Wengine hatuwezi ku-date na Mwanamke asiyeweza kujilipia nauli na kujinunulia vocha

Wengine hatuwezi ku-date na Mwanamke asiyeweza kujilipia nauli na kujinunulia vocha

Asilimia 80 ya wanawake wa sasa ni wadangaji wanatumia fimbo ya hela kuwachapa wanaume,ikiwa ni wanafki hawana true love nikionaga mwanamke anateseka kweny relationship kisa anampenda jamaa Fulani moyoni mwangu huwa na furaha sina time ya kumuonea huruma malipo ni hapahapa duniani

😂😂
 
Fact kbsa maskin wanaongoza sana kujitolea ktk mapenzi tena wanajua kutunza wanajua kujali
Unakuta mwanaume hana vocha ila kidemu sungura poli kikiomba vocha jamaa anatuma wakat yeye hana vocha
Unakuta kanaume kamemtoa demu out kananunua kuku ya demu kenyewe kanabaki kanameza mate demu anavunja mifupa kenyewe kanacheka
Ila yote ya yote kla mtu ashinde vita vyake, dunian kla mtu amekuja na purpose yke
 
Habari za Sabato!

Kwa kweli Sisi wengine tulishaweka miiko na mstari kuwa Mwanamke asiyeweza kujilipia nauli wala asiyeweza kujinunulia vocha huyo hatuwezi ku-date naye.
Kwanza hatuamini kabisa kuwa Mwanamke mrembo na mzuri anaweza kukosa nauli au vocha. Hilo siwezi kuamini.

Hiyo imetusaidia Sana kuepukana na Wanawake matapeli, Almaarufu wala nauli, wapiga mizinga ya kitoto toto, Wanawake wenye fikara za kimaskini hivi.

Mtoto yupo Arusha au Mwanza au Nairobi mnawasiliana anakuambia likizo anakuja, anajilipia nauli mwenyewe anakuja.

Hao ndio wasichana na Wanawake ambao Kwa kweli ninaweza kuingia nao kwenye mahusiano. Mnakaa mnajadili na mnapiga Stori za maana, sio unakaa na Mwanamke anawaza akiondoka utampa shilingi ngapi. Hizo sio type za Sisi Watibeli.

Vijana hasa ninyi vijana wadogo ambao mmetoka familia Duni, Vijana mnaojitafuta, chukueni ushauri wangu, utawasaidia pakubwa. Hakikisheni mnachukua Wanawake wanaowahitaji ninyi kimapenzi na kimahusiano. Wenye uwezo wa kujilipia Bills ndogondogo. Achaneni na Kutafuta Kupe na kunguni WA kuwanyonya Damu. Shauri yenu.

Asije Mwanamke Maskini akakuletea mawazo yake ya kimaskini aliyoyarithi Huko kwao, kwamba ati wewe mwanaume ndio unatakiwa umenyeke kumtunza, sijui umtumie nauli, sijui vocha sijui Pesa ya Kula, ukiona demu wako anamawazo ya hivyo jua huyo ni Maskini na atakuletea umaskini nyumbani kwako. Huo unaitwa umaskini wa kurithi. Lazima ufe mapema wewe. Lazima uso wako usiwe na Nuru wewe. Lazima ufubae, yaani huo ndio Utapeli ambao Watibeli hatutauruhusu.

Usije ukakubali kuwa mtumwa WA MTU mwingine Kwa vigezo vya kijinga ATI sijui wewe ni Mwanaume. Tena Kwa MTU ambaye hujamuoa, na hata kama umemuoa lakini ni MTU mbinafsi.
Yaani wewe ndio usulubike? Watibeli hatupo hivyo.

Yaani usulubike Wakati kuna wanawake kibao wanaojiweza, wanaoweza kukupenda na mkaenjoi Maisha Kwa kusaidiana wote pasipo ubinafsi.

Yaani upo na Mwanamke ambaye hata hajawahi kukusaidia chochote zaidi ya wewe ndio kuwa msukule wake kisa akupe ngono. Thubutu!

Vijana, eleweni kuwa Mwanamke akikupenda huwezi kuteseka, eleweni kuwa Mwanamke akikupenda atapata nauli na vocha ya kukutafuta tuu.
Vijana eleweni kuwa ukiona Mwanamke wako ni mbinafsi anataka tuu wewe ndio umhudumie ujue huyo hakupendi, jua wewe ni mtumwa wako.

ATI Mwanamke anakuambia kama usiponipa hiki Mimi na wewe basi, na wewe unaanza kuhangaika. Mpumbavu wewe!

Mbona Sisi hao Wanawake hawathubutu kusema hivyo. Usipende kupelekeshwa kijinga jinga!
ATI Mwanamke anakuambia, mwanaume gani huna Pesa alafu lenyewe linalokuambia kazi halina, Pesa Hana, lakini anatumia maneno yake kukuadhibu wewe ili umtumikie. Nawe Kwa ujinga wako na kutokujiamini kwako unajitutumua ili upate Sifa zake. Aliyekuambia Sifa za Mwanamke Maskini zitakusaidia ni Nani?

Umaskini wa fikra,
Umaskini wa Mali
Umaskini wa Roho.

Vijana wangu, kuweni Wanaume. Na uanaume hautatokana na Maoni ya Wanawake juu yako.
Uanaume ni kujitambua, kujua nafasi yako, kujua nini chakufanya. Kuishi kifalme na sio kutumikishwa kama Lofa. Pumbavu!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Umetisha mkuu [emoji120][emoji120]
 
Fact kbsa maskin wanaongoza sana kujitolea ktk mapenzi tena wanajua kutunza wanajua kujali
Unakuta mwanaume hana vocha ila kidemu sungura poli kikiomba vocha jamaa anatuma wakat yeye hana vocha
Unakuta kanaume kamemtoa demu out kananunua kuku ya demu kenyewe kanabaki kanameza mate demu anavunja mifupa kenyewe kanacheka
Ila yote ya yote kla mtu ashinde vita vyake, dunian kla mtu amekuja na purpose yke

Kwa kuongezea zaidi, Maskini wengi ndio husomesha wachumba zao.
Wenye Pesa huo muda hawana
 
Mkuu hao wanawake unaowasema ndiyo Bwana Elon Musk ameamua kuwatengenezea.

Mwanamke hakuombi hata hela ya kununua Peruvian Hair, sembuse ya kwenda kusafisha Kucha Saluni.

Unadate na Mwanamke ambaye hakuombi Vocha si atafanya akili yako ilale, Mwanamke lazima akuombe vi elfu 50, 50 ili akufanye utie bidii kutafuta hela
Uzuri kila mtu Ana hoja zake
 
Hahahahah ataelewa tu, mwanamke hana excuse za kijinga akiwa anakuzimia fulu🤣 hata Depal anajua jinsi ambavyo alikuwa anatumia pocket money kumpelekea muhuni mbususu na zawadi za boxer.
🤣🤣🤣 nampelekea za elf 50
Kesho kutwa namuomba elf 70
 
Dada kwa style hiyo unaweza usipate mwanaume sahihi sio kwamba mwanaume hawezi kutoa hela ya nauli la hasha anachohofia anaweza kukupa usije au akakuona haupo serious ila kwa mwanaume ambaye anaongozwa na hamu ya kufanya ngono ni rahisi kukupa cos ya kutaka utelezi
😂😂😂😂Hapa nilipigwa sana mwisho wasiku wanakuja wenyew na nauli situmi
 
Asilimia 80 ya wanawake wa sasa ni wadangaji wanatumia fimbo ya hela kuwachapa wanaume,ikiwa ni wanafki hawana true love nikionaga mwanamke anateseka kweny relationship kisa anampenda jamaa Fulani moyoni mwangu huwa na furaha sina time ya kumuonea huruma malipo ni hapahapa duniani
Hahahahah wadangaji ndio wako shazi 🤣 mi nachekaga zaidi nikiona mwanaume anajitapa kuhonga demu ambaye hana mkataba naye wa kudumu. Wanaishiaga pabaya sana na majuto ni mjukuu 🤣🤣🤣
 
Hujamwelewa mtoa mada naona umekurupuka kumponda ili upate likes za wadada sijui.

Nilivomwelewa mtoa mada ni kuwa yeye hajakataa kumpa hela mke/mpenzi wake, kwasababu kiuhalisia Na kihaki kabisa hilo ni jukumu letu sisi wanaume kuwapa hela wake/wapenzi wetu, alichokataa Mtibeli ni yeye kutumika.

Na hii ni kwasababu kuna wanawake wana mindset za kishetani, yupo na wewe kwenye mahusiano ili umpe hela na kiuhalisia moyoni hakupendi kabisa na havutiwi na wewe kimapenzi.

Mara nyingi wanawake wanawaambiaga rafiki zao kwenye vijiwe vyao vya story, yule mwanaume sio type yangu, simpendi ila niko naye tu kwenye mahusiano ili nimalizie nyumba yangu, aweze lipa kodi mjini, ajikimu kimaisha, infact hata humu jf wanawake wengi wanakiri kuwa wanaolewa kisa matunzo/pesa ilhali hawavutiwi kimapenzi na waume zao.

Huo ndio utapeli ambao mtibeli ameukataa uttoh2002
Mwamba uko makini sana,hata mm nimejiuliza mbona mtibeli ameeelezea vizuri nahoja zake ziko wazi juu ya upendo baina ya mwanaume na mwanamke...mtibeli anapinga unyanyasaji wa wanawake kwa wanaume kwa kigezo au kisingizio cha mbususu.
 
Back
Top Bottom