yake na wagonjwa mbalimbali bila hata Kumuuliza au Kusikia maelezo yake Tunaita Spot diagnosis..

Unasema Nguvu kazi?

Nguvu kazi ambao bado wanahitaji Kufundishwa!

Unajua Ukiwa kazini na Ukiwa Chuoni ni Vitu viwili tofauti tena Ukute Hivi Vijunior Degree mnaviita Sijui Bachelor Degree hivi vyanafunzi vyenye Degree Moja..

Huwa vinakuja Tunaviassigns kwa Supervisor wa Diploma Na wanavifundisha Kazi kwa miaka Miwili ndo vinaanza Kuwa vi Junior Staff..

Mwaka wa Tatu mpaka Wanne ndo wanakuwa Angalau Junior wenye Uelewa na Kazi ili waupate u seniority Wanatakiwa angalau wawe kazini kwa Miaka angalau 9 au Kumi..

Si kwamba nakashfu ila Kiukweli Watu wenye Bachelor Bado sana Kuwaachia Office Angalau Awe na Experience ya Miaka kuanzia Mitatu.. Ni bora Nimpe Ofisi Mwenye Certificate au Diploma ila Sio Bachelor Nimepita Huko Kote najua na Ndo maana Nasema..

Unafikiri waziri Mkuu kasema Bahati mbaya?🀣🀣

Ila Huu mjadala Huu 🀣🀣🀣
 
vichawi sana hvyo
 
mjadala umekua nongwa
 
Miaka 45 au 50 ni miaka michache sana kazini. Let's say unaanza kazi una miaka 30 ina maana utatumika miaka 15 au ishirini tu unarudi mitaani tena ukiwa kijana mbichi. Kama vipi hizo ajira ziwa za mikataba ya miaka mitano, mitatu au mwaka mmoja tu ili kupisha wengine wasio na ajira kama ni rahisi hivyo. Kwa mtindo huo ufanisi wa kazi utashuka sana na hakuna atakayeenda chuoni kwenda kupoteza muda wa kusoma kisha kuja kutumika kwa muda mfupi
 
duuh miaka 20 unaona michache ? umri wa kijana huu
 
Hii inaweza saidia kupunguza tatizo la ajira nchini ikibidi kutoka miaka 60 mpka 45 au 50 ili vijana nao wapate nafasi kwani hii itatoa nafasi nyingi katika kada mbalimbali .
Bado haiwezi saidia wanahitimu ni wengi kuliko wanaostaafu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…