Uchaguzi 2020 Yaliyojiri katika Kampeni za Tundu Lissu Jijini Mwanza

Uchaguzi 2020 Yaliyojiri katika Kampeni za Tundu Lissu Jijini Mwanza

Tundu Antipas Lissu Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewasili Mwanza kwa kishindo kikubwa.

Akiambatana na Mgombea Mwenza pamoja na Mwenyekiti wa chama Freeman Mbowe mgombea huyo amelakiwa na umati mkubwa wa watu ambapo maandamano yameanzia katika Uwanja wa ndege kuelekea Uwanja wa Furahisha.

Msururu mkubwa wa Bodaboda,magari na watu kujipanga kandokando ya Barabara ndivyo vilivyopamba mapokezi yake.

-------------------

Yaliyojiri mkutanoni Viwanja vya Furahisha

Akihutubia Malaki ya watu mgombea wa Urais Tundu Lissu alilaani serikali ya CCM kwa kumhujumu zao la Pamba ambalo no kitega uchumi Cha watu wa Kanda ya ziwa.

Lissu amesema serikali yake itawajali Wafanyakazi na kila mwaka wataongezewa mshahara kwa mujibu wa sheria za nchi.

Amesema serikali yake inafuata kauli Mbiu ya Uhuru Haki na Maendeleo ya watu.

Amesema serikali yake itaondoa ukandamizaji wa wafanyabiashara ambapo kwa Sasa Mamlaka ya Mapato Tanzania imekuwa sehemu ya kuhujumu na kuua biashara za Watanzania.

Awali Lissu alisema tangu arejee nchini Mapokezi ya Mwanza ndiyo yamevunja Rekodi kwa wingi wa watu
View attachment 1555426View attachment 1555625View attachment 1555626View attachment 1555627View attachment 1555628
Hii nimeshuhudia live mitaa ya round about ya utopolo mkoa,rpc kaziba njia ya nyerere road msafara usipite wananzengo wakataka kulianzisha.
Busara za wenje ndio zimesaidia
 
Baada ya mahudhurio viwanjani kudoda Chadema wamehamia kwenye mapokezi ambapo wanakodi bodaboda na honi zao na mbwembwe zao za uendeshaji na kulipa vijana wa kuruka ruka njiani Kama chura katumbukia kwenye sufuria la moto la mpika supu ili kuvutia mabarabarani watu wawasogelee kuwaona Halafu wanasema cheki anavyokubalika!!!

Nenda viwanjani uone vituko bodaboda wote wakishamfikisha uwanjani wanambwaga Hapo hapo hao wanaondoka zao kuendelea na shughuli zao hawana Mpango na Mkutano wake

Anayebisha aeleze huo umati wa bodaboda mbona hazionekani hapo mkutanoni zimepaki kusikiliza mgombea?

Cha kukodi hakikai mkutanoni!!!!
Nyie wasanii 200 ni sawaa
 
Mgombea Urais wa Chadema Tundu Lissu leo anatarajiwa kuitikisa jiji la Mwanza katika mkutano mkubwa wa Hadhara katika viwanja vya Furahisha.

Tayari maandalizi yamekamilika na maandamano makubwa ya kumlaki yanasubiriwa kuanza wakati wowote kutoka sasa

Tayari mgombea huyo ameshafanya mikutano minne ya kampeni ambapo mitatu ilikuwa jijini DSM na mmoja ulikuwa jijini Arusha hapo Jana.

Chadema katika uchaguzi mkuu huu inatumia kauli Mbiu ya Uhuru,Haki na Maendeleo ya watu.

#UhuruHakiNaMaendeleoyawatu#
#Niyeye2020#
Molemo nyie ndio mnakwamisha maendeleo. Yaani mmeshindwa kuwa live kwa sababu gani? Leo nimehangaika kufuatilia naambulia vipande viapande tu vya dakika 3? Bure kabisa ngombe nyie!
 
Kwa kile nilichokiona leo mwanza nimeanza kuwa na mashaka Nahisi kuna nguvu ya ajabu aliyonayo huyu mhe lissu hatà kama ni mahaba kwa watu wa mwanza hii sasa imepitiliza mpaka nimehisi kuwa inawezekana wale wachawi 900 wamemkimbia mzeee hivyo upepo umegeukia upande wa lissu! Ikiwa upepo utaendelea hivi basi inabidi ccm waachane na maswala ya wasanii wajipime kwa kufanya mkutano bila wasanii ili waone kama kweli huu mziki watauweza vinginevyo hawataamini 28
 
Baada ya mahudhurio viwanjani kudoda Chadema wamehamia kwenye mapokezi ambapo wanakodi bodaboda na honi zao na mbwembwe zao za uendeshaji na kulipa vijana wa kuruka ruka njiani Kama chura katumbukia kwenye sufuria la moto la mpika supu ili kuvutia mabarabarani watu wawasogelee kuwaona Halafu wanasema cheki anavyokubalika!!!

Nenda viwanjani uone vituko bodaboda wote wakishamfikisha uwanjani wanambwaga Hapo hapo hao wanaondoka zao kuendelea na shughuli zao hawana Mpango na Mkutano wake

Anayebisha aeleze huo umati wa bodaboda mbona hazionekani hapo mkutanoni zimepaki kusikiliza mgombea?

Cha kukodi hakikai mkutanoni!!!!

Mwaka huu mtachina.
 
Attachments

  • VID-20200901-WA0027.mp4
    1.2 MB
Mumekusanya bodaboda na wakurya wamilimani,
 
Uwanja wa furahisha Ni padogo Sana Ni saizi ya mwakasege asubiri JPM atakapo tia team
 
Back
Top Bottom