Lord Denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 23,491
- 57,973
Anguko Kuu la CCM na Serikali yake halitotokana na jambo lingine lolote lile zaidi ya kukosa akili.
Kukosa kwao akili ndo kumesababisha wawapuuze Wananchi na madai yao ya ukweli kisha kukimbilia kuwateka, kuwaua na kuwapoteza hali iliyopelekea hasira za Wananchi kupanda na kufikia kikomo na hatimaye kufanyika maandamano ya Oktoba 29.
Kukosa akili kwa CCM ndiko kulikosababisha Waendekeze ufisadi badala ya kuelekeza fedha nyingi katika masuala yanayoondoa changamoto za Wananchi mfano maji safi na salama, miundombinu bora, umeme, huduma bora za hospitali pamoja na ajira kwa vijana. Matokeo yake Wananchi wamewachoka na kuzidisha hasira dhidi yao na sasa wako tayari kufanya chochote ili kuwatoa madarakani.
Wiki hii Kamishna ya Kamisheni ya Umoja wa Mataifa aliibua tuhuma nzito kuhusu Mauaji Makubwa yaliyofanyika nchini Tanzania huku Serikali ikihusika kuficha ukweli na kuzuia miili ya watu kuzikwa na ndugu zao.
Tukio la Wizara ya Afya kukanusha video halisi na ya kweli iliyochukuliwa na Mtumishi mzalendo kweli ikionesha miili ya watu hasa vijana zaidi ya 200 katika mochwari moja ya hospitali ya Mwananyamala linazidi kuthibitisha kuwa anguko kuu la Serikali ya Samia na CCM ambalo liko obvious si kwa sababu nyingine yeyote ile ila ni kukosa akili.
Katika dunia ya sasa hakuna video ya kweli ambayo itarushwa mitandaoni alafu unaweza kanusha sio kweli.
Teknolojia kwenye dunia ya sasa imekuwa sana kiasi kwamba kuna mifumo ya ku verify uhalisia wa video, ilichukuliwa kwenye kifaa kipi? na kurushwa kutoka kwenye kifaa kipi? Na lini? Hivyo kwa kusema Video fulani ni feki ni kama unajitia mwenyewe hatiani na kuuthibitishia ulimwengu kuwa kumbe ni kweli unaficha ukweli kuhusu mauaji uliyofanya.
Tamko hili la Wizara ya Afya bila shaka limeuthibitishia ulimwengu kuwa, Serikali ya Tanzania ilifanya mauaji makubwa kipindi cha Uchaguzi na imefanya kazi kubwa sana kuficha huo ukweli hivyo kustahili kuwajibishwa.
Tamko la Wizara ya Afya linathibitisha kuwa ni kweli Serikali ya Tanzania haipaswi kujichunguza kwa mauaji ya kutisha iliyofanya na zaidi inapaswa kuchunguzwa na kuchukuliwa hatua kali na Jumuiya ya Kimataifa ikiwemo Viongozi wake hasa Samia na Wakuu wake wa vyombo vya dola kufikishwa Mahakama ya ICC.
Anguko la Samia na Serikali yake lipo obvious. Alishauriwa sana akashupaza shingo na kwa alipofika hakuna anayeweza kumuokoa. Bahati mbaya kwa namna mnavyojitoa uhafamu kukanusha masuala ya kweli ndivyo mnavyozidi kumuweka kwenye sehemu mbaya.