Nakuelewa Kwa sababu nilikua na malengo kama yako tokea nikiwa shule ya msingi. Nilifanikiwa Kwa asilimia 98.
Nilianguka na mtu aliyetarajia kuwa mke wangu ila Kwa kua mipango si matumizi , mambo hayakwenda kama ilivyopangwa. Nilichofanikiwa ni kutojihusisha na kimasihara ujana wote hadi pale nilipotaka kupata mwenza wa maisha.
Hilo jambo linahitaji kujikana na udhamirie kutoka ndani ukiwa unajua nini unataka. Lazima uwe na ujihusishe sana na mambo yanayokuweka karibu na uwepo wa Mungu. Vitu Gani unasikiliza, unasoma, unatumia muda wako mwingi, nyimbo zipo unasikiliza na kuangalia, watu Gani wanakuzunguka na unatumia muda mwingi pamoja.
Na mwisho kwanini unataka kukaa mbali na kimasihara, lengo lako hasa ni lipi? Hiyo inaamua sana uwezo na namna utakavyoikimbia zinaa.
Mstari uliokua unanisaidia sana enzi hizo ni Mithali 6:32.
Kwaleo natishia hapa.