tweenty4seven
JF-Expert Member
- Sep 21, 2013
- 15,863
- 19,626
Hii nimeshuhudia live mitaa ya round about ya utopolo mkoa,rpc kaziba njia ya nyerere road msafara usipite wananzengo wakataka kulianzisha.Tundu Antipas Lissu Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewasili Mwanza kwa kishindo kikubwa.
Akiambatana na Mgombea Mwenza pamoja na Mwenyekiti wa chama Freeman Mbowe mgombea huyo amelakiwa na umati mkubwa wa watu ambapo maandamano yameanzia katika Uwanja wa ndege kuelekea Uwanja wa Furahisha.
Msururu mkubwa wa Bodaboda,magari na watu kujipanga kandokando ya Barabara ndivyo vilivyopamba mapokezi yake.
-------------------
Yaliyojiri mkutanoni Viwanja vya Furahisha
Akihutubia Malaki ya watu mgombea wa Urais Tundu Lissu alilaani serikali ya CCM kwa kumhujumu zao la Pamba ambalo no kitega uchumi Cha watu wa Kanda ya ziwa.
Lissu amesema serikali yake itawajali Wafanyakazi na kila mwaka wataongezewa mshahara kwa mujibu wa sheria za nchi.
Amesema serikali yake inafuata kauli Mbiu ya Uhuru Haki na Maendeleo ya watu.
Amesema serikali yake itaondoa ukandamizaji wa wafanyabiashara ambapo kwa Sasa Mamlaka ya Mapato Tanzania imekuwa sehemu ya kuhujumu na kuua biashara za Watanzania.
Awali Lissu alisema tangu arejee nchini Mapokezi ya Mwanza ndiyo yamevunja Rekodi kwa wingi wa watu
View attachment 1555426View attachment 1555625View attachment 1555626View attachment 1555627View attachment 1555628
Busara za wenje ndio zimesaidia