Uchaguzi 2020 Yanayojiri Matokeo ya CHADEMA kura za maoni kwa Wagombea Ubunge 2020

Uchaguzi 2020 Yanayojiri Matokeo ya CHADEMA kura za maoni kwa Wagombea Ubunge 2020

Sio makamo ni makamu au ukishindwa sana sema NAIBU. Sorry for interrupting your message
Susan Lyimo ameshinda katika Kura za Maoni za kumteua mgombea wa Chadema Jimbo la Kinondoni. Amepata kura 71 kati ya 113. Sawa na asilimia 62.8. Amewashinda Moza Ally (Makamo Mwenyekiti Bavicha), Rose Moshi diwani Viti Maalum na Mbezi Mwombeki
 
Hiki chama hakina waislamu, sheikh ponda hebu watolee tamko maana hata wale wana afadhali
 
Mwanyamaki hajagombea ?

Nimeona kule Rungwe Mwambigija kapigwa chini na Sophia Mwakagenda
Duh Mwambigija A.K.A mzee wa upako? Dah asije susa tu na kujiunga CCM huwa namkubali sana huyu jamaa.

Nilitamani pia mwaka huu Mwakibinga angetinga bungeni sijui akaingia tamaa gani kapotea kabisa kwenye siasa.
 
Jimbo la kawe..

Mshindi wa uchaguzi kwenye kura za maoni za Ubunge CHADEMA Jimbo la Kawe ni Halima Mdee mwenye kura 63 (71.5%) akifuatiwa na Doricus Mwilafi mwenye kura 13 (14.7%), Joel Mwakalebela kura 7 (7.9%) na Felsta Njau kura 5 (5.6%)
FB_IMG_1594764402482.jpeg
 
Jimbo la musoma mjini

Nawashukuru Sana Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Jimbo la Musoma Mjini kwa kunipendekeza kuwa Mgombea Ubunge wa Jimbo kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)
#Julius_Gabriel_Mwita 116
#Kichere_Mhere. 39

Asanteni Musoma.
#MusomaYetu2020
#MbungeWetu2020


Julius Mwita
 
Endelea kutega sikio kutokea hapahapa JF
Kwa matumaini makubwa, natega sikio na macho, kama sikuchanganyikiwa! Nimechanganyikiwa?

Hadi hapa nimekuwa nikifuatilia kimya kimya, ila nasoma 'trend' ambayo nadhani itakuwa ni mwanzo mpya kwa nchi yetu.

Hawa mabinti wamepania hasa, na najua huu ni mwanzo tu, hata huko CCM 2025 kama watakuwa bado wapo hali itakuwa ni tofauti kabisa na sasa.

Darasa la akina Mdee, Ester wawili na wenzao naona linasomeka vizuri.

Mwisho nikuulize hili swali Erythro:Alinanuswe Mwalwange, KE/ME? Ana jina gumu huyu mtu.
 
Nimeshangaa kuona wagombea ubunge kupitia Chadema zaidi ya watano wakiwa wamepitishwa kwa kura za "NDIO" bila uwepo wa wagombea shindani.

Je, hii ndio demokrasia ndani ya chama kinachojiita cha demokrasia?
 
Nimeshangaa kuona wagombea ubunge kupitia Chadema zaidi ya watano wakiwa wamepitishwa kwa kura za "NDIO" bila uwepo wa wagombea shindani.
Je hii ndio demokrasia ndani ya Chama kinachojiita cha demokrasia??

POVU RUKSA


Mbona kawaida hata mapombe kapita bila kupingwa
 
Back
Top Bottom