Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hahahahaha.......sema ulikuwa umekusudia kudanganya.Sorry ni Gridi ya Taifa. Mfupa hauna ulimi!
Katika masnitch wakubwa wa Samia huyu jamaa ni konkiNchi inaenda vizuri sana. Mungu ni mwema. Ukizunguka huko mikoani (nje ya Majiji) utaona jinsi ambavyo halmashauri na maeneo yote ya kiutendaji yanavyofanya kazi za miradi kwa bidii na bila malalamiko.
Kwa wasiofahamu, Serikali imemwaga fedha nyingi kwenye halmshauri zote nchi nzima. Huko ndipo walipo wananchi wengi wanaofikiwa na huduma za kijamii kama za afya, elimu, maji, umeme, miundombinu na kadhalika. Tusishtuke tukiona picha za mashule, mahospitali, mabomba ya maji na mengine.
Kipekee naipongeza Wizara ya Fedha na watendaji wake wote kwa ujumla. Ubunifu, uchapakazi na weledi wao umeisaidia nchi kunufaika na miradi ya kimaendeleo inayoendelea kufanyiwa kazi huko 'site'. Ule msisitizo wa 50% pesa ya bajeti zinazopelekwa kwenye wizara zote zitumike kwenye maendeleo imesaidia mno. Na usimamizi umekuwa mkali kuhakikisha pesa haipotei na matumizi yake yanaonekana.
Kama mtu ni mfuatiliaji wa mambo, bila shaka atakubaliana nami kuwa hivi sasa pesa imemwagwa kweli kweli. Sijui ndio ile inaitwa injection au induction. Nina uhakika matokeo yake yataonekana tu kwani hata vyuma vilivyokaza vimeanza kulegea.
Nimpongeze pia Dkt. Mwigulu Nchemba (almaarufu Zakayo), kiongozi aliyeamua rasmi kutumia taaluma yake kuisaidia nchi na kupunguza siasa za majukwaani. Ukifuatilia mwenendo wake unamuona kabisa ni mtu anayejitahidi kubadilika sana. Nilipenda ukaribu na ushirikiano wake na Odo Ummy Mwalimu alipokuwa TAMISEMI. Hata ule ushuhuda wa Rais Samia kuwa alipigiwa simu usiku kuhusu masuala ya kifedha sio wa kuuchukulia poa. Ilionesha dhamira yake ya dhati kwa maslahi ya nchi.
Mawaziri, watendaji na viongozi wengine nao wanafanya kazi nzuri katika maeneo yao. Kuanzia kwa kiongozi ninayemkubali Prof. Mbarawa, Odo Ummy, Mchengerwa, Bashe, Mulamula, Ndumbaro, Nape (promising) n.k.
Jambo moja tu linalotakiwa kuwekwa vizuri ni suala la demokrasia. Tena iwe demokrasia ya kweli. Vyama vya upinzani na viongozi wao wapewe nafasi ya kuichalenji serikali bila hofu ya kukamatwa au kushitakiwa kwa makosa ya kisiasa. Hilo tu!
Tuiombee nchi yetu. Tuwaombee viongozi wetu.
Hahahahaha.......sema ulikuwa umekusudia kudanganya.
Si kweli, angekuwa snitch basi asingemsaidia kuperform. Bahati mbaya sana Watanzania tuna tabia ya kujiaminisha mambo.Katika masnitch wakubwa wa Samia huyu jamaa ni konki
Aendelee kumfuga na kumrutubisha hadi siku ambayo itakuwa too late
Tuanze kwenye TOZO la kijizi.Si kweli, angekuwa snitch basi asingemsaidia kuperform. Bahati mbaya sana Watanzania tuna tabia ya kujiaminisha mambo.
Kwa historia ya chama cha CCM ya kulitafuna Taifa hili kupitia ufisadi inaniingia akilini Samia kuhamasisha ufisadi kwenye Serikali yake.Kama enzi za ufisadi wa Escrow na Richmond viongozi wa CCM walipakia hela kwenye viroba na kwenye Sandarusi, kwa nini nishangae leo Samia kuhamasisha ufisadi katika serikali yake?Well said, lakini hapo anaposhauri ziliwe kwa staha sijapasikia au ni maoni na tafsiri yako binafsi? Wapo walioona kama ni onyo lililotolewa kwa lugha ya upole.
Kuhusu fedha kutafunwa na kupelekea miradi hiyo kukwama, tayari wizara imeshatoa agizo kwa wakaguzi wa ndani kukagua na kutoa ripoti ndani ya mwezi mmoja ili kujua pesa zimetumikaje, wapi miradi imekwama, nani hakuwajibika na kama zimeliwa nani amekula ili hatua zichukuliwe. Tusubiri maamuzi baada ya ripoti.
NB: Nimekuwekea video hapo chini ujiridhishe. Hakuna namna kiongozi wa taifa atahalalisha rushwa na ufisadi hadharani. Wewe inakuingia akilini?
Mambo za Multi ID hizoCM 1774858 mwenzako huyu hapa.
Tuanze kwenye TOZO la kijizi.
Unadhani raia wanafurahia huu wizi?
Endeleeni kukopa mkimuaminisha Hangaya kuwa no worries.
Kwanza ndio Kazi hasa kutoa fedha za miradi kwa wakati.
Walioko ofisini na wanaotekeleza miradi na watoa huduma ni mashahidi kwa namna ambavyo flow ya pesa inatoka kwa wakati..
Hongera SSH maana miaka mingine utekelezaji wa bajeti ulikuwa chini ya asilimia 70%.
Sawa mkuu. Inaonekana kwako hii ni imani. Ngumu mno kukuelewesha tofauti na unavyoamini. At least nimejaribu!Kwa historia ya chama cha CCM ya kulitafuna Taifa hili kupitia ufisadi inaniingia akilini Samia kuhamasisha ufisadi kwenye Serikali yake.Kama enzi za ufisadi wa Escrow na Richmond viongozi wa CCM walipakia hela kwenye viroba na kwenye Sandarusi, kwa nini nishangae leo Samia kuhamasisha ufisadi katika serikali yake?
Samia alikuwa anahamasisha ufisadi kwa sababu kwa maneno yake alikuwa anawaambia mawaziri kuwa siyo kweli kwamba hawapati kitu kwenye maeneo yao na aliwasisitiza kuwa tatizo wanakula hadi kuvimbiwa kitu ambacho kinakwamisha miradi.Ndipo akawashauri kuwa wajipimie badala ya kula kwa ulafi kitu ambacho kinakwamisha miradi ya maendeleo.
Nyie ndio mnaoajiriwa na kukomba mishahara minono bila kuwa na weledi halafu unataka uje JF tuwapeni maarifa ya jinsi ya kumshauri Hangaya na mkifanikiwa hamsemi mlitumia akili za nani Mpaka mkafanikiwa!! You have to acknowledge kuwa BULESI ndio aliwapa hilo suluhisho!! Uzalendo una mwisho watu hawali uzalendo!!! Tonny Blair mnamlipa lakini wazalendo mnataka wawafanyie kazi bure!!!Ukipewa maelezo unaita mapambio. Hoja yako nzuri inaharibiwa na mihemko. Una ushauri wowote? Andika hapa, huwezi kujua nani anasoma na huenda maoni/ushauri wako ukafanyiwa kazi.
Ni hatua zipi zinaweza kuchukuliwa na bei zikashuka?
Nyie ndio mnaoajiriwa na kukomba mishahara minono bila kuwa na weledi halafu unataka uje JF tuwapeni maarifa ya jinsi ya kumshauri Hangaya na mkifanikiwa hamsemi mlitumia akili za nani Mpaka mkafanikiwa!! You have to acknowledge kuwa BULESI ndio aliwapa hilo suluhisho!! Uzalendo una mwisho watu hawali uzalendo!!! Tonny Blair mnamlipa lakini wazalendo mnataka wawafanyie kazi bure!!!
Nimekumegea kidogo nenda kasome , hopefully utaelewa!!Hii inaashiria kuwa huna mawazo mbadala zaidi ya kuponda, kusiliba na kuongea vibaya. Jikague mkuu!
Hakika bongo nyoso kwelikweli.Pengine unaishi maeneo ya mjini au upo kwenye comfortable life so unaweza usielewe hizi unazoita tozo za kijizi zinavyosaidia huko site. Na hakuna nchi duniani isiyokopa, msijiaminishe na kuaminisha umma kuwa kukopa ni jambo baya, hatutafika.
La muhimu tupigie kelele uwajibikaji na ndicho kinachofanywa na wenye nia ya dhati serikalini kwa sasa, japo msafara wa mamba na kenge huwa hawakosekani.