BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826

Kuhusu tetesi za uwepo wa Covid 19; Nawaomba wananchi muondoe hofu. Tunachakata taarifa tulizokusanya kutoka Hospitali/Vituo mbalimbali ndani ya wiki hii tutatoa taarifa kama kuna ongezeko la magonjwa ya mfumo wa hewa au la?

Kwa taarifa za wagonjwa waliopimwa virusi vya UVIKO-19 wiki ya tarehe 6 - 12 Mei 2023 Watu 6 kati ya 288 walithibitishwa kuwa na corona. Hii ikiwa ni pungufu ikilinganishwa na wiki ya tarehe 29/04/23 hadi 05/05/23. Hakuna kifo chochote kilicho thibitishwa kusababishwa na UVIKO-19.

Wizara ya Afya inaendelea kufuatilia kwa karibu kwenye hospitali mbalimbali na tutawapa taarifa kamili.
Nawaomba wananchi muendelee kuzingatia kanuni za Afya na Usafi.

#MtuNiAfya #Afyayanguwajibu
wangu
 
Jamii imeanza kustuka aisee.

Kuna unreported cases zinajiri kwa kasi kubwa huku mitaani.

Baba yake rafiki yangu tunamuaga leo kafariki kwa tatizo la upumuaji
 
Yaani Kwa serikali ya Mama hapo mmesingizia Ile juzi huko Kagera homa ya kutoka damu Kila mahala iliyotokea mlisikia ilivyotangazwa?mnyonge mnyongeni Haki yake apewe Kwa hili Muacheni mama wa Watu......namtetea ktkt hili.
 
Siipingi mkuu kuna jirani yetu mfanyakazi wa B.O.T licha ya kuwa na shida zingine ila mafua ndio sababu
 
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amewatoa hofu wananchi baada ya kuanza kuenea tetesi za uwepo wa ugonjwa wa COVID-19. Waziri Ummy ameyasema hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter.

"Kuhusu tetesi za uwepo wa #COVID19; Nawaomba wananchi muondoe hofu. Tunachakata taarifa tulizokusanywa kutoka Hospitali/Vituo mbalimbali ndani ya wiki hii...tutatoa taarifa kama kuna ongezeko la magonjwa ya mfumo wa hewa au la??

Kwa taarifa za wagonjwa waliopimwa virusi vya UVIKO-19 wiki tarehe 6 - 12 Mei 2023 Watu 6 kati ya 288 walithibitishwa kuwa na corona. Hii ikiwa ni pungufu ikilinganishwa na wiki ya tarehe 29/04/23 hadi 05/05/23. Hakuna kifo chochote kilicho thibitishwa kusababishwa na UVIKO-19
Wizara ya afya inaendelea kufuatilia kwa karibu kwenye hospitali mbalimbali na tutawapa taarifa kamili.

Nawaomba wananchi muendelee kuzingatia kanuni za Afya na Usafi.#MtuNiAfya
"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…