Wengi wanaotaka wake zao wasifanye kazi wana upeo mdogo wa kufikiri halafu ni wabinafsi

Wengi wanaotaka wake zao wasifanye kazi wana upeo mdogo wa kufikiri halafu ni wabinafsi

Ndio nakuuliza unaweza kujenga Ukweni na kimshahara chako ambacho hata wewe mwenyewe hakikutoshi?
Kwa nini ujipendekeze kujenga ukweni, huku mama mkwe wako anawatoto wakiume aliowazaa kama wewe?.

Mambo mengine niyaziada hayatakiwi kuyatilia maanani, au Dada yako, mdogo wako wakike akiolewa ungependa shemeji yako ndio amjengee mama/Baba yako?.
 
Kwa nini ujipendekeze kujenga ukweni, huku mama mkwe wako anawatoto wakiume aliowazaa kama wewe?.

Unaona sasa ulivyo mbinafsi.
Mtoto ni mtoto awe wakike au wakiume.
Na wote wanahaki sawa kwa mzazi.

Wewe ukizaa watoto wakike wote hawataki wa na wajibu wa kukutunza?
 
Hukutakiwa kuongelea habari za ndoa kama hujui majukumu ya mume.

Majukumu ya mume na mke ni yaleyale kwa sababu wao ni mwili mmoja. Au wewe unazungumzia wale wanawake mnaowanunua na kuwaita mke huku mkiwageuza vijakazi na misukule yenu.
 
Unaona sasa ulivyo mbinafsi.
Mtoto ni mtoto awe wakike au wakiume.
Na wote wanahaki sawa kwa mzazi.

Wewe ukizaa watoto wakike wote hawataki wa na wajibu wa kukutunza?
Mwanamke akiolewa ukoo automatically umepungua, na mwanaume akioa basi ukoo umeongezeka. Ukishatambua Hilo mambo mengine hayatokusumbua.

Nawakifanya hivyo nijambo laziada ambalo kwangu hatawasipofanya sintowalaumu.
 
Mwanamke ni pambo hatakiwa kufanya kazi yeyote zaidi yakumburudisha mume wake.

Ukishamuoa mwanamke amebadili koo, kutoka ukoo wao kuja upande wa mume, ndio maana wengine hubadili mpaka majina ya wazazi wao.

Baada yakumuoa apaswa kufata Sheria na taratibu za upande wa mumewe, hayo yakuhudumia ndugu zake sijui wadogo zake nimambo ya ziada. Mnapooana jukumu kubwa nilakuangalia familia yenu nyinyi wawili nakujenga mpango mkakati wa watoto wenu baadae waishije. Kila mtu akianza kuhudumia nakutoa kipaumbele kwao hapatakua na familia tena.

Kila mtu ajenge kwao, Kila mtu awe anatuma hela kwao, kwenu nyie wawili mtapajenga lini?.

Mwanamke akikubali kuolewa basi ajue na atambue anaenda kufata taratibu na Sheria za mumewe kama hayupo tayari basi asikubali kuolewa.

Sisi wengine tunaamini hata kama niko wrong basi mwanamke anafaa kunisikiliza na kutii nilichokisema.

Ndio maana Koo nyingine wanaume hawali chakula sehemu Moja na wanawake jiulize Kwa nini?. Hili nikuwafunza watoto wakiume na kike Kila mtu kujua majukumu ya baba yake na mama yake niyapi , na namna mwanamke anavyopaswa kumtii na kumuandalia chakula mumewe.

Majukumu yamwanamke ndani ya nyumba yanafahamika na majukum ya mwanamme ndani ya nyumba yanafahamika, Sasa ukitaka kila upande uingilie majukumu ya nwenzake hapatotosha, ndio maana familia nyingi zinaparaganyika Kwa Kila upande kuona unaweza kuhimili kufanya majukumu ya mwenzake.

Kila mtu aishi nakufanya yale ambayo anatakiwa kufanya nakutekeleza majukumu yake.

Nakipindi unaoa au kuolewa basi mwenzi wako ajue lengo ni nini hasa, mimi nikitaka kuoa basi lengo nimke wangu aagalie watoto basi, mengi kama yakija basi niyaziada. Lakini lengo kuu lazima hata yeye alifahamu Kwa mantiki kwamba anaolewa kuja kuwa mama wa nyumbani.
Dunia inabadilika inabidi majukumu yatafakariwe upya.

Mfano tu uwepo wa vitu kama mashine za kufulia, kuoshea vyombo kunarahisisha mambo

Mtasema ni ghali lakini hizi mashine zitakuja kuwa kawaida kama tv na pasi zilivyo sasa tofauti na zamani

Narudia tena, dunia inabadilika
 
Back
Top Bottom