Wengi wanaotaka wake zao wasifanye kazi wana upeo mdogo wa kufikiri halafu ni wabinafsi

Wengi wanaotaka wake zao wasifanye kazi wana upeo mdogo wa kufikiri halafu ni wabinafsi

Kwani akifanya kazi hawezi kuwa pambo au kumburudisha mumewe?

Kuna wanawake wanaofanya kazi na bado ni warembo kuliko wanaokalizwa nyumbani.
Hoja yako haina mashiko
Japo Sina shida kabisa na mwanamke kufanya kazi ila ukweli ni kwamba, mwanamke akiwa anafanya kazi mwanamme lazima ukose huduma mhimu nyumbani.
 
Mwanamke ni pambo hatakiwa kufanya kazi yeyote zaidi yakumburudisha mume wake.

Ukishamuoa mwanamke amebadili koo, kutoka ukoo wao kuja upande wa mume, ndio maana wengine hubadili mpaka majina ya wazazi wao.

Baada yakumuoa apaswa kufata Sheria na taratibu za upande wa mmewe, hayo yakuhudumia ndugu zake sijui wadogo zake nimambo y ziada. Mnapooana jukumu kubwa niliangalia familia yenu nyinyi wawili nakujenga mpango mkakati wa watoto wenu baadae waishije. Kila mtu akianza kuhudumia nakutoa kipaumbele kwao hapatakua na familia tena.

Kila mtu ajenge kwao, Kila mtu awe anatuma hela kwao, kwenu nyie wawili mtapajenga lini?.

Mwanamke akikubali kuolewa basi ajue na atambue anaenda kufata taratibu na Sheria za mumewe kama hayupo tayari basi asikubali kuolewa.

Sisi wengine tunaamini hata kama niko wrong basi mwanamke anafaa kunisikiliza na kutii nilichokisema, ndio maana Koo nyingine wanaume hawali sehemu Moja na wanawake jiulize Kwa nini?.

Majukumu yamwanamke ndani ya nyumba yanafahamika na majukum ya mwanamme ndani ya nyumba yanafahamika, Sasa ukitaka kila upande uingilie majukumu ya nwenzake hapatotosha, ndio maana familia nyingi zinaparaganyika Kwa Kila upande kuona unaweza kuhimili kufanya majukumu ya mwenzake.

Kila mtu aishi nakufanya yale ambayo anatakiwa kufanya nakutekeleza majukumu yake.

Nakipindi unaoa au kuolewa basi mwenzi wako ajue lengo ni Nini hasa, mimi nikitaka kuoa basi lengo nimke wangu aniangalizie watoto basi, mengi kama yakija basi niyaziada. Lakini lengo kuu lazima hata yeye alifahamu Kwa mantiki kwamba anaolewa kuja kuwa mama wa nyumbani.
Mods naomba mfute post ya mtoa mada halafu hii comment ndio iwe uzi kamili, hii ni comment bora kwa mwaka huu.
 
Nina mifano hao miwili nakuunga mkono...Father mdogo idea za biashara zake kapewa na mkewe sasa ni billionaire,nina brother nae anamsikiliza sana mkewe kweny biashara yupo mbali sana..

Wanawake ukiwashirikisha mipango yao tena yule mke halali kuna 80% chance ya kufika mbali ...Hata mzee wangu alijenga kupitia mama kwa biashara ndogo ndogo

Tatizo ,mifumo ya familia nyingi upande wa mume wanamfanya mke kama adui wao ,hawataki awe sehemu ya mipango ya mtoto wao(mume) japo kuna ndoa...

Hilo suala naunga mkono hata ukifuatilia matajiri wengi ndio wamefanikiwa hivyo ndio ule msem " Nyuma ya kila mwanaume aliyefanikiwa kuna mwanamke"
Eee Mungu saidia wanawake wa jf wasije wakaona hiii comments
 
Back
Top Bottom