Wengi wanaotaka wake zao wasifanye kazi wana upeo mdogo wa kufikiri halafu ni wabinafsi

Wengi wanaotaka wake zao wasifanye kazi wana upeo mdogo wa kufikiri halafu ni wabinafsi

Mwanamke akiolewa ukoo automatically umepungua, na mwanaume akioa basi ukoo umeongezeka. Ukishatambua Hilo mambo mengine hayatokusumbua.

Nawakifanya hivyo nijambo laziada ambalo kwangu hatawasipofanya sintowalaumu.
Hizo ni blue print za mifumo dume ambazo umeaminishwa hivyo.

mtoto wakike alikuwa apelekwi shule sababu yeye alikuwa kama mtumwa tu itafika umri atachukuliwa na mwanaume kwenda kumtumikia.

Hii ni karne ya ngapi? Unataka dunia iendelee kuwa vile vile miaka 1000 nyuma?
 
Kutokufanya kazi ni kitu kigumu sana.

Hizo ni wishes tu ambazo kiuhalisia wa maisha hazipo, hakuna hata mtu tajiri Mke wake ambaye hafanyi kazi.

Kazi ni kipimo cha utu.
Tambua kitu kikiwa kigumu kwako haimaanishi ni kigumu kwa kila mtu

Mimi nimesema nikija kuwa Bilionea mke wangu sitaki afanye kazi yoyote, kama unabisha nipe billion 3 Halafu uone kama mke wangu atatoka kwenda kuhangaika na mafoleni huko barabarani
 
Kwanini umeuliza kwamba ni jukumu lake? Kuna limit ya kuhudumia ndugu zako?
Mbona wanaume tunatuma pesa nyumbani kwetu na tunahudumia

Asipofanya kazi yeye kwao anawasaidia vipi?
Kunakitu ndhani hukifahamu, mnapofunga ndoa mke na mume, tayari mmtoka katika familia zenu mnakuja kuanzisha familia yenu. So jukumu lenu kuu ni kuihudumia hii familia yenu.
 
Tambua kitu kikiwa kigumu kwako haimaanishi ni kigumu kwa kila mtu

Mimi nimesema nikija kuwa Bilionea mke wangu sitaki afanye kazi yoyote, kama unabisha nipe billion 3 Halafu uone kama mke wangu atatoka kwenda kuhangaika na mafoleni huko barabarani
Kama yupo mtu ambaye hafanyi kazi hapa duniani basi tuonyeshe.

Tuishie hapa mkuu” kama unabisha nipe bilion 3 Halafu uone kama Mke wangu atatoka kwenda kuhangaika”

😀Hongera mkuu
 
Kutokufanya kazi ni kitu kigumu sana.

Hizo ni wishes tu ambazo kiuhalisia wa maisha hazipo, hakuna hata mtu tajiri Mke wake ambaye hafanyi kazi.

Kazi ni kipimo cha utu.
Hakuna tajiri na hatokuwepo pale Top 10 ambaye mkewe anafanya kqzi nje ya himaya yake...Nikiwa na maana biashara zake.. Hakuna hilo usidanganywe.!

Matajiri wengi wake zao wapo kweny management ya biashara zao ... Magufuli tu alimwachisha mkew ualimu..
 
Ndio maana nilimjibu huyo jamaa alisema Mke wake yeye hatafanya kazi.

Nikaomba anionyeshe mtu ambaye hafanyi kazi kabisa.
 
Kunakitu ndhani hukifahamu, mnapofunga ndoa mke na mume, tayari mmtoka katika familia zenu mnakuja kuanzisha familia yenu. So jukumu lenu kuu ni kuihudumia hii familia yenu.
Umenena vyema!
Kesi ikibaki hivi hupaswi kuhangaika na familia yako kwa aina yoyote ile sababu mbahudumia familia yenu.
Na uhakikishe Mke wako anapata matunzo yote.
ILA kama ni hawa tunaowaona mtaani Mke nguo mpaka inaisha, mafuta hakuna huna sababu ya kumkataza
 
Ndio maana nilimjibu huyo jamaa alisema Mke wake yeye hatafanya kazi.

Nikaomba anionyeshe mtu ambaye hafanyi kazi kabisa.
Maana ukiangalia k lyn aliachishwa kazi ya mziki na Mengi ili kumsaidia baadhi ya biashara...Lazaro nyalandu nae yule kamchukua Faraja kotta ndio maana unamuona kimya ila anasimamia biashar za mzeee....Wale waarabu huwezi kuona wake zao ila wapo kweny biashara za wanaume zao .

Rejea kuna kipato ukiwa nacho ni best akasimamia ,mke kuishi nae karibu ni bora kuwa kama partner wako kweny biashara ila hizi ajira mara kahamishwa mkoani ni utapeli hazifai.
 
Hizo ni blue print za mifumo dume ambazo umeaminishwa hivyo.

mtoto wakike alikuwa apelekwi shule sababu yeye alikuwa kama mtumwa tu itafika umri atachukuliwa na mwanaume kwenda kumtumikia.

Hii ni karne ya ngapi? Unataka dunia iendelee kuwa vile vile miaka 1000 nyuma?

Kama yupo mtu ambaye hafanyi kazi hapa duniani basi tuonyeshe.

Tuishie hapa mkuu” kama unabisha nipe bilion 3 Halafu uone kama Mke wangu atatoka kwenda kuhangaika”

😀Hongera mkuu
Wapo wengi hawana hata idadi. Usipende kulazimisha kila mtu aishi kama unavyotaka wewe
 
Wapo wengi hawana hata idadi. Usipende kulazimisha kila mtu aishi kama unavyotaka wewe
Mkuu Miti
Mimi sijakataa nilitaka kumuona huyo mtu ambaye hafanyi kazi.
Tutajie ili wote tufahamu.

Maana matajiri wote wakubwa duniani wake zao wanafanya kazi ndio nikataka kujua huyo mtu ambaye hafanyi kazi kabisa ni nani?
 
Mwanamke ni pambo hatakiwa kufanya kazi yeyote zaidi yakumburudisha mume wake.

Ukishamuoa mwanamke amebadili koo, kutoka ukoo wao kuja upande wa mume, ndio maana wengine hubadili mpaka majina ya wazazi wao.

Baada yakumuoa apaswa kufata Sheria na taratibu za upande wa mumewe, hayo yakuhudumia ndugu zake sijui wadogo zake nimambo ya ziada. Mnapooana jukumu kubwa nilakuangalia familia yenu nyinyi wawili nakujenga mpango mkakati wa watoto wenu baadae waishije. Kila mtu akianza kuhudumia nakutoa kipaumbele kwao hapatakua na familia tena.

Kila mtu ajenge kwao, Kila mtu awe anatuma hela kwao, kwenu nyie wawili mtapajenga lini?.

Mwanamke akikubali kuolewa basi ajue na atambue anaenda kufata taratibu na Sheria za mumewe kama hayupo tayari basi asikubali kuolewa.

Sisi wengine tunaamini hata kama niko wrong basi mwanamke anafaa kunisikiliza na kutii nilichokisema.

Ndio maana Koo nyingine wanaume hawali chakula sehemu Moja na wanawake jiulize Kwa nini?. Hili nikuwafunza watoto wakiume na kike Kila mtu kujua majukumu ya baba yake na mama yake niyapi , na namna mwanamke anavyopaswa kumtii na kumuandalia chakula mumewe.

Majukumu yamwanamke ndani ya nyumba yanafahamika na majukum ya mwanamme ndani ya nyumba yanafahamika, Sasa ukitaka kila upande uingilie majukumu ya nwenzake hapatotosha, ndio maana familia nyingi zinaparaganyika Kwa Kila upande kuona unaweza kuhimili kufanya majukumu ya mwenzake.

Kila mtu aishi nakufanya yale ambayo anatakiwa kufanya nakutekeleza majukumu yake.

Nakipindi unaoa au kuolewa basi mwenzi wako ajue lengo ni nini hasa, mimi nikitaka kuoa basi lengo nimke wangu aagalie watoto basi, mengi kama yakija basi niyaziada. Lakini lengo kuu lazima hata yeye alifahamu Kwa mantiki kwamba anaolewa kuja kuwa mama wa nyumbani.
Hawa vijana walamba lips wa kipindi hiki hawatakuelewa sababu wanataka majukumu yao yabebwe na wake zao.

Mwanamke ni pambo la nyumba ikiwa na maana yeye mwenyewe apendeze, awaweke watoto wakiwa safi, mume wake aende kazini akiwa msafi wa mwili na akili pamoja na usafi wa ndani.

Mwanamke huyu akienda kazini nani atafanya hayo?
Kama ni hivyo si angebaki kwa wazazi wake afanye kazi ili asomeshe wadogo zake 🤔
 
Umenena vyema!
Kesi ikibaki hivi hupaswi kuhangaika na familia yako kwa aina yoyote ile sababu mbahudumia familia yenu.
Na uhakikishe Mke wako anapata matunzo yote.
ILA kama ni hawa tunaowaona mtaani Mke nguo mpaka inaisha, mafuta hakuna huna sababu ya kumkataza
Sasa hapa inategemea mtu mwenyewe, nakupa mfanohai, mimi mwenyewe nilikataa mke wangu kufanya kazi, kwa sasa namgai laki moja na nusu kila mwezi, hiyo ni hela yake binafsi atumie atakacho simuulizi, na walanhaijotoke mwezi nakaiaitisha na hii hela hua inapanda kila baada ya muda flani.
 
Maana ukiangalia k lyn aliachishwa kazi ya mziki na Mengi ili kumsaidia baadhi ya biashara...Lazaro nyalandu nae yule kamchukua Faraja kotta ndio maana unamuona kimya ila anasimamia biashar za mzeee....Wale waarabu huwezi kuona wake zao ila wapo kweny biashara za wanaume zao .

Rejea kuna kipato ukiwa nacho ni best akasimamia ,mke kuishi nae karibu ni bora kuwa kama partner wako kweny biashara ila hizi ajira mara kahamishwa mkoani ni utapeli hazifai.
Mkuu Accumen,

Unajua jamaa amesema Mke wake hatafanya kazi kabisa.

Ndio maana nikataka kujua hicho kiumbe ambacho hakifanyi kazi na kipo na afya au wewe tusaidie
 
WENGI WANAOTAKA WAKE ZAO WASIFANYE KAZI WANAUPEO MDOGO WA KUFIKIRI ALAFU NI WABINAFSI

Anàandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Chizi sio lazima uokote Makopo, kuna Chizi Fresh ambao ndio wengi wapo kundi hili tena wengine wasomi. Alafu kuna ambao ni Chizi Maarifa hawa wengi ukiwaona kwa mbali unaweza kudhani wako timamu lakini ukiwatazama kwa ukaribu ni wendawazimu.

Unakuta kajamaa kametoka familia Maskini, kameoa kutoka Familia Maskini. Kanafanya kazi iwe kwa kuajiriwa au kujiajiri lakini pato lake kwa mwezi hata Milioni moja halifiki.
Lakini ukikasikiliza mawazo yake kuhusu uchumi na mahusiano utabaki kuona kalivyo na upeo mdogo.

Yaani kisa umenunua mwanamke kwa bei ya jumla(kutoa mahari) labda shilingi milioni nne. Basi Mwanamke huyo ambaye sasa ataitwa mkeo unasema asifanye kazi kisa umemuoa.

Ukiulizwa kwa nini asifanye kazi? Huna hoja ya maana hata moja zaidi ya kutokujiamini, ubinafsi na ukandamizaji kama sio unyanyasaji.

Unamwambia mkeo asifanye kazi au asimiliki kipato kingi tena inafikia hatua kwa uzuzu wako unamhujumu mkeo na kumuwekea vikwazo ili asifanikiwe. Ati unaogopa atakunyanyasa ati atakuwa jeuri. Chizi weeeh!

Mkeo asifanye kazi, unapesa za kumhudumia mahitaji yake yote?
Alafu wengi wenye mtazamo kama huu unakuta Wake zao hata mafuta ya kupaka hawana, nguo wanazovaa mtumba, tena bora mtumba lakini ziwe nyingi. Lakini hata pesa ya kuwanunulia wake zao nguo walau kila mwezi nguo moja au mbili hawana. Mke kapauka, kazeeshwa. Yaani hatamaniki tena. Kila siku kumlisha mkeo Maharage kazi kujambajamba. Alafu unakuta jitu linasema linahudumia mke. Alafu halitaki mkewe afanye kazi. Ili angalau pesa ya kubadilisha chakula hapo nyumbani iwepo sio kila siku ugali na mchicha au maharage. Nyama na samaki mpaka sikukuu. Familia inapitisha Wiki hata maziwa hakuna. Alafu ulivyo chizi unaona sawa tuu. Alafu ukijaribu mtandaoni huku ooh! Mwanamke asifanye kazi utadhani umemudu mahitaji yake. Mwehu wewe!

Watoto wako ada zenyewe zinakusumbua, lishe yenyewe hawali. Utapiamlo na kifaduro kinawasumbua. Watoto mpaka imefikia hata uwezo wa kufikiri hawana Kwa sababu kila siku unawalisha chakula kingi cha wanga kama ugali, mihogo, maandazi na maujiuji ya nafaka. Ilhali kiafya watoto chini ya miaka 20 wanatakiwa kula protein nyingi kuliko kundi jingine la chakula ili miili yao ijengwe vyema. Vyakula vya protini ambavyo vinatakiwa viwe vingi katika mlo wenu hapo nyumbani ni Samaki, nyama, maharage, maziwa, mayai n.k.
Lakini kwa vile kipato chako ni duni huwezi kuhudumia hivyo. Alafu kwa vile tayari unakifaduro cha ubongo huoni kama unahitaji usaidizi na kwa ubinafsi wako unataka watoto wako nao wakose lishe kama wewe ulivyokosa. Ati mke asifanye kazi au asikusaidie majukumu. Kwa huduma gani unazotoa mwehu wewe!

Haya, mshahara wako wenyewe haukutoshi kutunza Wazazi wako.
Alafu hutaki mkeo asifanye kazi. Hivi unafikiri wazazi wake mwanamke watahudumiwa na kutunzwa na nani kama sio huyo mke wako. Mbuzi wewe.

Pesa yako hata milioni moja haifiki kwa mwezi. Unataka wadogo wa mkeo wahudumiwe na nani?
Unataka ile nyumba ya wazazi wa mkeo ifanyiwe ukarabati na nani kama sio mkeo.

Alafu haya machizi Fresh hapohapo unayasikia yakisema, usijenge Ukweni, mara Usitoe pesa Ukweni. Alafu hapohapo unayakuta yanazuia Wake zao wasifanye kazi. Hivi kama sio Ushetani na laana hizo ni kitu gani? Hivi kuna ubinafsi na ukatili wa kutisha zaidi ya huo?

Bado umfulishe na kumfanyisha makazi mengi bila kumpa lishe bora. Zaidi ya hapo umpige kisa ameona mambo sio mambo na umemgeuza msukule wake hapo.

Embu acheni Upumbavu wenu.
Ni mara elfu Mwanamke asioelewe au awe single Mother alee Watoto wake kitabutabu kuliko kuishi na mwanaume mwenye Ushetani wa namna hiyo.

Mwanaume elewa kuwa kama wewe unavyopenda na kuhitaji kuhudumia Wazazi wako ndio hivyohivyo mkeo naye anataka wazazi wake wahudumiwe.

Na ndio maana Watibeli Hawatoi Mahari kwa sababu inaharufu ya manunuzi au biashara ya binadamu kwa visingizio vya kishetani.

Hutaki mkeo afanye kazi alafu ukiombwa pesa ya kuwasomesha wadogo zake unapiga yowe na kulalamika. Wewe mwehu nini.

Na mimi nawaambia Wanawake hasa Watibeli ni lazima wafanyekazi. Kufanya kazi ni amri ya kila kiumbe ili kiwe huru na kujitegemea chenyewe. Binadamu asiyefanya kazi ni mfu.
Mtu mwenye akili na Mwanamke kamili na mke mwema hujisikia aibu na fedheha kumtegemea mumewe kwa kila kitu.

Mimi nimemaliza.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Ni mawazo yako,na yanaweza kua ni ya kipuuzi kwa wengine,kama wewe una ndugu au rafiki amekwama kwakua anawajibika peke yake,nenda kaseme nae huyo,usiwasemee watu,wako wanaoweza kuja hapa na wakakupa masaibu ya unacho jitetea nacho
 
Sasa hapa inategemea mtu mwenyewe, nakupa mfanohai, mimi mwenyewe nilikataa mke wangu kufanya kazi, kwa sasa namgai laki moja na nusu kila mwezi, hiyo ni hela yake binafsi atumie atakacho simuulizi, na walanhaijotoke mwezi nakaiaitisha na hii hela hua inapanda kila baada ya muda flani.
Hakika hili ni jambo jema.
Mimi Mke wangu huwa tukiamka kila siku tunaondoka maana tunafanya kazi sehemu moja na yeye ndio msimamizi wa biashara.

Hili unalofanya wewe ni wanaume 1% wanafanya hivi, wanawake wengi mpaka nguo, au lotion au gel yakuogea wanakosa na bado n mwanaume anakazana hataki mke afanye kazi.

Hongera sana mkuu
 
Mkuu Miti
Mimi sijakataa nilitaka kumuona huyo mtu ambaye hafanyi kazi.
Tutajie ili wote tufahamu.

Maana matajiri wote wakubwa duniani wake zao wanafanya kazi ndio nikataka kujua huyo mtu ambaye hafanyi kazi kabisa ni nani?
Acha ubishi wa kijinga.

Nimekuambia nipe billion 3 Halafu uone kama mke wangu atatoka kwenda kuhangaika na mafoleni huko barabarani.

Kama huna hiyo hela subiri mimi nitakapopata utaona mke wangu hafanyi kazi yoyote

Huu ni msimamo wangu usitake kunipangia mimi maisha
 
Mkuu Accumen,

Unajua jamaa amesema Mke wake hatafanya kazi kabisa.

Ndio maana nikataka kujua hicho kiumbe ambacho hakifanyi kazi na kipo na afya au wewe tusaidie
Nadhani anamaanisha kazi za kuajiriwa, maaba kazi za ndani tu pekeyake zinatosha na ndio maana watu wanaajiri madada wakazi na wanawakipa kwakua kazi za ndani pekeyake na nyingi. Kibwa hapa wale wanaokataa wake zao wasiajiriww basi wawe wanawakipa kulingana na vipato vyao.
 
Ni mawazo yako,na yanaweza kua ni ya kipuuzi kwa wengine,kama wewe una ndugu au rafiki amekwama kwakua anawajibika peke yake,nenda kaseme nae huyo,usiwasemee watu,wako wanaoweza kuja hapa na wakakupa masaibu ya unacho jitetea nacho
Safi kabisa
 
Nadhani anamaanisha kazi za kuajiriwa, maaba kazi za ndani tu pekeyake zinatosha na ndio maana watu wanaajiri madada wakazi na wanawakipa kwakua kazi za ndani pekeyake na nyingi. Kibwa hapa wale wanaokataa wake zao wasiajiriww basi wawe wanawakipa kulingana na vipato vyao.
Kazi yake kubwa nimesema itakuwa ni kula, kulala na kufanya mazoezi ya viungo
 
Hakika hili ni jambo jema.
Mimi Mke wangu huwa tukiamka kila siku tunaondoka maana tunafanya kazi sehemu moja na yeye ndio msimamizi wa biashara.

Hili unalofanya wewe ni wanaume 1% wanafanya hivi, wanawake wengi mpaka nguo, au lotion au gel yakuogea wanakosa na bado n mwanaume anakazana hataki mke afanye kazi.

Hongera sana mkuu
Mimi ni mtu wa mwsho wa mwezi, nikipokea mshaara kitu cha kwanza natoa hela ya matumizi ya nyumbani namkabizi wife pamoja na hela yake binafsi.
 
Back
Top Bottom