Kwako Kaburu Robert Amsterdam
Anafatananalo, unasema huyu anafatana na lile jitu kwanini?Manake sio heshima huyu kuandamana na yule.
Lakini unagundua anaandama hela. Ni, hii tabia ya kimalaya Malaya hii.
Na tunao wanasiasa wenye tabia ya kimalaya malaya namna hii, wananunulika.Heshima yao inauzwa, inabei.
Anakuuliza, fanya kitendo kadhaa ambacho ni kitendo cha aibu lakini anakuuliza ngapi baba ukitoa bei!ukimlipa!basi anakubali.
Mwanasiasa anatabia ya kimalaya Malaya hii!
Sasa dhahiri mtu mwenyetabia ya umalaya malaya kwasababu yeye ananunulika anafikiriki na wenzie vilevile wananunulika. Kwahiyo anatoka anakwenda kwa watu wengine kuzani watu wengine wanaweza kufanya vilevile mambo ya aibuaibu ambayo hayana heshima, alafu anajuta, anajuta.
Kuna majeshi duniani humu ni majeshi yanaitwa mercenaries walikuwa pale wako wako Congo pale wanaitwa mercenaries, nyinyi nyinyi vijana mnajua.
Itaendelea.