Uchaguzi 2020 Yaliyojiri katika Kampeni za Tundu Lissu Jijini Mwanza

Uchaguzi 2020 Yaliyojiri katika Kampeni za Tundu Lissu Jijini Mwanza

Hao wanaoshinda uchaguzi kutoka vyama vya upinzani, tume inakuwa ni nyingine au ni hii hii?.

Wapinzani huwa wanatangazwa washindi baada kujitoa muhanga. Na isitoshe hayo yalifanyika wakati wa JK wakati demokrasia ikiwa na nafuu.
 
Tundu Lissu Mwanza;
Viwanja vyote vya ndege vilianzishwa na Waingereza isipokuwa KIA, Songwe na Chato.
Reli inayokuja Mwanza ilijengwa na Waingereza.
Reli ya Tanga hadi Arusha ilijengwa na Wajerumani.
Reli ya Kati ilijengwa na Wajerumani.
Reli ya TAZARA ilijengwa na Nyerere kwa msaada wa Wachina.

Bandari ya Mwanza ilianzishwa na Wajerumani.
Bandari ya Kigoma ilianzishwa na Wajerumani.
Bandari zote kubwa za bahari ya hindi zilianzishwa na Wajerumani.

Hata ikulu ya Dar es salaam ilijengwa na Wajerumani na baadae ikaboreshwa na Waingereza.

Kwanini tuliwakataa Waingereza na Wajerumani?
Ni kwa sababu utawala wao haukuwa wa haki.

Oktoba mwaka 1968 Mwalimu Nyerere alichapisha andiko lake liloitwa Uhuru na Maendeleo.

Mwalimu alisema, Uhuru na Maendeleo ni kama Kuku na Yai. Hupati Kuku bila Yai na hupati Yai bila Kuku. Hupati maendeleo bila Uhuru na hupati Uhuru bila maendeleo. Maendeleo lazima yahusishe watu. Vitu kama barabara, majengo makubwa, reli nk sio maendeleo, bali ni nyenzo za kutuletea maendeleo. Hakuna maana kama tunajenga mabarabara halafu raia wanakamatwa hovyo kwa sababu ya kumuudhi mtu mwenye madaraka.

Lissu akaendelea.
Sikatai kuwa ujenzi wa barabara ni jambo zuri. Sikatai ujenzi wa reli ni jambo zuri.
Lakini utawala wa haki ni muhimu kuliko hayo yote.
------------------------------------------------------------------------------------------------------

Rais wa Marekani, Ronald Reagan aliwahi kusema maneno kama hayo. Akaongeza kuwa Raia wa Marekani ana thamani kubwa kuliko mabarabara ya ghorofa na silaha za Nyuklia. Kwa sababu hayo yote yapo kwa faida ya Raia wa Marekani, na sio kwamba Raia wa Marekani yupo kwa faida ya hivyo vitu.
Theodore Roosevelt naye alisema; haki za Mali na haki za binadamu zinakwenda sawa. Lakini ikitokea haki hizi zinapihana basi haki za binadamu zipewe kipaumbele. Kwa sababu Mali zipo ili zimnufaishe binadamu, sio binadamu azinufaishe mali.

Kwa lugha nyepesi ili mswahili wa kawiada aelewe; ni kwamba, Kujenga miundombinu ya mikubwa huku wananchi wakitegemea mlo mmoja, huku raia wana hofu ya kutoa maoni yao, bado watu wanatekwa, kupotezwa na kuuawa bila uchunguzi, huku miili ya watu inaokotwa halafu serikali inaizika bila uchunguzi...

Asante Mwanza, Asante Tanzania.View attachment 1555631View attachment 1555632
Nikweli imetia fola,ila ameishtua anaposema Serikali yangu.......au ndiyo yaleyale kwamba wanasiasa wote sawa....Magu alilaumiwa na kurushiwa Sana mawe hasa aliposema Serikali yangu badala ya serikali ya sisiemu......tuendelee kula mtori nyama tutazikuta chini
 
Chini ya rais huyu na tume hii isiyo huru ya uchaguzi, hakuna uchaguzi bali kuna maonyesho ya kipimo cha ujinga wa mtu mweusi.
Kama unalijua hilo basi usitumie nguvu tulia usiburi october
 
Kwani magu Leo singida kasema atafanya nn?
Nimeshangaa anajitambulisha jina lake wkt hawa mazezeta ya lumumba yanasema hakuna asiyejua magufuli kafanya nn chato
 
Kuwe na fair play basi, sasa mnapitisha wabunge bila kilupingwa kisha mnajimwambafay.
Hao wabunge wa kupita bila kupingwa ndiyo huwa vinara wa kupitisha miswada mibovu bungeni, bunge la kupita bila kupingwa ni Bunge la laana halina baraka za wananchi
 
Lowassa hakuwa mpinzani, bali alikuwa ni tapeli wa kisiasa aliyekosa nafasi ya kugombea urais kupitia ccm, akanunua nafasi hiyo kupitia cdm.
Huyu wa sasa ni hatari kwani ni mtekelezaji wa hoja mbaya zenye agenda iliyojificha.
 
Hao wabunge wa kupita bila kupingwa ndiyo huwa vinara wa kupitisha miswada mibovu bungeni, bunge la kupita bila kupingwa ni Bunge la laana halina baraka za wananchi
Kupita bila kupingwa ni ushahidi kuwa umewavunja nguvu ya apinzani wako.
 
Kama unalijua hilo basi usitumie nguvu tulia usiburi october

Ww ndio unatakiwa kusubiri, mimi sina cha kusubiri maana najua hakuna uchaguzi, bali kuna ushenzi kama ushenzi mwingine.
 
Wapinzani huwa wanatangazwa washindi baada kujitoa muhanga. Na isitoshe hayo yalifanyika wakati wa JK wakati demokrasia ikiwa na nafuu.
Ukijua unawafanyia nini watu na wakakubaliana na unachokifanya, tume hata iundwe na watu kutoka China na Marekani utashinda tu uchaguzi.

Ukiwa na substance katika kila unachokifanya pasipo kupenda siasa za kiuanaharakati hautakuwa na mashaka na tume ya uchaguzi.
 
Kwani kujaa kwa watu kwenye mkutano ni ishara ya kumpa kura ? Wengine wameenda kushangaa aliyepigwa risasi bado yupo hai? .... Huwajui wasukuma wewe tuulize sisi msukuma anapelekwa pilisi ukimuuliza vipi anakujibu ndoho tabu , yaani hakuna shida ..... Wasukuma wepesi wa kukubali juuu juu ila subiri kwenye vitendo ndio utachoka ngome ya ccm ni kanda ya ziwa subiri october utaamini haya ninayokwambia hata leo nilikuwepo Mwanza yaliyotokea ni ya kawaida sana ni jmati tu kama wa mkutano wa injili wa mwl mwakasege ... october sio mbali utaona
Lakini mwanza mbona siyo ya wasukuma, fuatilia utajua ukweli
 
Hoja za kipumbavu kabisa. Utawala wa ujerumani na waingereza hata ungekuwa wa kimalaika, bado tusingeukubali sababu ni ukoloni, ukoloni ni kitu ambae hakuna anaweza kukikubali, hata iweje.

Marndeleo ya watu yataletwa na vitu, au hamuini jinsi maendeleo ya watu yanavoweza kuletea na umeme wa kutosha na wa bei nafuu toka Rufiji, huo ni mfano mmoja tu.

Hili xenge halina hoja, ni kubwabwaja utumbo tu, linakera sana!
Mbona mkoloni mweusi ccm ametawala miaka 60 huunhanishi nguvu kumtoa huku akifanya mambo machafu zaidi ya wakoloni weupe?
 
Uvccm kwa sasa hivi wamehamia kwenye kushindanisha umahiri wa kucheza SINGELI baada ya mgombea wao kuwaruka kwenye sera na kujikuta anaongelea kugongana bila kinga.
😆😆😆😆😆😆😆😆🤸🤸🤸 We jamaa wewe ni ful comedian aisee nimecheka balaa
 
Ukijua unawafanyia nini watu na wakakubaliana na unachokifanya, tume hata iundwe na watu kutoka China na Marekani utashinda tu uchaguzi.

Ukiwa na substance katika kila unachokifanya pasipo kupenda siasa za kiuanaharakati hautakuwa na mashaka na tume ya uchaguzi.

Kwa macho yangu nimeshuhudia ushenzi, ukatili na uhayawani wa wazi dhidi vya wapinzani ili ccm watangazwe washindi. Na uhayawani huo ulikuwa ukiratibiwa na tume ya uchaguzi na vyombo vya dola. Usidhani mambo hayo yalipokuwa yakifanyika tulikuwa hatuyaoni.
 
Back
Top Bottom