Wizara ya Afya: Tutatoa taarifa kama kuna ongezeko la Magonjwa ya Mfumo wa Upumuaji

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
1684072316746.png

Kuhusu tetesi za uwepo wa Covid 19; Nawaomba wananchi muondoe hofu. Tunachakata taarifa tulizokusanya kutoka Hospitali/Vituo mbalimbali ndani ya wiki hii tutatoa taarifa kama kuna ongezeko la magonjwa ya mfumo wa hewa au la?

Kwa taarifa za wagonjwa waliopimwa virusi vya UVIKO-19 wiki ya tarehe 6 - 12 Mei 2023 Watu 6 kati ya 288 walithibitishwa kuwa na corona. Hii ikiwa ni pungufu ikilinganishwa na wiki ya tarehe 29/04/23 hadi 05/05/23. Hakuna kifo chochote kilicho thibitishwa kusababishwa na UVIKO-19.

Wizara ya Afya inaendelea kufuatilia kwa karibu kwenye hospitali mbalimbali na tutawapa taarifa kamili.
Nawaomba wananchi muendelee kuzingatia kanuni za Afya na Usafi.

#MtuNiAfya #Afyayanguwajibu
wangu
 
Ni kwamba 'Kitu cha Kichina' kimerejea kwa Kasi ya Kinyemela na kwamba hata aliopita nao Israeli ghafla Mikocheni Juzi na Mnazi Mmoja leo tunazugwa tu ila ni 'Kitu cha Kichina' kilichorejea.

Na taarifa nilizozipata ni kwamba Wahusika wa Wizara husika na Mamlaka zingine zinakaa Kikao dharula ili kuwatangazia Wabongo juu ya 'Kitu cha Kichina' kusudi kila Mtu aanze kuchukua Tahadhari.

Na Kinachowaumiza Kichwa zaidi ni kuwa je, Wakitangaza uwepo wake rasmi Watalii hawatapungua? Je, Filamu ya Royo Tua itakuwa na la maana tena?

Ngoja sasa na Mimi GENTAMYCINE nianze Kupangua Nguo zangu moja baada ya nyingine nitafute zilikojificha Barakoa zangu Tukuka ili nami nisiwe THE NEXT baada ya Mmwela na Mgogo kisha nchi ikatikisika na JamiiForums nako Kukatikisika.
Jamii imeanza kustuka aisee.

Kuna unreported cases zinajiri kwa kasi kubwa huku mitaani.

Baba yake rafiki yangu tunamuaga leo kafariki kwa tatizo la upumuaji
 
Yaani Kwa serikali ya Mama hapo mmesingizia Ile juzi huko Kagera homa ya kutoka damu Kila mahala iliyotokea mlisikia ilivyotangazwa?mnyonge mnyongeni Haki yake apewe Kwa hili Muacheni mama wa Watu......namtetea ktkt hili.
 
Ni kwamba 'Kitu cha Kichina' kimerejea kwa Kasi ya Kinyemela na kwamba hata aliopita nao Israeli ghafla Mikocheni Juzi na Mnazi Mmoja leo tunazugwa tu ila ni 'Kitu cha Kichina' kilichorejea.

Na taarifa nilizozipata ni kwamba Wahusika wa Wizara husika na Mamlaka zingine zinakaa Kikao dharula ili kuwatangazia Wabongo juu ya 'Kitu cha Kichina' kusudi kila Mtu aanze kuchukua Tahadhari.

Na Kinachowaumiza Kichwa zaidi ni kuwa je, Wakitangaza uwepo wake rasmi Watalii hawatapungua? Je, Filamu ya Royo Tua itakuwa na la maana tena?

Ngoja sasa na Mimi GENTAMYCINE nianze Kupangua Nguo zangu moja baada ya nyingine nitafute zilikojificha Barakoa zangu Tukuka ili nami nisiwe THE NEXT baada ya Mmwela na Mgogo kisha nchi ikatikisika na JamiiForums nako Kukatikisika.
Siipingi mkuu kuna jirani yetu mfanyakazi wa B.O.T licha ya kuwa na shida zingine ila mafua ndio sababu
 
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amewatoa hofu wananchi baada ya kuanza kuenea tetesi za uwepo wa ugonjwa wa COVID-19. Waziri Ummy ameyasema hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter.

"Kuhusu tetesi za uwepo wa #COVID19; Nawaomba wananchi muondoe hofu. Tunachakata taarifa tulizokusanywa kutoka Hospitali/Vituo mbalimbali ndani ya wiki hii...tutatoa taarifa kama kuna ongezeko la magonjwa ya mfumo wa hewa au la??

Kwa taarifa za wagonjwa waliopimwa virusi vya UVIKO-19 wiki tarehe 6 - 12 Mei 2023 Watu 6 kati ya 288 walithibitishwa kuwa na corona. Hii ikiwa ni pungufu ikilinganishwa na wiki ya tarehe 29/04/23 hadi 05/05/23. Hakuna kifo chochote kilicho thibitishwa kusababishwa na UVIKO-19
Wizara ya afya inaendelea kufuatilia kwa karibu kwenye hospitali mbalimbali na tutawapa taarifa kamili.

Nawaomba wananchi muendelee kuzingatia kanuni za Afya na Usafi.#MtuNiAfya
"
 
Back
Top Bottom