MATUMIZI YA HUO UNGA
Hutumika kuufabya ule moshi unaotoka kwenye bomba uwe msafi kimazingira.
KWANINI HUU UNGA UNAIBWA HAPA BONGO
Huu unga umekuwa dili , wezi wengi (wakiwamo mafundi wenye tamaa) wanaendaga kuuza wanakojua kwa elf 80 hadi laki ya chap chap.
Zimbabwe na South africa kuna makampuni yananunua huo unga, hali hii imepelekea vijana kuchangamkia hili dili, vijana wanakufata ukiwa umepaki gari wakiwa na dola 150 mkononi ( ๐น๐ฟ 347,000 ) wanakuomba wautoe huo unga wakupe pesa, wao wanaenda kuuzia makampuni hata kwa dola 200 (๐น๐ฟ 460,000)
Kiufupi wanaonunua huu unga hapa bongo ๐น๐ฟ wanaendaga kuuza ๐ฟ๐ฆ sauzi au ๐ฟ๐ผ zimbabwe kwa faida kubwa zaidi
HUO UNGA WANAOUNUNUA WANAUTUMIAJE
1.Huo unga husafishwa na mitambo na kuwa mpya (recycled) ili kwenda kuuzwa Marekani na nchi nyingi za ulaya ambazo hawaruhusu gari halirusiwi kutembea barabarani kama linatoa moshi mchafu, huu unga kazi yake ndio kusafisha moshi mchafu, kupata spare mpya ya kifaa chenye unga huu kwa nchi kama marekani unaweza kugharamika hata dola elf 2 (takribani milioni 4 na nusu),
2.Pia huo unga unaweza kuchakatwa na mitambo maalum ili kupata kiasi kidogo cha madini aina ya palladium ambayo yana thamani kuzidi dhahabu, japo zinapatikana gram zisizozidi hata 5 baada ya kuchakatwa na mtambo (grams 28 sawa na ounce 1 bei ni $ 2,500 sawa na 5,780,000 ๐น๐ฟ ).
3. Hii sina uhakika nayo ila kwa spidi ya huu wizi hapa bongo basi itakuwa huu unga ukiibwa gari fulani unaenda kuuzwa kwa alieibiwa.
UFANYE NINI KUEPUKANA NA WIZI HUU
Linda sana gari yako ukienda gereji, ni wizi unaofanyika ndani ya dakika kadhaa tu, ukiona gari yako imechomelewa huko chini kwenye bomba la moshi basi washapita hapo,Pia unaponunua gari kagua vizuri.