Wizara: Sababu serikali kuanzisha tahasusi za dini hizi hapa

Ukiwasikiliza wanaoitetea hiyo kitu wanasema serikali inaandaa fursa kwa watakaosoma hiyo michepuo wakaanzishe makanisa na misikiti yao kwa maana ya kujiajiri
Wanavyo vyuo vyao. Wawapeleke huko.
Mbona mapadre wanasoma kwenye vyuo vyao, vya Seminari.
 
Kumjua Mungu ndicho chanzo Cha Maarifa na HEKIMA na ufahamu.

Sayansi ifundishwe, BIBLIA pia ifundishwe.

Kumjua Mungu na dini ni vitu viwili tofauti. Mashuleni kuna Bible Studies na Islamic Studies, masomo haya yali/natosha kumpa mwanga mwanafunzi kuhusu imani yake. Haya mnayoleta ninyi ni dini. Kitu ambacho ni upumbavu tu.
 
Dunia nzima (wakiwemo waliotuletea hizi dini) wanawekeza kwenye STEM (Science, Technology, Engineering and Math); sisi ndiyo kwanza tunawekeza kwenye dini za watu.

Na kwa nini tumekwepa kufundishana African Religions? Au kwa vile tuliaminishwa ni Upagani/Ukafiri? 😳
 
Quran ni moja tu hakuna ya Zanzibar wala ya Tanganyika .. ya mshia wala Msuni wote tunatumia kitabu kimoja kisicho na agano jipya wala la kale .. pia katika dini ya kiislam kuna mitaala mbalimbali ... Kama fiqhi , tawheed na kadhalika watoto wetu hawafundishwi tu kusoma na kukariri bali pia kujua utaratibu mzima wa dini ya kiislam kuanzia finance mpaka jinsi ya kuingia na kutoka chooni ..
 
Kama wanakubaliana kwa nini kuna madhehebu ya kiiskamu ya sunni, shia, kadiani, isnalia, ahmadiya, bohra , ansar sunna nk?

Eti watakubaliana una hakika watakubaliana? Mbona suala la kufunga na kufungua ranadhani tunaona wanatofautiana tena hapa hapa Tanganyika?

Biblia ya kikatoliki ina vitabu 72 wakati ile ya amaa wengine ina vitabu 64, ifuatwe ipi ,

Mtihani atatunga nani anayekubalika.

Usiunge mkono hoja kishabiki.
 
Ni wakati sahihi suala la dini kufundishwa shuleni na vyuoni, kunaweza kuwepo hoja nyingi nzuri ila mimi naziona kuu 2
1. Kuna ombwe kubwa la uelewa wa asili ya imani nyingi zilizopo Tanzania.
Hapa tumejikuta waumini na viongozi wa madhehebu mengi wote hatuna hata ule uelewa wa msingi( basics) ya ile imani yetu. Kinachofanyika ni utashi na uelewa binafsi vinavyojengwa katika ushawishi unaotumika kwa sasa kwa baadhi ya madhehebu.
Zikifundishwa shuleni na vyuoni naamini itasaidia kupunguza hii hali
2. Dini zimekuwa tasisi kubwa na zinawafuasi wengi. Tasisi zina muundo wake uongozi na utendaji pia.
Serikali kama mlezi/ msimamizi wa uhuru wa kuabudu kuna wajibu wakuepusha hatari zote zinazoweza kutokea kwa raia wake katika kutekeleza ibada zao vizuri. Hili linawezekana kwa kutoa elimu katika tasisi na kuwapima viongozi/waumini wao juu ya kile wanachokiamini ili kisije kuleta madhara kwa wengine na taifa kwa ujumla.
 
Allah akuongoze
 
Quran ni moja tu dunia nzima, ingawa madhehebu tofauti
 
Hakuna Qur'an ya Zanzibar wala Tanganyika, Qur'an haijawahi kubadilika tokea iteremshwe. Na hivi sasa ina miaka 1400.
 
Kwani hayo masomo ya dini si yameanza kufundishwa mda mrefu tu hata mitihani ya Taifa tumefanyia pia

Kilichofanyika sasa hivi ni kuyafanya yawe na tahasusi rasmi ambapo sio kitu kibaya....Dini zikifundishwa mashuleni tena ikiwa katika tahasusi hivi itasaidia kupunguza Uchafu ambao unafanywa na wanafunzi nowadays kwa kukosa maadili mashuleni....
 
Quran ni moja tu dunia nzima, ingawa madhehebu tofauti
Usipotoshe watu mkuu. Korani ya Bakwata na Ahmadiya hazifanani. Sasa hao wanafunzi watasomaje?
 
Usipotoshe watu mkuu. Korani ya Bakwata na Ahmadiya hazifanani. Sasa hao wanafunzi watasomaje?
QUran ni moja tu narudia tena ,haijawahi kutokea quran nyingine ingawa madhehebu tofauti ila hakujawahi kutokea quran tofauti, quran ya ahmadiya na bakwata ni hiyo hiyo moja
Chini hapo umetolewa ufafanuzi mzuri soma ujifunze, acha kupotosha


The Holy Quran is the only scripture that has stood the test of time; never has it successfully been interpolated. In Surah al-Hijr, Allah takes on the responsibility of safeguarding the Holy Quran Himself – both in letter and spirit.

Logically, how can a Muslim claim another has successfully misled others by altering the Holy Quran? The Ahmadiyya Muslim Community has been accused of committing tahrif (alteration) in the Holy Quran and its meaning. Should this claim be true, what can be said about the promise and responsibility of God?

Anyone can pick up a copy of the Holy Quran published by the Ahmadiyya Community and verify that not a single word or punctuation mark has ever been altered. However, this allegation – stemming from disagreement on certain translation matters – is made to appear as if the Ahmadiyya Community has altered the text, God forbid.
 
Bible knowledge na Islamic knowledge zimekuwa zikifundishwa Ordinary level hapa Tanzania Kwa miongo kadhaa ila hazikuwa zinafundishwa Advanced level, Sasa serkali imeamua iendelee kufundishwa advanced level Sasa sioni tatizo hapo. Kama tatizo ni udini, huko O level zinafundishwa Kwa miaka Sasa katika shule zote za uma kumutokea tatizo la udini?
Mtu anaepinga masomo ya dini kufundishwa advance level ikiwa o level yanafundishwa nashindwa kumuelewa kabisa
 
Kuna mijitu imekaa kupinga kila kitu, hii nchi ina usalama wa taifa, wazee wa nchi, na vyombo mbali mbali kwa ajili ya ulinzi na maendeleo ya nchi, kuna watu akili zao kisa samia muislamu basi kila kitu anachofanya ni kwa ajili ya uislamu, ni ujinga mtupu na elimu duni ndio inazalisha vijana wavivu wa kufikiri kazi kulaumu na malalamiko
 
Dini bhana…..ni hujuma sometimes
Serikali ya CCM inapenda kuchanganya elimu na dini ili kuwafanya wasomi wawe waoga kuhoji mambo ya msingi na kuwaachia mafisadi waendelee kuguguna rasilimali za umma. Hii ni mbaya sana.
 
Je, wahindu na wapagani watafundishwa kwa kutumia korani au biblia? Maana inaonekana ulihusika kutunga huu mtaala wa kipuuzi usiokuwa na mwelekeo kwa taifa.
 
Dini ni ulevi kama ulevi mwingine Tu, hakikisha Imani yako haikupeleki mbali kiasi cha Kuacha kutumia akili zako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…