Mafundi wa magari maswali yangu mbona sijibiwi?
Ni kweli ukishaibiwa hayo masega gari inaharibika?Kwa nini?
Na kwanini ni Brevis Tu zinaibiwa hayo masega???
Naomba nikujibu...
Si Brevis tu zinazoibiwa hayo masega, gari lolote hata Passo wanaiba bora tu mazingira ya wizi yawe yamekaa vizuri..
Kitendo cha kuiba huwa ni cha muda mfupi sana....kwa mfano fundi anaweza kukuambia katafute hii spea dukani, akakupa kijana wake uende naye, muda huo ndiyo fundi huku nyuma anapiga bao huku akiwasiliana na kijana wake akimpa uhakika kuwa hamjaanza kurudi... wana mbinu nyingi za kuiba..
Hayo masega (catalytic converter) wengi wameshaeleza kazi yake huko juu...
Labda na mimi nieleze kazi yake ni kusaidia kuunguza tena mchanganyiko wa mafuta na hewa (ambao sasa tuite moshi) ili B kubadilisha moshi huo uwe na gesi ya Carbon dioxide na maji ili visilete athari ya uchafuzi wa hewa...
Utajuaje chawa wameshakuibia masega..
1.Harufu ya moshi wa gari lako itabadilika na utasikia harufu ya petrol mbichi..
2. Mlio wa gari utabadilika kwa kiasi fulani,
3.Kuna baadhi ya magari taa ya check engine itawaka, na kuna mengine taa inaweza isiwake...(yale magari yenye oxygen sensor kabla na baada ya cat converter mara nyingi lazima yawashe check engine light (CEL)
4.Kuna baadhi ya magari ukitoa Cat converter utaona gari limeongeza nguvu kidogo na kiwango cha utumiaji wa mafuta kitapungua kidogo......kwa sababu kuna magari engine zake hazina madhara zikikosa back pressure ambayo hupatikana kwa uwepo wa Cat converter
ila kuna magari ukitoa cat converter hupungua nguvu ya engine na mafuta yatatumika mengi zaidi...Kwa sababu kuna magari engine zake zinafanya kazi vizuri kwa kupata kitu kinaitwa Back pressure ambapo presha hii hutokana na kuwepo kwa cat converter.
Je, ni kweli ukitoa Cat converter gari huharibika kabisa..?
Jibu ni HAPANA na Jibu ni NDIYO.
Jibu La HAPANA linakuja kwa yale magari ambayo yakitolewa cat converter hayawashi CEL....isipowasha CEL ina maana Oxygen sensor bado inapata uwezo wake wa kusoma kiwango cha hewa ambacho hakikuunguzwa during combustion process....kwa hiyo mwenye gari hili anaweza kuendelea kuendesha gari lake japo anakuwa anachafua hewa.
Jibu la NDIYO linakuja pale endapo gari lako umetoa Cat converter, taa ya CEL ikawaka....
Check Engine Light ikiwaka ina maanisha kuwa masega yalipotolewa, moshi unapita kwa haraka bila kizuizi chochote hivyo oxygen sensor inashindwa kusoma kisi cha hewa ambayo haikuungua kwenye combustion chamber.....sensor hii ikishindwa kusoma kiasi cha oxygen ambacho hakijaungua, sensor kupeleka taarifa za uongo kwenye ECU, na ECU inaamuru mifumo ya hewa na mafuta kuingiza mchanginyiko mwingi zaidi wa hewa na mafuta kwenye combustion chamber......
Kitendo hiki hufanya kuwepo na uwiano usio sahihi wa mafuta na hewa...gari lako linaweza ku"behave isivyo kawaida baada ya muda fulani....mwisho wa siku kupelekea damage to other engine components....
Hapa unaweza kuona gari linakunywa mafuta sana lakini nguvu haiendani na mafuta yanayotumika
HITIMISHO...Hayo ndiyo madhara na faida za kuondoa Catalytic Converter a.k.a masega..
Usiondoe Cat converter kama haijaziba, na kama imeziba kidogo inaweza kusafishwa ukapata unafuu.
Mafundi wamekuwa si waaminifu, ni vyema ukimkabidhi gari umwambie nimekuachia gari lenye conditions A,BC...