Mungu ni Hana limits.
1. Ijumaa, JUMAMOSI na Jumapili kwenye nyumba za Ibada ataabudiwa.
2. Maofisini lazima aingie Mungu Ili watu waache kupokea RUSHWA.
3. Mashuleni lazima Mungu aingie Ili kusaidia watoto wetu wawe na HOFU ya Mungu, wajue dhambi ni nini, wakatae USHOGA, wizi, kutotii nknk wawe wema.
4. Mungu lazima aingie Bungeni Ili wabunge wasimamie HAKI na kuhakikisha wananchi wanapata HAKI Yao, wanapata mgao katika cake ya Taifa, nknk
5. Mungu aingie IKULU, Ili Mahali hapo pasigeuzwe pango la WANYANG'ANYI Bali pawe Mahali Patakatifu, maslah ya nchi yatangulizwe mbele.
6. Mungu aingie Kwa wavuvi, Baharini, ziwani na katika mito, Samaki waongezeke, wajue UVUVI haramu ni DHAMBI, waache uchawi Ili Ajali majini zipungue.
7. Mungu aingie migodini, wajue Mungu ndiye mwenye madini yote, waache kuua albino Kwa Imani mbovu, wajue Mungu yupo na wamtegemee, wasikwepe Kodi, Amani itawale, mashimo Yao yateme.
8. Mungu aingie mashambani, Ili mvua zije Kwa wakati, mazao yapatikane, chakula kuwepo Cha kutosha nchini, majanga yaondoke.
Mungu Si jini wa kufungiwa kwenye chupa pekee, Mungu Hana mipaka, tumkaribishe katika sekta zote.
Naunga mkono Divinity,mafundisho mashuleni ya Imani juu ya Mungu Mmoja yafundishwe mashuleni.
Amen
Umeelewa?