Wizi, udokozi na ujambazi vimeibuka kwa kasi huku mitaani

Wizi, udokozi na ujambazi vimeibuka kwa kasi huku mitaani

Daraja lipi?hilo kama la mlalakuwa kitambo tu uhalifu umekuwa ukifanyika hapo

Ova
 
Wakati majambazi yaliogopa na wengine kuacha uuwaji au kuuwawa nilikuwa naenda mikoani tena usiku ila sasa hali inatisha
 
Mama sio Polisi, sasa kama yanafanyika ili kuonekana Mama hafanyi kazi ni upuuzi wa hali ya juu sana, Polisi fanyeni kazi yenu
 
SUKUMA GANG NA MATAGA ni adui wa Taifa.
Mama piga chini huyo Mjita, mkuu wa hilo jeshi.
Hao wanajaribu ni kama kum' blackmail' Mama kama vile ameshindwa kazi,lakini hawataweza......ujanja wa kitoto..kazi iendelee.
 
Hakuna anayewapenda majambazi, hakuna anayemsikitikia jambazi akiuawa. Lakini Polisi wakipewa mamlaka ya kumwua kila mtuhumiwa wa ujambazi, mjue kuna watu wema watapoteza maisha kwa kusingiziwa kuwa ni majambazi, au kwa kuhisiwa ni majambazi wakati ni raia wema.

Kuna mwaka mmoja, mjini Mwanza, vijana watatu wa kidato cha sita walipokuwa likizo, wakati wanatoka disco, waliuawa kwa kuhisiwa ni majambazi wakati wakipita eneo ambalo kulikuwa kumetokea ujambazi. Miongoni mwa aliyeuawa alikuwa ni mtoto wa kiongozi mmpka ngazi ya mkoa (RC au RPC, sikumbuki vizuri).
 
Jana nikauliza...!

Hili wimbi la majambazi kuongezeka Kwa Kasi kabla hata ya siku 80 za Mwendazake kufikia, Je ndio hao wamekuwa wakifurahia kuondoka kwake duniani kwamba warudi Kwenye upolaji na wizi Kwa kutumia nguvu na siraha mchana kweupe??

Badala yake Uzi wangu ukafutwa Kwa kuhisiwa Mimi ni sukuma gang

Hili likiachwa itampa credit Mwendazake, binafis nitasema, enzi za Mwendazake, hatukuwa tunayaona haya

Vizuri Wakuu wa vyombo vya usalama ni walewale, labda iwe Kweli mama anawashauri jeshi lake kutokutumia siraha, lakini aelewe hivi, kipindi cha nyuma ujambazi ulipokuwa umekolea, Vituo vya police kila wakati zilikuwa zikiporwa siraha, na ndiko tutafikia

Mtu aliyechoka na maisha Kwa kuwafyatulia wengine risasi, achapwe Moto vilevile
 
SUKUMA GANG NA MATAGA ni adui wa Taifa.
Mama piga chini huyo Mjita, mkuu wa hilo jeshi.
Siro siyo mjita, ni Mwikizu. Sawa kama Warioba. Lakini Siro hawezi kufanya hujuma kwa Mama.
 
Hali ikiendelea hivi dar es salaam itakuwa kwenye kundi la miji isiyo salama. Najiuliza hawa majambazi waliogopa nini miaka mitano iliyopita? Je kwa nini serikali isitumie njia iliyotumika miaka mitano iliyopita? Pia hahihitaji press conference ndipo wende kutafta majambazi. Je hauwezi kwenda kimya kimya tu ukayapata bila kutaarifu majambazi? Simba mwenda kimya ndo mla nyama. Kwa kweli usalama wa dar es salaam unaanza kutia shaka sana. je kuna muwekezaji anaweza kuwekeza kwenye sehemu ambayo haina usalama? Iweje wote tuambiwe kwamba tuweke hela kwenye simu(M-Pesa, tigopsa n.k.)? Je tutaishi kwa masharti sababu tu ujambazi haujathibitiwa na wakati miaka mitano iliyopita tulienda benki na kuchukua pesa ndefu bila woga? Mimi kama raia naona kuna shida mahali fulani. Sisi kama walipa kodi usalama ni kipaumbele namba moja. Nyumba zetu zimajaa grill kwenye madirisha na milango kama stoo za kutunzia bidhaa, Perimeter walls zimejaa nyaya za umeme kama no go zone za kutunzia mabomu ya kivita. Ukiona haya yote ujue usalama hakuna.
 
Mama haiwezekani Magufuli afe, halafu baada ya mwezi ujambazi uuamke kwa Kasi ya kimbunga. Sema vizuri na Vyombo vyako vya Usalama.

Tulizoea Majambazi hawakamatwi, bali utasikia walijibizana risasi na Askari Polisi na mwisho wakajeruhiwa, na bahati mbaya walipofikishwa hospital walifariki. Eti leo hii wanakamatwa.Mama unahujumiwa.

Mama usije ukawa umewakataza wasijibizane na majambazi kwa risasi bali wawakamate na kuwafikisha mahakamani, huku mtaani tutakwisha. Kaza roho waache wapambane nao, ukisikia majambazi wameuawa, ziba masikio na kama hakuna aliyefikishwa mahakamani na nchi ipo shwari Sema hewala.

Juzi kuna jamaa amekutana na Askari Polisi wapo kiraia wakiwa kwenye doria,kwa upole kabisa wakamwambia usikatize tena hapa darajani Ukiwa peke yako, iwe mchana au usiku, Ujambazi umerudi kwa Kasi. Sasa unajiuliza Magufuli ameondoka na Vyombo vyake vya Usalama au?.Mama Kaa upya na vyombo vyako hasa Mapolisi. Fanya kama alivyowahi kufanya Magufuli aliwaita maafisa wote wa Polisi na kuna wakati aliita wadogo wakiwemo Traffic ,. Usipuuze hata kidogo,na hakikisha hawakosi walichokuwa wakikipata kwa Magufuli, na ikiwezekana waongezee.
sukuma gang wapinga mama
 
Una maana jeshi la Polisi linamhujumu Mama?
 
Kosa lingine Mama alilofanya nikuendelea kukumbatia viongozi wa Magu. Alitakiwa aanze hivi sasa kuwaondoa mmoja mmoja.Ki ukweli wengi wao hawamuamini hata kidogo
 
Daraja la salender
Uhalifu umekuwepo hapo muda tu tena wezi wa hapo wanatokea Moscow
Kuna mke wa kigogo fulani aliibiwa wakati fulani
Hapo,ndipo wakaanza kukaa askari wa Doris ila wakiondoka wanarudi

Ova
 
Back
Top Bottom