Yanga yashikilia msimamo wake wa kutocheza derby ya Kariakoo 15/6/2025

Yanga yashikilia msimamo wake wa kutocheza derby ya Kariakoo 15/6/2025

Alafu nyie tu awadai pesa zetu mara mbili mjue...derby na ile ya berkane. Shenz type
Mechi ya Berkane walitumia kodi za wananchi vibaya. Timu inashindwaje kushinda hata mechi moja ya fainali?
 
Screenshot_20250607_164546.jpg
 
Mechi ya Berkane walitumia kodi za wananchi vibaya. Timu inashindwaje kushinda hata mechi moja ya fainali?
Wewe uliyeshinda una nini cha kuonyesha ambacho Simba hana?
 
Mimi ni simba ila hili liwe funzo kwa viongozi wetu wa ligi kuwa makini katika maamuzi Yao.
 
Hii sentensi ya mwisho kama imenitia ukakasi.. mpaka matakwa yatimizwe sio pamatafutwa mwaya wa kuja kucheza???! Mana bodi inaweza kuja hadharani tarehe 12 wakasema tumeyatimiza matakwa yenu ambayo kimsingi hayajawekwa wazi! Tutakataa kucheza?
 
Sisi hatuigi waliokimbia tunataka haki itendeke.
Mngekuwa mnaiishi haki kama mnavyohubiri basi msingethubutu kuwazuia Simba wasifanye mazoezi wakati mnajua fika kuwa ni haki yao.

By the way huna haki yeyote kwenye hili na ndio maana CAS, TFF mmeshindwa na saizi naskia hapo juzi mlienda mahakama ya serikali nako mkashindwa.

Sasa how dare you kusema unataka haki itendeke ilihali vyombo vyote vinavyohusika na huo utoaji Haki vimekutema?

Gomeni kuja tuwaoneshe kwanini huwa wanagawa ndimu kwenye boti.
 
1: Mwenyekiti wa bodi ya ligi ajiuzuru
2: Ajiuzuru Afisa mtendaji mkuu wa TPLB
3: Ajiuzuru katibu mkuu wa TFF
4: Bodi ya Ligi Kuu, inakuwa chombo huru.
Yakifanyika hayo, Yanga itapeleka timu uwanjani!
Unahisi yanawezekana?
 
Timu yenye confidence na uhakika wa kushinda isingeweza kugomea mechi.

Kugomea mechi kumetokana na tafakuri ya kina walioifanya na kuona hakuna mazingira yeyote wanayoyaona kwa wao kuweza kushinda mechi.
kugomea mechi kumekuja baada ya bodi ya ligi kumkimbiza mpinzani kwa hofu ya kupigwa nyingi

hii ni baada ya kuonekana nyota wake kadhaa kuwa majeruhi mahaba ya bodi ndiyo yanafanya mtambe sasa hivi
 
TAARIFA KWA UMΜΑ
JUNI 09, 2025​

Uongozi wa Young Africans Sports Club, unapenda kuutarifu umma kuwa, tarehe 7 Juni, 2025 tulipokea barua kutoka Bodi ya Ligi Kuu Tanzania kwa ajili ya kuhudhuria kikao maalum cha kujadili masuala yahusuyo mchezo namba 184 wa Ligi Kuu ya NBC, YANGA dhidi ya Simba.

Uongozi wa Klabu yetu ulitii wito huo na kushiriki kwenye kikao kilichofanyika leo, Jumatatu Juni 9, 2025 kwenye ofisi za Bodi ya Ligi Tanzania zilizopo jengo la NSSF Mafao House, Dar Es Salaam, kuanzia saa 4:00 asubuhi.

Baada ya majadiliano ya saa kadhaa, Viongozi wa Klabu waliwasilisha msimamo wa Klabu yetu kuwa hatutashiriki mchezo namba 184 uliopangwa kufanyika tarehe 15 Juni 2025 mpaka pale matakwa yetu tuliyoyawasilisha kwa maandishi kwao yatakapotimizwa.

Tunawatakia kila la heri Bodi ya Ligi na Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini katika kushughulikia matakwa yetu yenye mustakabali mkubwa kwenye maendeleo ya mpira wa miguu Tanzania.

Imetolewa na
Kamati ya Utendaji
Young Africans Sports Club

Soma Pia: Ali Kamwe: Bodi ya Ligi ikisikiliza na kutekeleza mahitaji yetu tutacheza Kariakoo Derby ya Juni 15, 2025


Soma Almas Kasongo: Tumekutana na Yanga, Derby ya Kariakoo iko palepale na hakuna kilichobadilika
Hata mje na drama gani hatutoki kwenye
No REFORMS No ELECTION
 
kugomea mechi kumekuja baada ya bodi ya ligi kumkimbiza mpinzani kwa hofu ya kupigwa nyingi

hii ni baada ya kuonekana nyota wake kadhaa kuwa majeruhi mahaba ya bodi ndiyo yanafanya mtambe sasa hivi
Mi nadhani nyie ndio mliokuwa na malengo ya kukimbia mechi that's why mkaja na njama za kuwazuia wachezaji wasifanye mazoezi mkijua hiyo ndio nafasi ya nyie kujifichia.
 
Wewe uliyeshinda una nini cha kuonyesha ambacho Simba hana?
Mbwembwe zote zile mkapigwa tatu halafu mkapigwa tatu tena shirikisho la nchini. Mechi 3 shots on target 3 goli mbili
 
Mi nadhani nyie ndio mliokuwa na malengo ya kukimbia mechi that's why mkaja na njama za kuwazuia wachezaji wasifanye mazoezi mkijua hiyo ndio nafasi ya nyie kujifichia.
Simba walizuiwa na mabaunsa wa Simba wenyewe. Leteni ushahidi kama kweli Yanga walihusika.
 
Simba walizuiwa na mabaunsa wa Simba wenyewe. Leteni ushahidi kama kweli Yanga walihusika.
Mmoja wa mabaunsa wa Simba akiongea namna walivyo wazuia Simba kufanya mazoezi
 
  • Nzuri
Reactions: Tui
Simba walizuiwa na mabaunsa wa Simba wenyewe. Leteni ushahidi kama kweli Yanga walihusika.
Naona na wewe huna nafuu.Ukichaa wako kujidhihirisha lilikuwa ni suala la muda tu.Gongowazi mnatofautiana sura tu lakini uwezo wenu mdogo sana wa kutafakuri ni ule ule.
Umesoma barua walioandika vichaa wenzako?
Pia msikilize kichaa mwenzako hapo juu.
 
Back
Top Bottom