Interest
JF-Expert Member
- Apr 11, 2015
- 3,434
- 7,072
Nchi inaenda vizuri sana. Mungu ni mwema. Ukizunguka huko mikoani (nje ya Majiji) utaona jinsi ambavyo halmashauri na maeneo yote ya kiutendaji yanavyofanya kazi za miradi kwa bidii na bila malalamiko.
Kwa wasiofahamu, Serikali imemwaga fedha nyingi kwenye halmshauri zote nchi nzima. Huko ndipo walipo wananchi wengi wanaofikiwa na huduma za kijamii kama za afya, elimu, maji, umeme, miundombinu na kadhalika. Tusishtuke tukiona picha za mashule, mahospitali, mabomba ya maji na mengine.
Kipekee naipongeza Wizara ya Fedha na watendaji wake wote kwa ujumla. Ubunifu, uchapakazi na weledi wao umeisaidia nchi kunufaika na miradi ya kimaendeleo inayoendelea kufanyiwa kazi huko 'site'. Ule msisitizo wa 50% pesa ya bajeti zinazopelekwa kwenye wizara zote zitumike kwenye maendeleo imesaidia mno. Na usimamizi umekuwa mkali kuhakikisha pesa haipotei na matumizi yake yanaonekana.
Kama mtu ni mfuatiliaji wa mambo, bila shaka atakubaliana nami kuwa hivi sasa pesa imemwagwa kweli kweli. Sijui ndio ile inaitwa injection au induction. Nina uhakika matokeo yake yataonekana tu kwani hata vyuma vilivyokaza vimeanza kulegea.
Nimpongeze pia Dkt. Mwigulu Nchemba (almaarufu Zakayo), kiongozi aliyeamua rasmi kutumia taaluma yake kuisaidia nchi na kupunguza siasa za majukwaani. Ukifuatilia mwenendo wake unamuona kabisa ni mtu anayejitahidi kubadilika sana. Nilipenda ukaribu na ushirikiano wake na Odo Ummy Mwalimu alipokuwa TAMISEMI. Hata ule ushuhuda wa Rais Samia kuwa alipigiwa simu usiku kuhusu masuala ya kifedha sio wa kuuchukulia poa. Ilionesha dhamira yake ya dhati kwa maslahi ya nchi.
Mawaziri, watendaji na viongozi wengine nao wanafanya kazi nzuri katika maeneo yao. Kuanzia kwa kiongozi ninayemkubali Prof. Mbarawa, Odo Ummy, Mchengerwa, Bashe, Mulamula, Ndumbaro, Nape (promising) n.k.
Jambo moja tu linalotakiwa kuwekwa vizuri ni suala la demokrasia. Tena iwe demokrasia ya kweli. Vyama vya upinzani na viongozi wao wapewe nafasi ya kuichalenji serikali bila hofu ya kukamatwa au kushitakiwa kwa makosa ya kisiasa. Hilo tu!
Tuiombee nchi yetu. Tuwaombee viongozi wetu.