kitu ambacho sijaelewa ni hiki, wameandika barua ili wahesabu wanafunzi wa kiislam ni wangapi, wale wakristo wamehesabiwa?
1. kama wakiruhusu dini kufundishwa, kila watu wafundishwe kwa madhehebu yao. mfano, mimi ni mkristo, Mlokole, nisingependa kabisa mtoto wangu afundishwe dini ya padre, aende mchungaji wa kilokole akafundishe wanafunzi walokole.
2. kwenye hizo shule, wagawe madarasa, na wanafunzi wagawanywe, walokole watakuwa na darasa lao, walutherani darasa lao, anglican wanaoruhusu ndoa za mashoga wawe na la kwao, catholics wawe na darasa lao, AIC wawe na darasa lao na kina mwamposa wawe na madarasa yao.
3. Hii ni hatari sana, imeanza kuwatenga watoto kidini tangu wakiwa wadogo kabisa shuleni, wataendelea hivyo hadi watakapokuwa wazee. Samia atakuwa amekuwa rais wa kwanza kuleta utengano kwa minajili ya dini nchini hapa.
4. wale wanafunzi wanaosali pamoja, ndio watakuwa marafiki, ndio watasaidiana makazini wakimaliza shule, na wataonana ndugu kwa minajili ya dhehebu.
SAMIA ANAFIKIRI HII NCHI ANAIPELEKA WAPI? KWASABABU WAISLAM WAMETAKA BASI HATA TUKITENGA WATOTO NI POA TU? AU ANAFIKIRI HAPA NI ZANZIBAR? Huku bara tuna dini mbalimbali, na tuna madhehebu mbalimbali, na tumekuwa tukisoma pamoja bila kunyoosheana vidole kwamba huyu ni mpentecoste, huyu mkatoliki, huyu muislam, huyu mlutheran, huyu mni nini na nin, hatuna hiyo.