Haujaumbwa kuvumilia tamaa za mwili bali hayo ni matokeo ya kuchelewa kuolewa,kutokuwa na mume na kuishi katika ulimwengu wa vishawishi.
Umri wa kuolewa ni kati ya 16 hadi 26. Chochote chini ya hapo ni ubatilifu juu ya hapo ni ubabaifu. Ukiolewa chini ya huo umri si sawa, ukiolewa juu ya huo umri ni kukosa umakini na maisha yako kama mtoto wa kike.
Thamani ya mwanamke ipo ndani ya nafsi au tabia zake. Mwili ni kama kuta za kulinda hayo yote. Ukilinda nafsi na tabia utalinda mwili pia.
Ukisema kuwa unajizuia it means unatamani kufanya. Na kama natamani je akili na fikra zako muda mwingi zipo kwenye nini? Akiwazacho mtu ndicho hugeuka kuwa sehemu kubwa ya matendo yake.
Nijibu maswali yafuatayo nikuonyeshe njia:
1. Una umri gani?
2. Una kiwango gani cha elimu?
3. Wewe ni mtoto wa ngapi kwenu wanawake ni wa ngapi na wanaume ni wangapi, wangapi wameoa na kuolewa?
4. Unaishi wapi na nani?
5. Unakipato?
6. Unafuata imani gani?
7. Wewe ni mwenyeji wa mkoa gani?
8. Upo katika mahusiano kama ndio yamedumu kwa muda gani?
9. Mahusiano yako ya muda mrefu yalikuwa kwa muda gani yaani ulikuwa na mtu kwa muda gani?
10. Unapenda kuwa na familia?