Yawezekana hali halisi ndani ya Israel ni mbaya kuliko….

Yawezekana hali halisi ndani ya Israel ni mbaya kuliko….

Hakuna shaka kuwa safari hii Israel imepata zaidi ya ilichokuwa inakitafuta kwa kuishambulia Iran.

Pia hakuna shaka kabisa kuwa Iran inao uwezo wa kupambana na Israel moja kwa moja na kusababisha madhara makubwa sana.

Vilevile, Iran imeonyesha kuwa, Israel, bila kupigwa tafu na Marekani, ni mchumba mbele ya Iran.

Iron dome ya Israel kumbe wala haina sifa wala ubora ambao tulikuwa tunaaminishwa inao.

Hiyo iron dome saizi yake ni hayo makundi tu ya wanamgambo na sungusungu kama Hamas, Hizbollah, na hao Wahouth wa huko Yemen.

Kama licha ya military censorship iliyopo ndani Israel na tumeweza kupata picha kama hizi….

View attachment 3381009View attachment 3381010View attachment 3381011View attachment 3381012

Pata picha ya yale ambayo hatuyaoni kutokana na kuwepo kwa hiyo military censorship.

Hali hii ndo inayonifanya nihitimishe kuwa hali ndani ya Israel ni mbaya kuliko.

Na yote hayo ni kwa hisani ya jeshi la Iran!

Nchi ambayo inapambana peke yake dhidi ya mataifa mawili yenye silaha za nyuklia na ni nchi ambayo ipo chini ya vikwazo vingi vya kiuchumi, imejitahidi sana.

Jana kumetangazwa kuwepo kwa makubaliano ya kusitisha mapigano.

Kwa uzoefu wangu, kama kweli hayo makubaliano yapo, yanaweza yasidumu hata kwa siku mbili na wataanza kulaumiana na kunyoosheana vidole kuhusu nani kaanza kuyakiuka.

Natumaini hayo makubaliano yatadumu.

Wairan wana sababu zote za kujivunia jinsi nchi yao ilivyopambana na kuisababishia madhara Israel, madhara ambayo Israel haijawahi kuyapata.

Iran wana haki zote za kutembea vifua mbele na vichwa juu kwa somo walilowapa Israel.

They far exceeded my wild expectations!!

NB: Na kwa vile propaganda ni sehemu muhimu sana ya vita, kama Iran ingekuwa haisababishi madhara makubwa, Israel wangetuonyesha na wangejitapa kuwa iron dome yao ni kiboko.
Sema hii dunia ina ubabe mwingi sana
Marekani ana silaha nyingi za nuclear
Israel anazo pia na amegoma kusaini makubaliano ya kupunguza silaha za nuclear wala kuruhusu wakaguzi kwenye vinu vyake
Iran hana hizo nuclear na ameruhusu wakaguzi
Lakini bado kashambuliwa, watu wake wameuliwa na hakuna anayemtetea
Ulaya na Marekani zinamshtumu yeye tu
Vikwazo anawekewa yeye tu wakati huo Israel anapewa misaada ya kijeshi na kuua wapalestina kila siku
Hii dunia hii.
 
Sasa kama mtu haelewi hata anachokionhelea, nimuiteje sasa?

Wapi nimefurahia Iran kumshinda Marekani ilhali vita ni kati ya Israel na Iran?

Kuna sehemu nimeandika kuwa nimefurahishwa na Iran kumshinda Marekani?

Mambo ya ajabu kabisa hayo.

Kijeshi Iran itawezaje kumshinda Marekani?

Ana mauerue huyo jamaa. Anaona vitu ambavyo havipo.
Ukikosolewa usikimbilie matusi au personal attack wewe mbona unakosoa
 
Hivi Israel nae aanze sasa kushanbulia residential building za Tehran ili mzani ubalansi sasa
Hayo majengo yanayoshambuliwa kule Israel ni mahali wanapojificha magaidi ya Kiyahudi.

Iran sio mjinga kuyashambulia majengo hayo.

Mbona kambi za kijeshi zilizopo Israel amekuwa akizishambulia unadhani anashambulia hayo majengo kwa bahati mbaya?

Magaidi ya Kiyahudi yatalengwa popote pale yatakapojificha hata chini ya mahandaki.
 
Iran wana censorship kubwa sana ndani ya iran huna uhuru huo unaotaka kuaminisha watu

Sisi waafrika tuendelee kushabikia vita ila hatuna tunachojua, mfano unaiponda marekani ila bado unanganinia kuishi marekani

Ni kama waarubu wanaziponda nchi za Western lakin kila siku wanakimbilia huko
Mkuu tuzungumzie vita Ngabu akiishi Yombo wewe unafaidika nini mambo ya mtu wewe yanakusaidia nini mazee hapo unaonyesha kuchukizwa na mmakonde kuishi USA kitu ambacho hata wewe ukiamua unaweza kufanya ingawaje sio rahisi kama unavyodhania.
 
Na kuna wengi tu ambao hawaitukani.

Na wapo raia wengi tu wa Marekani wanaoitukana Marekani.

So what’s your point?
Kwa mmarekani kuitukana nchi yake sio tatizo, hata na huku kwetu baadhi yao tunaitukana sana nchi yetu sio tatizo, tatizo ni mgeni kuitukana nchi ambayo sio yake hilo ni tatizo kubwa mnooo
 
Yaani Iran haidaiwi, wamefanya kitu cha kukumbukwa na vizazi na vizazi. Fikiria US yupo, Israel last born wa mabeberu, ana kila kitu kinachotakiwa kwenye vita.

Lakini katandikwa inavyotakiwa, kuepusha aibu Trump ndiyo kawa msemaji wa Israel 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣 anataka complete ceasefire. Iran kasema haitambui, kisharusha kitu huko 🔥🔥🔥

Hapo ndiyo ujue madhara Israel aliyoyapata, huwa tunasema Mungu ni wa wote, utaonea watu miaka ila iko siku yako, mambo lazima yakugeuke.

Trump kawatishia sana Iran akijua watarudi nyuma, alivyoona base yake ya Qatar inaanza kushambuliwa, akaona hawa wameshindikana. Iran angezipiga zote zilizo middle East.

Ahsante Allah/Mungu, Ahsante Iran, umejua kunyoosha watu, sasa watakuheshimu. Nina furaha, nilikuwa nawaombea sana. Tehran ni shangwe tu 🇮🇷🇮🇷🇮🇷🇮🇷🇮🇷🇮🇷🇮🇷🇮🇷🇮🇷🇮🇷🇮🇷🇮🇷🇮🇷🇮🇷
 
Mkuu tuzungumzie vita Ngabu akiishi Yombo wewe unafaidika nini mambo ya mtu wewe yanakusaidia nini mazee hapo unaonyesha kuchukizwa na mmakonde kuishi USA kitu ambacho hata wewe ukiamua unaweza kufanya ingawaje sio rahisi kama unavyodhania.
Mimi nikafanyaje marekani nikadandie mafanikio ya watu wengine na kujiona mjanja mintafia hapa hapa Tanzania kitovu change kilipotupiwa
 
Kwa mmarekani kuitukana nchi yake sio tatizo, hata na huku kwetu baadhi yao tunaitukana sana nchi yetu sio tatizo, tatizo ni mgeni kuitukana nchi ambayo sio yake hilo ni tatizo kubwa mnooo
Anaitukana kwa kila kitu au baadhi tu ya vitu?

Halafu ni akina nani hao wanaoitukana Marekani?

Weka orodha hapa…..
 
Mkuu tuzungumzie vita Ngabu akiishi Yombo wewe unafaidika nini mambo ya mtu wewe yanakusaidia nini mazee hapo unaonyesha kuchukizwa na mmakonde kuishi USA kitu ambacho hata wewe ukiamua unaweza kufanya ingawaje sio rahisi kama unavyodhania.
Na ku apply tu green card kwa sasa kuna malipo na hapo bado haujashinda😅😅😅
 
Back
Top Bottom