Wizi wa catalytic converter kwenye magari 'Masega'

Wizi wa catalytic converter kwenye magari 'Masega'

Cc: Biohazard

1. Kwanza kabisa unajua Oxygen sensor inaathiri vipi ulaji wa mafuta wa gari regardless ni oxygen sensor ipi?

2. Hakuna mahali mimi nmeandika kwamba masega yakitolewa mtu anafungiwa Oxygen sensor tatizo linakuwa limeisha. Unakurupuka sana karudie kusoma post zangu.

3. Zamani engine zilikuwa na Oxygen sensor moja tu. Lakini kwa sasa unakuta engine inakuwa na Oxygen sensor atleast kwa inline na atleast 4 kwa v type. Hizo sensor zimeongezwa kwa sababu ya efficiency. Hivi umeshafikiria engine kama V8 9.0L iwe na single oxygen sensor? Hiyo sensor ikifa gari itakunywa mafuta Bulldozer hutoitamani. Zikiwa nyingi kama ikizingua moja basi ni injector nozzles tu upande fulani ambazo ndio zitaingiza mafuta mengi na consumption haitodeviate sana.

4. Oxygen sensor haihakikishi efficiency katika combution. Kazi yake ni kupima content ya Oxygen iliyopo katika moshi na kutoa taarifa kama Oxygen ikiwa nyingi maana yake mafuta yanaungua mengi hivyo ECU itapunguza muda wa nozzle kuwa wazi. Kama oxygen ikiwa kidogo maana yake mafuta yanaungua kidogo hivyo ECU itaongeza muda wa nozzle kuwa wazi na hapo ndio mafuta huisha haraka.
 
Mafundi wa magari maswali yangu mbona sijibiwi?

Ni kweli ukishaibiwa hayo masega gari inaharibika?Kwa nini?

Na kwanini ni Brevis Tu zinaibiwa hayo masega???
Naomba nikujibu...

Si Brevis tu zinazoibiwa hayo masega, gari lolote hata Passo wanaiba bora tu mazingira ya wizi yawe yamekaa vizuri..

Kitendo cha kuiba huwa ni cha muda mfupi sana....kwa mfano fundi anaweza kukuambia katafute hii spea dukani, akakupa kijana wake uende naye, muda huo ndiyo fundi huku nyuma anapiga bao huku akiwasiliana na kijana wake akimpa uhakika kuwa hamjaanza kurudi... wana mbinu nyingi za kuiba..

Hayo masega (catalytic converter) wengi wameshaeleza kazi yake huko juu...

Labda na mimi nieleze kazi yake ni kusaidia kuunguza tena mchanganyiko wa mafuta na hewa (ambao sasa tuite moshi) ili B kubadilisha moshi huo uwe na gesi ya Carbon dioxide na maji ili visilete athari ya uchafuzi wa hewa...

Utajuaje chawa wameshakuibia masega..

1.Harufu ya moshi wa gari lako itabadilika na utasikia harufu ya petrol mbichi..

2. Mlio wa gari utabadilika kwa kiasi fulani,

3.Kuna baadhi ya magari taa ya check engine itawaka, na kuna mengine taa inaweza isiwake...(yale magari yenye oxygen sensor kabla na baada ya cat converter mara nyingi lazima yawashe check engine light (CEL)

4.Kuna baadhi ya magari ukitoa Cat converter utaona gari limeongeza nguvu kidogo na kiwango cha utumiaji wa mafuta kitapungua kidogo......kwa sababu kuna magari engine zake hazina madhara zikikosa back pressure ambayo hupatikana kwa uwepo wa Cat converter

ila kuna magari ukitoa cat converter hupungua nguvu ya engine na mafuta yatatumika mengi zaidi...Kwa sababu kuna magari engine zake zinafanya kazi vizuri kwa kupata kitu kinaitwa Back pressure ambapo presha hii hutokana na kuwepo kwa cat converter.

Je, ni kweli ukitoa Cat converter gari huharibika kabisa..?

Jibu ni HAPANA na Jibu ni NDIYO.

Jibu La HAPANA linakuja kwa yale magari ambayo yakitolewa cat converter hayawashi CEL....isipowasha CEL ina maana Oxygen sensor bado inapata uwezo wake wa kusoma kiwango cha hewa ambacho hakikuunguzwa during combustion process....kwa hiyo mwenye gari hili anaweza kuendelea kuendesha gari lake japo anakuwa anachafua hewa.

Jibu la NDIYO linakuja pale endapo gari lako umetoa Cat converter, taa ya CEL ikawaka....
Check Engine Light ikiwaka ina maanisha kuwa masega yalipotolewa, moshi unapita kwa haraka bila kizuizi chochote hivyo oxygen sensor inashindwa kusoma kisi cha hewa ambayo haikuungua kwenye combustion chamber.....sensor hii ikishindwa kusoma kiasi cha oxygen ambacho hakijaungua, sensor kupeleka taarifa za uongo kwenye ECU, na ECU inaamuru mifumo ya hewa na mafuta kuingiza mchanginyiko mwingi zaidi wa hewa na mafuta kwenye combustion chamber......

Kitendo hiki hufanya kuwepo na uwiano usio sahihi wa mafuta na hewa...gari lako linaweza ku"behave isivyo kawaida baada ya muda fulani....mwisho wa siku kupelekea damage to other engine components....

Hapa unaweza kuona gari linakunywa mafuta sana lakini nguvu haiendani na mafuta yanayotumika

HITIMISHO...Hayo ndiyo madhara na faida za kuondoa Catalytic Converter a.k.a masega..
Usiondoe Cat converter kama haijaziba, na kama imeziba kidogo inaweza kusafishwa ukapata unafuu.

Mafundi wamekuwa si waaminifu, ni vyema ukimkabidhi gari umwambie nimekuachia gari lenye conditions A,BC...
 
Nilivyoelewa mimi Kwa gari na gari
Mfano Brevis zinaharibika kabisa yakiondolewa hayo masega.
Wakati IST pengine sio sana
Ndio kwa gari nyingine ambazo sensor inawasiliana na Engine Computer Unit au ECU ni lazima mwisho wa siku isababishe malfunction sababu inapeleka signal ya uongo.

Alichoeleza mdau hapo juu ni kina make big sense.

Sent from my Redmi S2 using JamiiForums mobile app
 
Kila gari wanaiba mimi nikiwa Dodoma mwka 2015 nlilaza Mark II GR namba AAA gereji jamaa waliiba,

gari likabadilisha mlio nikawastukia wakaenda kuiba kwingine wakanirudishia

images.jpg

Nasikia kwamba wanatengenezea Milipuko kama baruti kwa ajili ya kulipulia miamba huko kwenye machimbo

imgres.jpg
 
Kila gari wanaiba mimi nikiwa Dodoma mwka 2015 nlilaza Mark II GR namba AAA gereji jamaa waliiba,

gari likabadilisha mlio nikawastukia wakaenda kuiba kwingine wakanirudishia...
Hahahha..pole mkuu...ulikula nao sahani moja wakaona salama yao waine kwingime wakuwekee wewe..

Me naona ifike mahali mafundi wawe na vimikataba simple ambavyo tunasaini pamoja kuwa nimekukabidhi gari lina..

1.Betri aina fulani na ni mpya au kuukuu..
2.Cat converter ipo
3..Raidio aina fulani
4. Taa bado zinang'aa au zimepauka..
na kadhalika..
Hvyo ndiyo vitu vinavyoibiwa kwa haraka sana huko garage..
 
Kwa ujumla bongo, polisi si sehemu salama ya kulala wewe mwenyewe au kulaza mali yako......Jamaa wahuni sana
Kuna mchizi wangu huohuko Dom gari yake ilikamatwa ikakaa siku mbili ile anaenda kuitoa akakuta washaiba fog light na wakabadilisha redio ya screen wakamuwekea nyingine mbovu ila anafatilia wakamchimba biti. kwakua hakutaka makuu akasamehe
 
Noma sana...hao ndiyo watu wanaolinda uslama wa raia na mali zao...

Wanakula sana dhuluma ndiyo maana wengi wao watoto wao huwa hawafanikiwi...
 
We jamaa umeelezea vizuri aione JituMirabaMinne .

Anabisha oxygen sensor haisaidii combustion system.

Anyway nimepata madini mengine ambayo nilikua siyajui.

Tupo kwenye page moja.

Sent from my Redmi S2 using JamiiForums mobile app

Mimi nilichokataa ni wewe kusema eti O2 sensor inamonitor tu na haina kazi nyingine kwa hiyo hata masega yakitolewa hii inakuwa haina kazi. Hapa ndio ulitudanganya.
 
Nilivyoelewa mimi Kwa gari na gari
Mfano Brevis zinaharibika kabisa yakiondolewa hayo masega.
Wakati IST pengine sio sana

Yes.

Kwa ist (ncp61 cc 1500) sijaona madhara kabisa. Tuliyachokonoa masega yote kwenye ist, kwa ridhaa yangu mwenyewe na nikiwepo nashuhudia.

Baada ya hapo gari iliongezeka power ya kukimbia ikawa nyepesi sana tofauti na awali.

Ni mwaka sasa tangu niondoe masega, engine bado mbichiiii na sijawahi kuona check engine light wala nini.

On daily basis naenda KM 70 (go & return). Long trip (KM 700+) kila miezi mitatu. Sijapata any defect na power ya engine inaridhisha to the fullest.
 
Yes

The only impact inayoweza kutokea sababu ile ni sensor ukiitoa itawasha taa ya engine. Na magari yenye mfumo huo ni kuanzia 1996 kuendelea.

Sensor hiyo kazi yake ni kumonitor efficiency ya catalyst converter sasa kama hayo masega yametolewa itafanya kazi gani?

Sent from my Redmi S2 using JamiiForums mobile app
Aiseeeee. Hebu nikuambie kitu kimoja. Katika gari kila sensor unayoijua signal yake lazima inatumika mahali. Siyo tu kumonitor halafu basi.

Mfano ECT sensor na TPS sensor za engine signal zake hutumika katika gear shifting kwenye gearbox.
 
Kwa kizungu inaitwa catalyst inafanya kemikali zingine kureact nayo pasipo yenyewe kunadilika.

Haiwezekani kitu kika react halafu kisibadilike.

Usitake kutudanganya danganya kama wauza dagaa wa ziwani.
 
Back
Top Bottom