Salaam Mkuu,
leo Ijumaa tarehe 28 Agosti 2020 Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, kinafanya uzinduzi wa kampeni za urais wa Tanzania zinazofanyika, Uwanja wa Zakhiem, Mbagala jijini Dar es Salaam.
Tundu Lissu ndiye anayepeperusha bendera ya Chadema kwenye nafasi ya urais na Salumu Mwalimu mgombea mwenza.
Kampeni za Uchaguzi Mkuu zilifunguliwa rasmi tarehe 26 Agosti na zitahitimishwa tarehe 27 Oktoba 2020 ambapo kesho yake yaani Jumatano itakuwa ni siku ya uchaguzi. Katika uchauzi huu, Lissu atachuana na wagombea wengine 14 akiwemo Dk. John Magufuli, mgombea wa Chama cha Cha Mapinduzi (CCM), Prof. Ibrahim Lipumba (CUF), Yeremia Maganja (NCCR-Mageuzi).
Nitawaletea Kila kinachojiri.
View attachment 1550719View attachment 1550720View attachment 1550721
Lissu ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Chadema bara na Mwalimu, naibu Katibu Mkuu-Zanzibar tayari wamewasili uwanja hapo.
Ulinzi umeimarishwa katika viwanja hivyo, ambapo kuna baadhi ya askari polisi wa kawaida na wale wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU).
Pia, kuna walinzi maalum wa Chadema ambao wanafanya kazi ya kuongoza watu waliofika katika kampeni hizo.
======
UPDATES: 1600HRS
Mkutano Umeanza kwa Kuimba Wimbo wa Taifa na kufuatiwa na Maombi kutoka Madhehbu mbalimbali