Wazungu kuja kufanya mikutano ya Injili ya Kilokole litazamwe kwa umakini

Tuwe macho kwani hata wamisionari walioleta dini walikuwa na nia ya kuitawala Afrika. Walituachia Biblia tuendelee kufunga macho kwa kusali ila wao wanachapa kazi.
 
Huduma walizotupa ni kama unampa mtoto pipi mdomoni huku unamfinya, atavumilia maumivu ili aendelee na utamu wa pipi.
 
Kuna Mnigeria mmoja mwenye kanisa lake moja tu mjini Dar alikuja kufanya mikutano ya injiri mwaka flani. Sadaka zoote za siku tano alikusanya yeye na baada ya kumaliza akapita bureau de change kubadilisha na kupata dollars then akasepa

Kanisani kwake TZ aliwaachia msaala wa kulipa madeni yote ya maandalizi ya mikutano ile na waumini wakaanza kuchangishwa kulipa madeni

Imani kwa sasa wengi wamezigeuza kuwa vyanzo vya mapato. But surely, tunahitaji kweli manabii kutoka Nigeria? Yaani Tanzania nzima kanisa lipo moja tuu na watu hawashtuki tu?
 
Mkuu stress zingine ni za kujitakia na hakika zitakupeleka kaburini kabla ya muda wako bure tu. Achana nazo!.

Hujawahi wakubali wazungu ila hapo unachat kwa kutumia simu zao na teknolojia yao, unatumia magari yao na ukiumwa wa kwanza kwenda hospitali kutumia dawa zao.

Usijenelolaizi mkuu utapata depression very soon. Yapo mazungu mengine makorofi kama ambavyo wapo wamakonde wengine machizi ila achana na dhana kuwaza wazungu ni wabaya mara wanataka kukuibia utajiri wako mara wanataka kukuua
 
Acha wivu, kunywa maji m

Hawajaanza kuja leo, tangu miaka hiyo wazungu wanakuja kuhubiri injili
 
Futa kauli yako mkuu sidhani kama kuhubiri neno la Mungu kwa imani ya mtu husika ni jambo la kijinga.
Jiepushe na chuki mkuu hakuna aliyekamilika dunia hii lakin wenye neema ya kueneza habari njema si watu wajinga usipende kuhukumu nawe usihukumiwe.
One love One people usitengeneze matabaka kwa kigezo cha rangi za ngozi zetu.
 
Fafanua"ukristu ulikuwa Afrika kabla ya wamisionari" Yesu alizaliwa Uyahudini, nani angefahamisha Afika kama yupo? Labda useme kuna Yesu Mwafrika. Hakika tulipokea neno bila kuhoji.
 
Fafanua"ukristu ulikuwa Afrika kabla ya wamisionari" Yesu alizaliwa Uyahudini, nani angefahamisha Afika kama yupo? Labda useme kuna Yesu Mwafrika. Hakika tulipokea neno bila kuhoji.
Inshu ni wamisionary na ukristo ama inshu ni eneo Yesu alipozaliwa?.
Ni wapi nimeuliza ama nimekanusha suala la Yesu kuzakuliwa uyaudini?.

Unakumbuka vizuri maudhui ya comment iliyofanya nikukot?.
 
Hii mikutano ya injili ya wazungu ilianza zamani za kale,tangu miaka ya 90,maubili kama haya yalikuwa yanafanyika pale jangwani Dar,
 
Hizo ni project za magumashi. Kuna wapelelezi. Kuna waganga njaa na kuna wahubiri. Ila ndio dunia yetu ilivyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…