Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hizo kiki za kipuuzi hazitotusahaulisha BEI ZA MAFUTA kandamizi Kwa Raia. Hakuna case hapo.Lema Alivuliwa Ubunge Na Mahakama, Alikata Rufaa Lakini Alifukuzwa Bungeni, Spika Hakusubiri Rufaa Yake Isikilizwe, Wabunge 9 wa CUF Walifukuzwa Uanachama. Walienda Mahakamani Lakini Walitolewa Bungeni, Spika Hakusubiri Kesi Yao Isikilizwe, Je Kwa Kina Halima Sheria Imebadilika?
Uchafuzi uliyofanyika uchaguzi uliyopita utachukua muda mrefu kusafishika, hivyo tuombe uishe kwa salama.Ni kinyaa kitupu ukisikiliza anachosema. Huwa najiuliza imekuwaje tunaongozwa na watu wajinga wa kiwango hiki. Cha ajabu watu wanaofanya haya wanajiita ni wasomi!
Nilichogundua baada ya ccm kupoteza ushawishi kwa umma na kuamua kutumia vyombo vya dola kukaa madarakani kwa shuruti, kumetokea ukiukwaji mkubwa wa sheria, na hali inazidi kuwa mbaya labda CDM ifutwe au wakubali kutawaliwa na ccm kwa mabavu. Na tabia hii ya ukiukwaji mkubwa wa sheria itachukua muda mrefu hadi hali halisi kujirudia.
Wachaaaaa! Nipo hapa nasikiliziaKesi namba 16 ya mwaka 2022 iliyofunguliwa Mahakama Kuu na Wabunge 19 wa viti maalum wa CHADEMA kupinga uamuzi wa kuwavua uanachama na mwenendo mzima wa maamuzi yaliyofanyika dhidi ya Baraza la Wadhamini CHADEMA, tume ya Taifa ya Uchaguzi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Kaa nami kujua yatakayojiri Mahakama Kuu, Dar.
==========
Wakili Peter Kibatala na Wakili John Malya tayari wapo ndani ya Chumba Cha Mahakama Mbele ya Jaji Mgeta.
Jopo la mawakili wa Chadema lina mawakili wanne Adv. Kibatala Adv. Mtobesya Adv. J. Mndeme Adv. j. Malya Wengine. Kesi namba 16 ya Mwaka 2022, Mdee na Wenzake 18, ilifunguliwa Mahakama Kuu Mbele ya Jaji Mgeta.
Mdee na wenzake 18 Wanawakilishwa na Mawakili Adv Ikupilika Panya, Adv Edson Kilatu na Adv Aliko Mwamanenge. Baadae likaingia Jopo la Mawakili wa Serikali wapo Wanne Wakiongozwa na Wakili Gabriel Mallata.
Mawakili wa Mdee na wenzake wametoa ombi la Mahakama Iweke zuio "Court Injunction"Wasivuliwe Ubunge na Bunge. Wanaomba Kwanza Mahakama itoe zuio la Mdee na wenzake waendelee Kuwa wabunge mpaka pale ambapo Kesi ya msingi Kesi itakapoisha. Baada Wasilisho lao, Mahakama italazimika Kusikiliza Ombi hilo Kwanza kutoka pande zote.
Amesimama wakili Peter Kibatala anachambua kwanza Viapo vyao ambavyo vimesainiwa na Mawakili wao na Wateja (Wakina Mdee)
Mawakili wa CHADEMA wanaendelea Kuchambua Viapo na Kutaja Mahitaji ya Kisheria na sifa zinazohitajika katika Viapo wakiwa na Lengo Kuweka Zuio la awali, preliminary Objection (P.O) Mahakama isikubali Kupokea Maombi yao ya kesi.
- Viapo havionyeshi waapaji (Wakina Mdee) Wameapa wapi.
- Waapaji hawajataja Dini zao katika Viapo vyote
- Ombi lao la kubaki na ubunge halijaelekezwa kwa yoyote kati ya wadaiwa (Mdee na wenzake)
- Katika maombi yao hawasemi kama wanataka kuendelea kuwa wanachama wa Chadema ila wanataka kuendelea na ubunge tu.
Mawakili wa Halima Mdee na wenzake kwa pamoja na Mawakili wa Serikali Wanafanya (Re-joinder) Wanasimama kujibu hoja za Jopo la Mawakili wa Chadema Kuhusu hitilafu katika Viapo na Mapungufu yake katika ufunguaji wa Kesi.
Majibu ya wakili wa Halima Mdee na wenzake 18
Mawakili wa wabunge 19 na Wanasheria Serikali wanaomba wapewe "status quo" Wakitaka Wakina Mdee na wenzake Waendelee Kuwa Wabunge mpaka Kesi ya Msingi itakapo malizika Kusikilizwa.
- Wamesema hawajataja dini lakini kiapo kinajieleza
- Wahusika wanaoombewa amri wametajwa kwenye Viapo
- Wamekubali baada ya kuelekezwa na Mahakama kwamba inaongeza jambo jipya
- Kuhusu kumuunganisha Speaker au Katibu wa Bunge, amri zilizoombwa zimeombwa na wahusika ambao wapo kwenye Maombi yaani Chadema, NEC (tume ya Uchaguzi) na Mwanasheria Mkuu
- Kuhusu kwamba NEC ina ulinzi wa Katiba chini ya ibara ya 74(12), hakuna sehemu ambayo wao wameombwa kuchunguza NEC
- Kuhusu kwamba hakuna hatari yoyote inayopelekea kutolewa kwa amri iliyoonyeshwa na waleta maombi, wamesema hii ni amri ya upande mmoja na kwenye hayo maombi ya amri hiyo; wameomba kwamba wasitolewe kama wabunge wa viti maalum Kwamba wadaiwa wanajua kwamba watatolewa kuwa Wabunge.
Yanasubiriwa maamuzi ya Jaji
Pia, soma=> Wabunge 19 viti maalum CHADEMA wafungua kesi. Bunge lasema linasubiri uamuzi wa Mahakama kuu
umejaza usaha kichwani unajiita una akili bumunda weweTulikubaliana tupo awamu inayotenda haki. Tusihangaike ku-influence kwa namna iwayo yote uamuzi wa mahakama. Tuwaachie mawakili na wanasheria wafanye kazi zao.
Na yeye amejuaje leo hii,kabla ya Tulia?Hii ni tweet ya Godbless Lema:
Mawakili wa Mdee na Wanasheria Serikali wa Serikali Katika Maombi ya😵mbi la Kwanza Wanaomba Mahakama Iweke zuio "Court Injunction"Wasivuliwe Ubunge na Bunge
Kabla ya ombi hili halija sikilizwa Leo asubuhi Spika Tulia Kashasema wataendelea na Ubunge.
Bunge linaheshimu mahakama, kama mahakama inavyoheshimu Bunge, yaani mtafika 2025 mmmechokaa, na bado, kazi yetu ni kuwapa matukio ya kukimbizana nayo Kila kukichaHii ni tweet ya Godbless Lema:
Mawakili wa Mdee na Wanasheria Serikali Katika Maombi ya ombi la Kwanza Wanaomba Mahakama Iweke zuio "Court Injunction"Wasivuliwe Ubunge na Bunge
Kabla ya ombi hili halija sikilizwa Leo asubuhi Spika Tulia Kashasema wataendelea na Ubunge.
Ahhh ahhhKwamba Tanzania itafutika!!![emoji56][emoji56][emoji56]
Au itaondolewa duniani!!![emoji23][emoji23][emoji23]
Sent from my TECNO Camon CX using JamiiForums mobile app
Hata hivyo kwa kauli ya spika kuwabakiza bungeni kwa maelekezo yapi ya mahakama? issue tunajiuliza kuna amri gani ya mahakama inayowataka waendelee kuwa bungeni spika hapa kuna shida. Leo ndio warufani ndiyo wameomba suala lao lisikilizwe na kuwa wameomba wasitolewe bungeni sasa mbona bado wamo bungeni wanaomba nini?utra viresLema Alivuliwa Ubunge Na Mahakama, Alikata Rufaa Lakini Alifukuzwa Bungeni, Spika Hakusubiri Rufaa Yake Isikilizwe, Wabunge 9 wa CUF Walifukuzwa Uanachama. Walienda Mahakamani Lakini Walitolewa Bungeni, Spika Hakusubiri Kesi Yao Isikilizwe, Je Kwa Kina Halima Sheria Imebadilika?
Yeah leo wameingia bungeni kwa amri ya nani?Sasa Spika aliwaruhusuje kuendelea kubaki Bungeni wakati hakuwa na zuio la Mahakama?
Eti huyu ndio mwanasheria wa kiwango cha Phd na ndio anaongoza Bunge.
Hii nchi imepatwa mchana kweupe
Kwa vituko hivi, ndio mjue hapa hata kesi hamna.