Yaliyojiri kesi ya Wabunge 19 waliovuliwa uanachama Vs CHADEMA. Mahakama yaridhia Ubunge wao uendelee wakati kesi ikiendelea
Ni kinyaa kitupu ukisikiliza anachosema. Huwa najiuliza imekuwaje tunaongozwa na watu wajinga wa kiwango hiki. Cha ajabu watu wanaofanya haya wanajiita ni wasomi!

Nilichogundua baada ya ccm kupoteza ushawishi kwa umma na kuamua kutumia vyombo vya dola kukaa madarakani kwa shuruti, kumetokea ukiukwaji mkubwa wa sheria, na hali inazidi kuwa mbaya labda CDM ifutwe au wakubali kutawaliwa na ccm kwa mabavu. Na tabia hii ya ukiukwaji mkubwa wa sheria itachukua muda mrefu hadi hali halisi kujirudia.
Kwani dhalimu bado yupo?

Si mnapumua nyie?
 
Tanzania ikiendelea kucheza siasa hizi, haitadumu miaka 50 ijayo.

Kama kamati ya bunge ilimpa ushasuri Spika naye akawaambia anakwenda kuwauliza wakubwa zake je huo Muhimili wa Bunge uko huru? Ndio maana tutaka Katiba itakayotupa muhimili wa Bunge ulio huru kwa kumpata SPIKA ambaye hatapata maelekezo kutoka Muhimili mwingine!! Ilivyo sasa ni muendelezo ule ule wa Marehemu JIWE!!

Samia hawezi kupata siasa za kistaarabu kwa mtindo huu, kuna masalia ya Magufuli yanayotaka kuchafua utawala wake kwa kwenda kinyume na yale anayoyahubiri!!
 
-Kuna kila dalili Mhimili wa Bunge na Mhimili wa Mahakama walipanga matokeo,
-kwa nini kauli ya Kiti ya asubuhi ndiyo imefanyiwa kazi na Jaji jioni hii kukidhi vigezo,vya kutowasimamisha wabunge 19,waliofukuzwa uanachama CHADEMA, hakuna Uhuru wa Mhimili wa Mahakama/Bunge.
-Kauli ya Mhimili wa Bunge ya asubuhi ndiyo imefanyiwa kazi jioni hii.
-Kiti kijitafakari na kufanya maamuzi kwa weledi,ili kulinda heshima ya chombo nyeti.
-Huyo Judge wa Mahakama Kuu, nadhani ni mbobezi wa masuala ya katiba,afanye kazi kwa weledi ili kulinda heshima ya Muhimbili wa Mahakama.
 
CDM waulezee umma kosa la kina mama nini hasa?

Lissu kukataa matokeo ya uchaguzi aina maana CDM nzima iburuzwe kukataa matokeo.

Na kanuni gani za katiba ya CDM zilizotumika kuwavua uanachama, kosa lolote la kufukzwa chama lazima liwe limeorodheshwa, vinginevyo mwenyekiti kila anapopishana na mtu anaitisha kikao wanaamua maazimio uchwara unafukuzwa.

Ndio kama kosa la hakina mama kwenda kinyume na mtazamo wa Mbowe au Lissu au mwenyekiti wa chama chochote sio sababu ya kufukuzwa uanachama.

Ingekuwa ivyo msukuma, jerry slaa, nchimbi, bashe na genge lote lililopingana kukatwa kwa Lowassa sasa hivi wasingekuwa ndani ya CCM.

Hii kesi sio ya kufukuzwa ubunge tu na uanachama ni namna vyama vya siasa vinavyoendeshwa pia aiwezekani kila anachosema Lissu kwa maslahi yake binafsi liwe agizo la kila mtu.

Yaani Mbowe na Lissu ata kama wakifanya maamuzi ya ovyo CDM wote wanatakiwa kusema sawa baba; huko sasa ndio kutokuwa huru. Ata hao CCM japo awapingani hadharani lakini wakiingia kwenye caucus zao za vyama wanajiachia.

Haki kwa hakina mama ata wao walikipigania chama.

Kweli Tanzania haki ipo anaebisha ni mkaidi tu, ni kanuni gani za chama walizovunja kwenda kinyume na mtazamo wa Lissu sio kigezo cha kufukuza watu ovyo.
 
Niamini sasa kama Wahazabe, kuna Mungu wa mchana na wa usiku. Wa usiku ni wa kupanga michango tu.
 
Wataumbuka japo watabebwa.

Sasa Spika asubuhi ya leo aliwaruhusu kubaki Bungeni kwa amri ya Mahakama ipi ili hali jioni hii ndio Mahakama inatoa zuio?

Eti huyu ndio msomi wa kiwango cha Phd na ni mwanasheria!

Pathetic!
That's a problem...

Ni kuvunja sheria na kukiuka katiba ya JMT kwa kwenda mbele...!
 
Niamini sasa kama Wahazabe, kuna Mungu wa mchana naye wa usiku. Wa usiku ni wa kupanga michongo tu.
 
Niamini sasa kama Wahazabe, kuna Mungu wa mchana na wa usiku. Wa usiku ni wa kupanga michango tu.
Unasema nini ndugu? Hoja yako ni nini hapa? Ni Tundu Lissu, Freeman Mbowe au CHADEMA na katiba/kanuni zao?

Kwani wewe unayelalamika umeona ni kanuni au utaratibu gani umekiukwa na CHADEMA ktk kuchukua hatua za kusimamia nidhamu ya wanachama wao ..?

Sema halafu ndo tujadiliane. Lakini mjadala unakuwa mgumu if you're speaking out of nothing...!!
 
Waachwe tu jamani..hapo kila mtu anapigania tumbo lake na familia yake
 
CDM waulezee umma kosa la kina mama nini hasa?

Lissu kukataa matokeo ya uchaguzi aina maana CDM nzima iburuzwe kukataa matokeo.

Na kanuni gani za katiba ya CDM zilizotumika kuwavua uanachama, kosa lolote la kufukzwa chama lazima liwe limeorodheshwa, vinginevyo mwenyekiti kila anapopishana na mtu anaitisha kikao wanaamua maazimio uchwara unafukuzwa.

Ndio kama kosa la hakina mama kwenda kinyume na mtazamo wa Mbowe au Lissu au mwenyekiti wa chama chochote sio sababu ya kufukuzwa uanachama.

Ingekuwa ivyo msukuma, jerry slaa, nchimbi, bashe na genge lote lililopingana kukatwa kwa Lowassa sasa hivi wasingekuwa ndani ya CCM.

Hii kesi sio ya kufukuzwa ubunge tu na uanachama ni namna vyama vya siasa vinavyoendeshwa pia aiwezekani kila anachosema Lissu kwa maslahi yake binafsi liwe agizo la kila mtu.

Yaani Mbowe na Lissu ata kama wakifanya maamuzi ya ovyo CDM wote wanatakiwa kusema sawa baba; huko sasa ndio kutokuwa huru. Ata hao CCM japo awapingani hadharani lakini wakiingia kwenye caucus zao za vyama wanajiachia.

Haki kwa hakina mama ata wao walikipigania chama.

Kweli Tanzania haki ipo anaebisha ni mkaidi tu, ni kanuni gani za chama walizovunja kwenda kinyume na mtazamo wa Lissu sio kigezo cha kufukuza watu ovyo.
Kwa kilio cha kichawi kama hivyo, nadhani unafaa sana kwenda UMOJA party
 
Kesi namba 16 ya mwaka 2022 iliyofunguliwa Mahakama Kuu na Wabunge 19 wa viti maalum wa CHADEMA kupinga uamuzi wa kuwavua uanachama na mwenendo mzima wa maamuzi yaliyofanyika dhidi ya Baraza la Wadhamini CHADEMA, tume ya Taifa ya Uchaguzi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali inaendelea Mahakama Kuu.

Kaa nami kujua yatakayojiri Mahakama Kuu, Dar.

==========

Wakili Peter Kibatala na Wakili John Malya tayari wapo ndani ya Chumba Cha Mahakama Mbele ya Jaji Mgeta.

Jopo la mawakili wa Chadema lina mawakili wanne Adv. Kibatala Adv. Mtobesya Adv. J. Mndeme Adv. j. Malya Wengine. Kesi namba 16 ya Mwaka 2022, Mdee na Wenzake 18, ilifunguliwa Mahakama Kuu Mbele ya Jaji Mgeta.

Mdee na wenzake 18 Wanawakilishwa na Mawakili Adv Ikupilika Panya, Adv Edson Kilatu na Adv Aliko Mwamanenge. Baadae likaingia Jopo la Mawakili wa Serikali wapo Wanne Wakiongozwa na Wakili Gabriel Mallata.

Mawakili wa Mdee na wenzake wametoa ombi la Mahakama Iweke zuio "Court Injunction"Wasivuliwe Ubunge na Bunge. Wanaomba Kwanza Mahakama itoe zuio la Mdee na wenzake waendelee Kuwa wabunge mpaka pale ambapo Kesi ya msingi Kesi itakapoisha. Baada Wasilisho lao, Mahakama italazimika Kusikiliza Ombi hilo Kwanza kutoka pande zote.

Amesimama wakili Peter Kibatala anachambua kwanza Viapo vyao ambavyo vimesainiwa na Mawakili wao na Wateja (Wakina Mdee)
  1. Viapo havionyeshi waapaji (Wakina Mdee) Wameapa wapi.
  2. Waapaji hawajataja Dini zao katika Viapo vyote
  3. Ombi lao la kubaki na ubunge halijaelekezwa kwa yoyote kati ya wadaiwa (Mdee na wenzake)
  4. Katika maombi yao hawasemi kama wanataka kuendelea kuwa wanachama wa Chadema ila wanataka kuendelea na ubunge tu.
Mawakili wa CHADEMA wanaendelea Kuchambua Viapo na Kutaja Mahitaji ya Kisheria na sifa zinazohitajika katika Viapo wakiwa na Lengo Kuweka Zuio la awali, preliminary Objection (P.O) Mahakama isikubali Kupokea Maombi yao ya kesi.

Mawakili wa Halima Mdee na wenzake kwa pamoja na Mawakili wa Serikali Wanafanya (Re-joinder) Wanasimama kujibu hoja za Jopo la Mawakili wa Chadema Kuhusu hitilafu katika Viapo na Mapungufu yake katika ufunguaji wa Kesi.

Majibu ya wakili wa Halima Mdee na wenzake 18
  1. Wamesema hawajataja dini lakini kiapo kinajieleza
  2. Wahusika wanaoombewa amri wametajwa kwenye Viapo
  3. Wamekubali baada ya kuelekezwa na Mahakama kwamba inaongeza jambo jipya
  4. Kuhusu kumuunganisha Speaker au Katibu wa Bunge, amri zilizoombwa zimeombwa na wahusika ambao wapo kwenye Maombi yaani Chadema, NEC (tume ya Uchaguzi) na Mwanasheria Mkuu
  5. Kuhusu kwamba NEC ina ulinzi wa Katiba chini ya ibara ya 74(12), hakuna sehemu ambayo wao wameombwa kuchunguza NEC
  6. Kuhusu kwamba hakuna hatari yoyote inayopelekea kutolewa kwa amri iliyoonyeshwa na waleta maombi, wamesema hii ni amri ya upande mmoja na kwenye hayo maombi ya amri hiyo; wameomba kwamba wasitolewe kama wabunge wa viti maalum Kwamba wadaiwa wanajua kwamba watatolewa kuwa Wabunge.
Mawakili wa wabunge 19 na Wanasheria Serikali wanaomba wapewe "status quo" Wakitaka Wakina Mdee na wenzake Waendelee Kuwa Wabunge mpaka Kesi ya Msingi itakapo malizika Kusikilizwa.

Yanasubiriwa maamuzi ya Jaji

Jaji Mgeta ametoa zuio la Muda, "Status quo" Wakina Mdee Waendelee Kuwa Bungeni mpaka tarehe 13 June 2022 ambapo Nyaraka zitalepelekwa Mahakamani ambapo Kesi zote mbili zitaendelea Kusikilizwa

Pia, soma=> Wabunge 19 viti maalum CHADEMA wafungua kesi. Bunge lasema linasubiri uamuzi wa Mahakama kuu

Serikali imeingia kuwatetemekea akina Mdee kwa nini?. Wakati maombi yapo dhidi ya Mwanasheria mkuu wa serikali?.
 
Tulikubaliana tupo awamu inayotenda haki. Tusihangaike ku-influence kwa namna iwayo yote uamuzi wa mahakama. Tuwaachie mawakili na wanasheria wafanye kazi zao.

Bora tu turudi kwa Magufuli kuliko Hawa wanafiki wapumbavu wasio na haya. Wako tayari kufanya lolote ili kuiumiza Chadema. Serikali yenye laana, walaaniwe wote.
 
Jaji amepanga kesi kutajwa tarehe 13Juni2022, siku moja kabla ya kuwasilisha Bajeti Kuu ya serikali, Siku chache baada ya kuhitimisha bajeti za wizara mbalimbali.
Hii imekaa vizuri kwa maana Serikali,itakuwa imepokea michango ya wabunge wa upinzani wa CHADEMA,
Kuna uwezekano mkubwa uamuzi ukatolewa baada ya kikao hiki cha Bunge.

Funzo kwa CHADEMA
1). CHADEMA ilipaswa kuwaachisha wabunge (Mdee na wenzake) na kupendekeza majina ya wabunge wengine ili shughuli za Bunge ziendelea,(wangejifunza kutoka kwa Prof Lipumba wa CUF).
2). CHADEMA iache mambo ya kususa,ukisusa watu wanakula,walisusia matokeo ya uchaguzi 2020, watoto wa mjini wakachukua fursa.
 
Back
Top Bottom