Uchaguzi 2020 Yaliyojiri Vikao vya CHADEMA: Tundu Lissu aibuka kidedea kuwania Urais wa Tanzania kwa kupata kura 405 dhidi ya Nyalandu 36 na Dkt. Majige 1

Ipo...zipo youtube! Lissu bado mwanaharakati siyo 'presidential material'...mwanzo wa uombaji kura wake tu unaeleza kila kitu. Ngoja niendelee kufuatilia uombaji kura wa wengine.

Una grievances zako binafsi nadhani na Tundu Lissu.

Hujaona kitu kimoja katika hii "very well directed movie" wanayofanya CHADEMA ambayo mimi na naamini na wengine wameona....

Nimemsikiliza Nyalandu Lazaro mwanzo mwisho. Nikamsikiliza Dr MayRose Majinge naye mwanzo mwisho na mwisho nikamtazama na kumsikiliza Tundu Lissu mwanzo mwisho

Kwa hakika kabisa, TUNDU LISSU ameshapita hata kabla ya kura kupigwa. Hii kitu ndivyo ilivyokuwa planned.

Hotuba yake tu inaeleza na kuthibitisha kila kitu hata namna ilivyopokelewa na kuamusha hisia za wajumbe.

Ni hotuba ambayo si ya kunyenyekea kuomba kura kwa wajumbe. Ni hotuba iliyobeba "authority" ndani yake kama vile tayari keshathibitishwa kuwa mgombea rasmi ili hali yuko kwenye mchujo...

Na ni hotuba ambayo moja kwa moja ikishambulia SERA na UTAWALA wa CCM chini ya Bwana John Pombe Magufuli. Ni picha inayoonesha kuwa Bw. Nyalandu na Dr MayRose ni wasindikizaji tu....!!

Nyalandu ni mtu mzuri na anaweza kuwa Rais. Lakini ktk uchaguzi wa mwaka huu 2020 hafai, hatawez. Huyu hawezi purukushani za kupambana na CCM. Ni kwa sababu CCM wenyewe wana mgombea mtukutu na mpenda Shari...

Huyu anapaswa kupambanishwa na mtu wa aina ya Tundu Lissu. Wagombea legelege wasiojiamini hawawezi kupambana na CCM hii na mgombea wao. Tundu kaonja mauti. Haogopi lolote. Huyu anafaa. Ni jasiri sana. Ana uelewa sana wa mambo mengi....!

Hii ndiyo tofauti ya wagombea hawa watatu....

Kwako wewe huyu bwana TL siyo "presidential material". Ni sawa na haki yako kabisa kumtazama na kum - describe kwa jinsi hiyo japo hujatoa sababu zote kuunga mkono hoja yako hiyo....

Lakini watoto wa mjini wanasema " .....usiyempenda kaja, yuko hapo anabisha hodi mlangoni mwako..."
 
Kila la kheri kwenye uchaguzi wao.
 
Wale wote walionde kumpokea. Lisu wakitoa 2000 @ na wale wipengine wasiopenda kuozesha mama zao ...... wakitoa 1000 Mbuyu ashoka moja mbaliiii. Sitanii atiii
Wale mbona ni kidogo sana, wengi hawakuweza kufika kwa vitisho vya polisi. Kampeni yake ilianza kuchangiwa miezi miwili iliyopita. Swala likiwa la Lissu watu watauza kuku, bata, mbuzi, kondoo, ng’ombe ili mradi wachangie.
 


Kuna upotoshaji katika post hii ambayo napata nayo mashakaπŸ™ŒπŸ»πŸ™ŒπŸ»
 
Naona Chadema hawajaruhusu camera kuingia kwenye uhesabuji kura. Naona wanaogopa wasijepigana ngumi humo halafu tukaona hewani. πŸ˜‚
Taratibu za kawaida kabisa za kiulinzi!
 
Nimependa sn hiiπŸ‘‡πŸ‘‡

Nyalandu ni mtu mzuri na anaweza kuwa Rais. Lakini ktk uchaguzi hafai, hataweza purukushani. CCM wenyewe wana mgombea mtukutu na mpenda Shari. Huyu anapaswa kupambanishwa na mtu wa aina ya Tundu Lissu...!
 
Kwa nini hamjaruhusu watu wa habari waingie? Au mnaogopa mtapigana makonde ?Upigaji kura ulipoanza naona live online tv hazionyeshi tena.
Mbona wanaonyesha Onlinetv hata zoezi LA kuhesabu?
 
Wazee wa Lumumba kazi mnayo mwaka huu! Tangu lini CCM mkawatakia mema Chadema wapate mgombea sahihi..
 
Kura zinahesabiwa sasa na ziko live online TV na Nyalandu na yule mama wanahakikisha kura zao huku Heche akimuwakilisha Lissu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…