Wizi wa catalytic converter kwenye magari 'Masega'

Wizi wa catalytic converter kwenye magari 'Masega'

Ni kweli kabisa hii kitu ni dili mbaya
Nasikia zinatumika kutengenezea madawa ya kulevya, hasa baada ya udhibiti wa uingizaji wa madawa hayo, wanatengeneza kwa namna gani sijui? Yanauzwa kwa zaidi ya Sh. 450,000/=. Niligundua hili baada ya kuona gari la jamaa yangu linatoa sauti mbaya, wale mafundi wakasema hivyo.

TAHADHARI:
Usipeleke gari lako katika magereji ya vichochoroni, au linapotengenezwa usikae mbali, pia paki eneo lenye ulinzi wa kuaminika. Kuchomoa hiyo kitu ni dakika tano tu.
 
Nasikia zinatumika kutengenezea madawa ya kulevya, hasa baada ya udhibiti wa uingizaji wa madawa hayo, wanatengeneza kwa namna gani sijui? Yanauzwa kwa zaidi ya Sh. 450,000/=. Niligundua hili baada ya kuona gari la jamaa yangu linatoa sauti mbaya, wale mafundi wakasema hivyo.

TAHADHARI:
Usipeleke gari lako katika magereji ya vichochoroni, au linapotengenezwa usikae mbali, pia paki eneo lenye ulinzi wa kuaminika. Kuchomoa hiyo kitu ni dakika tano tu.
Dalili au mabadiliko gani huonesha kuwa tayari yamenyofolewa kwenyw gari?
 
Ndugu yangu kanunua gari la mkononi

Toyota Brevis ..baada ya siku chache
Likaanza kutoa taa ya engine na mlio tofauti..

Kuuliza uliza mafundi na wajuzi wengine
Ndo wanamwabia gari yako imeibiwa
'masega'..sijui kama Hilo jina ndo sahihi. Na kama Lina jina lingine la kitaalam..

Wanasema kwenye lile bomba la kutoa moshi kuna hayo masega ..sijui ni aina ya Madini yanakuja na Brevis zote. Na ni deal huku Tz kuna watu wana matumizi nayo mengine sijui kwenye kitu Gani ..sasa kuna wizi mkubwa mno

Watu wengi wakipeleka gari garage..
Wanaibiwa ..na wengine hawajui wameibiwa ...

Nina maswali kidogo...Kwa wenye uelewa

Hivyo vitu vinaitwaje?Kuna jina la kitaalam? Why Brevis??

Nasikia vikishaibiwa gari linaharibika
Haraka sana?Why? Hakuna namna ya Ku replace?

Kwanini gari zingine hili tatizo sio kubwa? Kuna technological solution?
 
Hio no Catalyst Converter ni unga unga mweusi unakua upo kwenye exhaust system ya gari hapo suluhisho ni kununua catalyst converter ya gari husika tafuta gari ya aina hio iliopata tatizo jingine ununie hio
Inauzwaje?
Kama zinaibiwa zote unaweza pata ambayo
Haijaibiwa huo unga??
 
Inauzwaje?
Kama zinaibiwa zote unaweza pata ambayo
Haijaibiwa huo unga??
Unaweza ukabahatisha sehemu wanazochinja magari kwa mfano tandale kule pia hao wanaoiba wanaenda kuuza unaweza ukabahatisha wapaouza spare za magari pia..ilitolewa kwa chini inakua imeungwa ungwa kuna uzi wa mdau humu umeonesha iliotolewa inavyokua
 
Kwa kizungu inaitwa catalyst inafanya kemikali zingine kureact nayo pasipo yenyewe kunadilika. Inatumika kubadilisha moshi wa sumu kutoka katika engine kuwa gesi ya carbon dioxide na maji.

Ikiondolewa hiyo mnakua mnatuongezea sumu tu kwenye hewa na kuharibu ozone, ndo maana dar joto 😁
 
Kwa kizungu inaitwa catalyst inafanya kemikali zingine kureact nayo pasipo yenyewe kunadilika. Inatumika kubadilisha moshi wa sumu kutoka katika engine kuwa gesi ya carbon dioxide na maji.

Ikiondolewa hiyo mnakua mnatuongezea sumu tu kwenye hewa na kuharibu ozone, ndo maana dar joto 😁

Naomba wataalam mtujibu maswali yot
Why za Brevis ndo zinaibiwa sana?

Magari mengine hayana??

Halafu ni kweli gari inaharibika ikishatolewa
Hiyo?Why?
 
Mtuambie na matumizi mbadala ya hayo mavitu kwakuwa yapo kwenye kila aina ya gari na kwa wale wamama/wadada wajivuni wanaomiliki magari bila kumiliki wababa/wanaume hapa mjini wanaweza kuwa wahanga wakubwa mno.

Ukiniibia mimi nitajua tu hata kama nitachelewa, ila wanaoendesha peku peku ndo watateseka.

Toeni elimu ya kukagua masega yao....sorry, masega ya hizo catalytic converter, kama imeguswa, watajuaje? Itawasaidia wote ikiwa ni pamoja na taifa kuondokana na uchafu wa hewa
 
1608055875785.png


MATUMIZI YA HUO UNGA

Hutumika kuufabya ule moshi unaotoka kwenye bomba uwe msafi kimazingira.

KWANINI HUU UNGA UNAIBWA HAPA BONGO

Huu unga umekuwa dili , wezi wengi (wakiwamo mafundi wenye tamaa) wanaendaga kuuza wanakojua kwa elf 80 hadi laki ya chap chap.

Zimbabwe na South africa kuna makampuni yananunua huo unga, hali hii imepelekea vijana kuchangamkia hili dili, vijana wanakufata ukiwa umepaki gari wakiwa na dola 150 mkononi ( 🇹🇿 347,000 ) wanakuomba wautoe huo unga wakupe pesa, wao wanaenda kuuzia makampuni hata kwa dola 200 (🇹🇿 460,000)

Kiufupi wanaonunua huu unga hapa bongo 🇹🇿 wanaendaga kuuza 🇿🇦 sauzi au 🇿🇼 zimbabwe kwa faida kubwa zaidi


HUO UNGA WANAOUNUNUA WANAUTUMIAJE

1.Huo unga husafishwa na mitambo na kuwa mpya (recycled) ili kwenda kuuzwa Marekani na nchi nyingi za ulaya ambazo hawaruhusu gari halirusiwi kutembea barabarani kama linatoa moshi mchafu, huu unga kazi yake ndio kusafisha moshi mchafu, kupata spare mpya ya kifaa chenye unga huu kwa nchi kama marekani unaweza kugharamika hata dola elf 2 (takribani milioni 4 na nusu),

2.Pia huo unga unaweza kuchakatwa na mitambo maalum ili kupata kiasi kidogo cha madini aina ya palladium ambayo yana thamani kuzidi dhahabu, japo zinapatikana gram zisizozidi hata 5 baada ya kuchakatwa na mtambo (grams 28 sawa na ounce 1 bei ni $ 2,500 sawa na 5,780,000 🇹🇿 ).

3. Hii sina uhakika nayo ila kwa spidi ya huu wizi hapa bongo basi itakuwa huu unga ukiibwa gari fulani unaenda kuuzwa kwa alieibiwa.


UFANYE NINI KUEPUKANA NA WIZI HUU

Linda sana gari yako ukienda gereji, ni wizi unaofanyika ndani ya dakika kadhaa tu, ukiona gari yako imechomelewa huko chini kwenye bomba la moshi basi washapita hapo,Pia unaponunua gari kagua vizuri.
 
Unaweza ukabahatisha sehemu wanazochinja magari kwa mfano tandale kule pia hao wanaoiba wanaenda kuuza unaweza ukabahatisha wapaouza spare za magari pia..ilitolewa kwa chini inakua imeungwa ungwa kuna uzi wa mdau humu umeonesha iliotolewa inavyokua
Hebu weka link plz
 
Huo unga mafundi wengi wakiuza kibongo bongo wanapata laki ya fasta, kwa nchi kama zimbabwe na south africa kuna makampuni unaweza kuwauzia huo unga kitu kinachopelekea watu wanakufata kabisa ukiwa umepaki gari, wana dola 200 mkononi ( laki nne na ushehe) wanakuomba wautoe huo unga kwenye, wao wanaenda kuuzia makampuni, Kiufupi wanaonunua huu unga hapa bongo kwa hizi laki wanazowapa mafundi wezi, wao wanaenda kuuza sauzi au zimbabwe kwa faida kubwa zaidi
Kazi yake kubwa ni nini au unalewesha
 
Sio tu kuwa sheria hakuna, bali NEMC ni vilaza wa mwisho, tuna majenereta makubwa viwandani na migodini, yanatembea 24/7 na yanazalisha NOx ya kutosha, Europe na America pengine hata ASIA wana limit ya kiwango cha uzalishaji wa NOx kwenda hewani, labda 500mg ila sisi, tunaruhusu tu kila taka, gari ya 1993 unainunua na unadunda nayo, NEMC wanaenda kuangalia maji ya viwandani wanapuuza hewa inayochafuliwa inayovutwa na kila MTz kuanzia namba 1 mpaka zero.

Ila ni kuwa tunao wasomi mpaka levo ya uprofesa na wanazurula sana duniani, kama analyser huko na ni bei sawa na per diem zao za siku 5 tu za kuzurula huko, nani anajali,kasome Kayumba, kaimbe wimbo wa ajira hakuna, 5yrs later kachague kijani, anza tena kulalalamikia huduma za kijamii, and the cirle repeated itself.

PROUD TO BE IGNORANT(TANZANIAN) FOREVER
Lakini Tanzania converter ya nini wakati hakuna sheria ya kulazimisha kutumia converter
 
Naomba wataalam mtujibu maswali yot
Why za Brevis ndo zinaibiwa sana?

Magari mengine hayana??

Halafu ni kweli gari inaharibika ikishatolewa
Hiyo?Why?
Sio brevis boss ni magari karibu yote tu, nimeshaona Ist, raum, mark x, crown n.k.

Alteza tu ndo nasikia haikuwekwa madini hayo wameweka material tofauti.

Wanapenda sana kutoa kwenye magari ya injiin kubwa kama vile brevis kwa kuwa hayo madini yanakuwa mengi tofauti na Ist, hvyo pesa inakuwa ndefu. Kwa gari kama brevis nilisikia wanapata mpaka laki 7.

Binafsi sijajua hayo madini wanao nunua wanatengenezea nini. Magari mengi sana kwa sasa yametolewa, ukipiga resi unajua tu au ukiangalia bomba la kutolea moshi kwa chini utaona pia japo kuna baadhi ya magari nasikia huwa hawachani bali wanafungua na kuchokonoa.

Nb: Kwa sasa ukipeleka gari gereji usiliache, pia ukiamwazima mtu gari yako akirudisha kagua, wengine sio waaminifu, unamwazima gari kumbe lengo lake ni hilo tu.
 
Mafundi wa magari maswali yangu mbona sijibiwi?

Ni kweli ukishaibiwa hayo masega gari inaharibika?Kwa nini?

Na kwanini ni Brevis Tu zinaibiwa hayo masega???
 
Sio brevis boss ni magari karibu yote tu, nimeshaona Ist, raum, mark x, crown n.k.

Alteza tu ndo nasikia haikuwekwa madini hayo wameweka material tofauti...

Nimeambiwa Brevis ikishatolewa hayo masega inaharibika kabisa baada ya muda

The way unavyoongea ni kama unaweza ibiwa na gari isibadilike chochote..
Nashindwa kabisa ku elewa hapa
 
Back
Top Bottom