Uchaguzi 2020 Yanayojiri Matokeo ya CHADEMA kura za maoni kwa Wagombea Ubunge 2020

Uchaguzi 2020 Yanayojiri Matokeo ya CHADEMA kura za maoni kwa Wagombea Ubunge 2020

Halafu mbona wanawake wanashinda sana kura za maoni hapo Dar kwa CHADEMA, naona kwa leo tu kuna Agness Lambart ameshinda Segerea, Susan Lymo Kinondoni, na Lucy Magereri huko kigamboni, bado hatujaongelea kawe ambapo mdee lazima atachukua, kuna ukonga alishindaga Asia Msangi dhidi ya Waitara na najua hata this time atashinda. Wanaume wa Dar wa CHADEMA mnakwama wapi?
nadhani wanafanya rejea ya waliounga juhudi... wengi wao ni wanaume... so haina haja ya kuwabeba
 
Sio ukabila

Ila huyu ni Kati ya icon wa chama.
Icon wapi lazima CHADEMA iheshimu demokrasia, hii tabia ya kuwaona waliomkataa wajinga ndiyo mwisho wa siku tunakosa jimbo tunaanza kulaumu tumeibiwa kura kumbe tumeweka mtu asiyekubalika.

Hao waliopiga kura ni wajumbe wanaotoka jimbo hilo hivyo wanajua nani anafaa na nani hafai na huyo binti ni masikini kachupile labda angekuwa na mapesa tungesema amehonga sasa sahizi atakatwa kwa kutumia sababu gani?
 
Kura za maoni ni mchakato wa kidemokrasia , yeyote aweza kuteuliwa kati ya wawili wa juu , Mrema kutokana na kubanwa na majukumu ya Makao Makuu hakupata hata uchochoro wa kupiga kampeni , inashangaza hata hizo kura amepataje .
Naona unapiga debe upate mgao wako, ila ubunge mtausikilizia kwenye bomba chadema mkiendelea na ujinga wenu huo
 
Back
Top Bottom