Wengi wanaotaka wake zao wasifanye kazi wana upeo mdogo wa kufikiri halafu ni wabinafsi

Wengi wanaotaka wake zao wasifanye kazi wana upeo mdogo wa kufikiri halafu ni wabinafsi

Kwani akifanya kazi hawezi kuwa pambo au kumburudisha mumewe?

Kuna wanawake wanaofanya kazi na bado ni warembo kuliko wanaokalizwa nyumbani.
Hoja yako haina mashiko
Muda wa kufanya hayo atautoa wapi na kuna ratiba ya bosi kazini, huyu ni binadamu hawezi kuhudumia mabosi wawili.
 
Wewe ukienda kazini unashindwa kutoa huduma za kitandani kwa mkeo?
Ukitoka kazini unashindwa kuipa nyumba yako furaha?
Kuna tofauti sana kati ya mwanamke na mwanamme hasa kwenye maswala ya familia. Mwanamme siku zote ni mpita njia tu. Nyumba ni mwanamke.

Iwapo mwanamke atachelewa kuja nyumbani au akifika tu anakaa kwenye kochi analala kama mwanamme mambo huenda mrama.
 
Wanajiremba kwa ajili ya mabosi kazini sio nyumbani
Mkuu Aipolo,

Hili. Si kweli hata wewe kazini huwa unaenda ukiwa msafi, ni kweli unajipamba ili wanawake wengine wakuone?
usafi ni sehemu muhimu kwa mwanadamu na si mtu fulani akuone
Mke anapokuwa msafi unapata credit na wewe unapokuwa msafi atapata credit na kinyume chake ndio ivyo.
 
Kuna tofauti sana kati ya mwanamke na mwanamme hasa kwenye maswala ya familia. Mwanamme siku zote ni mpita njia tu. Nyumba ni mwanamke.

Iwapo mwanamke atachelewa kuja nyumbani au akifika tu anakaa kwenye kochi analala kama mwanamme mambo huenda mrama.

Hiyo ni kwa Mujibu wa dini gani au sheria ipi?
Kama ni mkristo kweli kasome mithali 31 utajua sifa za mke bora na mwema.
Kama mke hana sifa hizo huyo sio mke.
Na kama anasifa za mke bora hawezi kuwa hivyo unavyotaka awe lazima muachane na haoni hasara yoyote
 
Back
Top Bottom