Kama hilo halitafanyika haitakuwa rahisi kuishinda CCM, upinzani utoke kwenye kuamsha hisia pekee
"Upinzani unaamsha hisia"? Mkuu 'Smart Dude', nina kiasi fulani cha heshima kwako kutokana na hii michango unayotoa hapa, lakini nadhani huipi tafakuri ya kutosha.
Hivi wewe unawaonaje waTanzania! Kuwa ni watu duni sana wanaopokea tu kuamshwa hisia na wanasiasa?
Mfano wa Karatu na uadmire sana - ni ngumu sana kuishinda CDM karatu, au mfano wa Tunduma ya mwakajoka - hii inajumuisha kuweka wagombea wanaoappeal kwenye makundi yote na wenye ushawishu (mfano Karatu na Slaa, Mch Natse; Moshi na Ndesamburo; Sugu na Mbeya yake; Prof Jay na Mikumi yake; hawa ni mfano wa watu walokuwa na ushawishi sio wa Chama chao tu lakini makundi mengi yaliwaona kama reliable) sio zile habari za kina Wenje Mwanza na Pambalu Nyamagana (watu wa aina hii watashinda mara moja tu kwa upepo ukivumia kwao lakini hawawezi kusustain next election) upinzani ukiwa na majimbo angalau 50 hadi 100 yenye uhakika wa namna hiyo, CCM itakuwa inaelekea kuondoka.
Haya yote unay yaandika hapa ni maswala ambyo chama chochote cha siasa kinabidi kuyafanya; na CHADEMA wanayafanya hata kama wewe huyaoni. Hiyo ni programu ya chama chochote makini. Usitegemee CHADEMA wawe wanaimba tu "NO REFORM, NO ELECTION", na kubaki hivyo hivyo bila ya kuendelea kujijenga katika ngazi zote.
Ungekuwa ni mfuatiliaji wa maswala kama hayo humu JF, ungekuta kwamba miaka yote tumewahimiza CHADEMA wasipuuze waliko waTanzania, mitaani, vijijini n.k.
Kwa hilo siyo jambo jipya.
Jambo jipya ambalo wewe kwa sababu zako uzijuazo ni kutoona jinsi CCM yenyewe, pamoja na muundo wao mzuri inavyovurugwa na viongozi wao wa juu wanaotoka kabisa katika miiko ya chama hicho na kufanya mambo tofauti kabisa. CCM imekwisha jiundia anguko lake yenyewe; na ndiyo unayopaswa kuielekezea hayo "MATUKIO" unayoyazungumzia hapa.
Lakini kwa sasa ambapo CCM inaweza shinda majimbo 200 bila hata kampeni ya kishindo (mfano Karibu majimbo yote ya Dodoma, Simiyu, Shinyanga, Tanga, Tabora, Mwanza, Songea, Njombe, Iringa, Pwani, Singida, katavi, ) maana yke kama kila mkoa una majimbo 10 hapa CCM watapta majimbo si chini ya 115 hata hawatafanya kampeni intensively (ndiyo maana kuna muda wanatuletea wabunge ili mradi tu - wana uhakika na ushindi sana) , na wapinzani majimbo yasiyozidi 5 tu. daaah!!!!!! Kwa lugha Rahisi hapa CCM kwa mikoa 12 tu watakuwa wanaelekea kupata simple majority bungeni - wote tungependa hata bungeni pabalance angalau 60% kwa 40% lakini ukweli hata hii reality bado sana kuifikia kwa miaka mingi mbele, utashanga tunapoongelea kuiondosha kabisa CCM... aisee kazi kubwa inatakiwa kufanyika kabla hatujaanza kuota: ni ukweli mchungu lakini ndio ukweli ..
Mkuu 'Smart', fanya hivi:
Rudi nyuma katika chaguzi zote unazowasifia hapa CCM. Angalia kwanza idadi ya wapiga kura waliowapa CCM ushindi. Usiishie hapo, hata katika idadi hiyo angalia mizengwe mingapi iliyofanyika kabla, wakati, na baada ya upiga kura. Huo ushindi mkubwa unaowapa CCM ni kama wewe upo nchi nyingine tofauti kabisa na hapa tulipo sasa hivi!
Sijui ni sababu zipi zinakufanya wewe usielewe maana ya Samia Suluhu Hassan na GENGE lake wang'ang'anie kufanyika uchaguzi katika mazingira yaleyale unayo wapa ushindi wewe?
Kwa maana hiyo, nakuona hapo ukishangilia vile vile kama wao ushindi mkubwa uliopatikana katika uchaguzi wa serikali za mitaa 2024, au siyo? Na sasa unasubiri kuwapongeza kwa maandalizi hayo mazuri kwa ushindi watakaoupata Oktoba!!
Niseme tu kwamba unanishangaza sana!