Yawezekana hali halisi ndani ya Israel ni mbaya kuliko….

Yawezekana hali halisi ndani ya Israel ni mbaya kuliko….

Israel kafikia malengo yake yote,,,kauwa wanasayansi,,kauwa waandamizi,,kaharibu vinu vya nuke,,kafanikiwa malengo yake yote...Iran kisasi chake hakikuwa na malengo..ni kama crazy anaetumia nyundo kuuwa nzi
 
Hakuna shaka kuwa safari hii Israel imepata zaidi ya ilichokuwa inakitafuta kwa kuishambulia Iran.

Pia hakuna shaka kabisa kuwa Iran inao uwezo wa kupambana na Israel moja kwa moja na kusababisha madhara makubwa sana.

Vilevile, Iran imeonyesha kuwa, Israel, bila kupigwa tafu na Marekani, ni mchumba mbele ya Iran.

Iron dome ya Israel kumbe wala haina sifa wala ubora ambao tulikuwa tunaaminishwa inao.

Hiyo iron dome saizi yake ni hayo makundi tu ya wanamgambo na sungusungu kama Hamas, Hizbollah, na hao Wahouth wa huko Yemen.

Kama licha ya military censorship iliyopo ndani Israel na tumeweza kupata picha kama hizi….

View attachment 3381009View attachment 3381010View attachment 3381011View attachment 3381012

Pata picha ya yale ambayo hatuyaoni kutokana na kuwepo kwa hiyo military censorship.

Hali hii ndo inayonifanya nihitimishe kuwa hali ndani ya Israel ni mbaya kuliko.

Na yote hayo ni kwa hisani ya jeshi la Iran!

Nchi ambayo inapambana peke yake dhidi ya mataifa mawili yenye silaha za nyuklia na ni nchi ambayo ipo chini ya vikwazo vingi vya kiuchumi, imejitahidi sana.

Jana kumetangazwa kuwepo kwa makubaliano ya kusitisha mapigano.

Kwa uzoefu wangu, kama kweli hayo makubaliano yapo, yanaweza yasidumu hata kwa siku mbili na wataanza kulaumiana na kunyoosheana vidole kuhusu nani kaanza kuyakiuka.

Natumaini hayo makubaliano yatadumu.

Wairan wana sababu zote za kujivunia jinsi nchi yao ilivyopambana na kuisababishia madhara Israel, madhara ambayo Israel haijawahi kuyapata.

Iran wana haki zote za kutembea vifua mbele na vichwa juu kwa somo walilowapa Israel.

They far exceeded my wild expectations!!

NB: Na kwa vile propaganda ni sehemu muhimu sana ya vita, kama Iran ingekuwa haisababishi madhara makubwa, Israel wangetuonyesha na wangejitapa kuwa iron dome yao ni kiboko.
Usidhani,ni kweli madhara ni makubwa ndani ya israel ,na netanyahu hatorudia
 
Umeshaona Al jazeera alirusha picha za sehemu zilizoharibika kama anavyofanya kwa Israel na kumbuka Al jazeera alikuwa na studio kabisa Israel ila hajawahi kuwa na studio Iran umeshawahi jiuliza ni kwanini hajawahi kuwa na studio iran
Jana israel walishambulia Iran sehemu ambayo ni karibu na studio za al jazeera
 
Inabidi ufikirie tena usahihi wa msimamo wako.
Kwa vile ni maoni (opinion) siyo kielelezo cha hali halisi (fact) au uhalisia (reality) basi naheshimu hoja yako.
Maoni ya wengine nikiwemo Iran ameshinda pakubwa sana kwenye hii vita.
Maoni hayana basis. Iran kashinda vita kwenye nini wakati vinu vya nyuklia vimelipuliwa na Israel bado ipo. Nani katimiza lengo kati ya Iran na Israel?
Amefanya uharibifu mkubwa ndani ya Israel na kubwa zaidi amevunja heshima au sifa za uhodari wa mifumo ya ulinzi wa anga wa Israel na Marekani.
Iran ndio amevunjiwa heshima. Ndani ya miaka miwili Israel imeua:
1. Mkuu wa Hezbollah
2. Mkuu wa kisiasa wa Hamas
3. Mkuu wa military wing ya Hamas
4. Rais wa Iran "kafa kwa ajari" baada ya Israel kutangaza kulipa kisasi.
Tukija kwenye vita hii mwezi huu.
5. Mkuu wa jeshi la Iran kauwawa na Israel
6. Mkuu wa jeshi mpya kauwawa baada ya siku 3.
7. Mkuu wa Airforce kauwawa
8. Mkuu wa Intelligence kauwawa.

Iran inashambuliwa kutokea ndani ya nchi na mamluki, mamlaka zipo.
Iron Dome na nyingine zote sasa chali.
Air defense systems za Iran zimeharibiwa zote hata fighter moja wameshindwa kuangusha.

1. S-300 kutoka Urusi
2. Dezful
3. Sayyad
4. Bavar 373
4. Mersad

Zote hizo ziligeuka makopo tu. Israel ikitaka mkuu wa jeshi inaua, ikitaka kinu cha nyuklia inapiga.

Kwenye soko la hisa kwenye biashara ya silaha na mifumo ya ulinzi wa kivita hisa za hiyo mifumo zimeporomoka.
Ushindi wa Iran ni kuporomosha hisa za silaha za Israel (kwa muda). Ushindi wa Israel ni kuharibu urutubishaji wa Uranium na kuzuia Iran kutengeneza nukes.
Pili amewaondoa uoga wadau, mataifa au taasisi sitakazo jikuta zinakpambana na Israel na Marekani.
Hawakuwa waoga tangu mwanzo, na walipotezwa. Walianza Hamas ile October 17, wakafuata Hezbollah kisha Israel ikawafuata baba yao Iran.

Iran ndio aliondolewa uoga. Alafu kafanya vibaya kuliko hata Hamas.
Mwisho kabisa ni suala la kurutubisha Uranium (nuclear materials enrichment). Sasa Iran anaweza kuwa amepata uhalali wa kuendeleza huo mradi mara tatu ya hapo awali na kutowajibika kwa yeyote au kuogopa kelele za UN n.k. Amepewa leseni (literally) ya kufanya bila kuhojiwa. Anaweza kujiondoa IAEA.
Syria kinu chao kilipigwa na Israel, hawakurudia. Iraq kinu chao kilipigwa na Israel hawakurudia. Israel mzoefu wa hizi kazi, tumuone Iran sasa.
Israel kuanzia sasa ataiogopa Iran kwa miaka mingi ijayo. Na hii Vita inaweza kumuondoa Netanyau madarakani kitu ambacho kitapunguza mateso kwa Palestinians sababu hardliners wa Vita wa Israel watakuwa hawana mtu wao kwenye kitufe cha kuanzisha Vita.
Israel haogopi yeyote ndio maana ndani ya miaka miwili anapigana na mamluki na mfadhiri wao wote anapiga. Na hajawahi ogopa mtu hata wakiunganisha majeshi waje nchi mbili aliwahi wakabili.

Israel hatoiogopa Iran, si ajabu hata mwakani akashambulia tena. Iran imetumia silaha zote imeshindwa, Israel haijatumia cruise missile wala ballistic missiles ni ndege tu, inazo options nyingi imeziweka pembeni.

Netanyahu kuondoka madaraki haitakuwa nafuu ya Wapalestina wala Iran. Alikuwepo Ariel Sharon kubwa la maadui wa Wapalestina akaondoka na bado hawana unafuu.
Netanyahu ataondoka ila ndio the longest serving Israel PM, na ndio kaongoza mara 3 tofauti akiondoka na kurudi. Si ajabu akaondoka mazima maana hana deni.
 
Ikitokea ceasefire hakuna mshindi hapo, kuna kigezo kingine cha kutafuta mshindi kinatumika. Mshindi hutangazwa direct endapo kuna unconditional surrender, aliyepewa masharti bila akakubali ndio kashindwa.

Kwenye ceasfire au peace plan wote wamekubaliana. Tunarudi sasa kwenye chanzo cha vita.
Israel ilikuwa na lengo la kuharibu vinu vya nyuklia vya Iran, Iran huwa inaimba wimbo wa "Death to Zionists State, Death to Israel". Kipi kimefanyika hapo?

Tukija kwenye casualties. Israel imeua Wakuu wa majeshi wawili wa Iran, Chief of Staff mmoja (second in command), Chief of Airforce na mfyatua makombora mkuu, Chief of Intelligence na maafisa wengine waandamizi. Iran hata mgambo wa Israel kashindwa, ni kuua raia tu.
Israel katawala anga la Iran bila kikwazo.

Sasa Israel apigane kwa sababu zipi tena wakati urutubishaji wa nyuklia Iran hawezi tena. Iran ndio ilitakiwa igome kusitisha vita, Israel haina haja ya kugoma wakati lengo limetimia. Na Iran ikirudia kurutubisha Uranium tena utaona mashambulizi ya Israel yanajirudia.
Unasema hakuna mshindi alafu wakati huo unasema Israel ametimiza malengo yake basi tuseme Israel ndo imeshinda maana kushinda vita huwa kutimiza malengo.
Netanyau kipindi ana anzisha mashambuli alienda na malengo mawili kusambaratisha mpango wa nyukilia wa Iran na kubadilisha utawala nchini Iran na hakuna kilicho timia.
Mpango wa nyuklia Iran ina vinu 8 vya nyuklia vilivyo pigwa ni vitatu hata hivyo vilivyo pigwa hakuna uhakika iwapo vimeharibiwa kabisa, kuhusu mabadiliko ndo wameferi kwa aibu kubwa.

Kuhusu Israel kutawala anga ta Iran si bora Iran watasingizia hujuma zilizo fanywa dhidi ya mifumo ya ulinzi kutoka ndani, vipi kuhusu Israel ambaye mifumo yake yote ya anga ilikuwa ina fanya kazi na bado makombora ya Iran yakawa wanatawala anga lake na kufanya uharibifu?
 
Hapa naona Israel alishambulia akijua Iran atakaa kimya kama kawaida. Baadae kaona kina ni kirefu sana hakiwezi.
Na Israel watahakikisha wanarudi tena kushambulia Iran na hapo ndipo kutakuwa na vita kubwa zaidi.

Marekani nao wameishatambua uwezo wa Iran kwamba wana uwezo wa kushambulia vituo vyake vya kijeshi, hivyo atazidisha uzalishaji vifaa zaidi vya kiteknolojia khasa vya ADS na kuwauzia Qatar, Jordan, Kuwait, Bahrain na vingine

Yaani soko la silaha la Marekani litauza sana silaha kwa Israel na washirika wote wa Marekani katika mashariki ya kati.

Hali kadhalika Iran nao wataimarisha ADS zao, watanunua silaha zaidi kutoka Korea Kaskazini, China na Russia na itabidi wabadili mikataba yao ya kistratejia kwani haijumuishi masuala ya ulinzi na usalama isipokuwa biashara tu.

Russia nao watakuwa wamefurahi kwani wataendelea kuwepo Iran na kituo chao cha kijeshi na kuendelea kutoa msaada kwa Iran kwenye teknolojia zaidi kwani sasa hivi zile Shaheed zatengenezwa Russia na sio Iran.

Kwa upande wa utawala wa Iran ni kwamba umeshinda kupinduliwa kwani hakuna mtu au watu ambao waweza kwenda Tehran na umoja wa waIran ambao juzi wameandamana kuiunga mkono serikali ya nchi yao imewagopesha Israel na Marekani walokuwa wakipanga "regime change".

All in all Iran, itazidisha kasi ya kutengeneza silaha kali ikiwemo bomu lenyewe la nyuklia kwa msaada wa Korea Kaskazini na hapo atakuja kumfanya Israel wasilale usingizi.

Ni funzo tosha kwamba Iran siyo Iraq wala Libya ambazo mtu angeweza kufanya atakavyo bila kupata majibu "behind enemy lines".
 
Hakuna shaka kuwa safari hii Israel imepata zaidi ya ilichokuwa inakitafuta kwa kuishambulia Iran.

Pia hakuna shaka kabisa kuwa Iran inao uwezo wa kupambana na Israel moja kwa moja na kusababisha madhara makubwa sana.

Vilevile, Iran imeonyesha kuwa, Israel, bila kupigwa tafu na Marekani, ni mchumba mbele ya Iran.

Iron dome ya Israel kumbe wala haina sifa wala ubora ambao tulikuwa tunaaminishwa inao.

Hiyo iron dome saizi yake ni hayo makundi tu ya wanamgambo na sungusungu kama Hamas, Hizbollah, na hao Wahouth wa huko Yemen.

Kama licha ya military censorship iliyopo ndani Israel na tumeweza kupata picha kama hizi….

View attachment 3381009View attachment 3381010View attachment 3381011View attachment 3381012

Pata picha ya yale ambayo hatuyaoni kutokana na kuwepo kwa hiyo military censorship.

Hali hii ndo inayonifanya nihitimishe kuwa hali ndani ya Israel ni mbaya kuliko.

Na yote hayo ni kwa hisani ya jeshi la Iran!

Nchi ambayo inapambana peke yake dhidi ya mataifa mawili yenye silaha za nyuklia na ni nchi ambayo ipo chini ya vikwazo vingi vya kiuchumi, imejitahidi sana.

Jana kumetangazwa kuwepo kwa makubaliano ya kusitisha mapigano.

Kwa uzoefu wangu, kama kweli hayo makubaliano yapo, yanaweza yasidumu hata kwa siku mbili na wataanza kulaumiana na kunyoosheana vidole kuhusu nani kaanza kuyakiuka.

Natumaini hayo makubaliano yatadumu.

Wairan wana sababu zote za kujivunia jinsi nchi yao ilivyopambana na kuisababishia madhara Israel, madhara ambayo Israel haijawahi kuyapata.

Iran wana haki zote za kutembea vifua mbele na vichwa juu kwa somo walilowapa Israel.

They far exceeded my wild expectations!!

NB: Na kwa vile propaganda ni sehemu muhimu sana ya vita, kama Iran ingekuwa haisababishi madhara makubwa, Israel wangetuonyesha na wangejitapa kuwa iron dome yao ni kiboko.
Fact
 
Kuna hoja ukizidoma humu unajua moja kwa moja zimetoka kwenye vijiwe vya kahawa.


Kuna hoja mtu anakuambia Israel ni mkorofi, wanasahau Iran na proxy zake slogan yao ni kuifuta Israel kwenye ramani, nchi kama hiyo wanairuhusuje kwa mfano kumiliki silaha za maangamizi.


Wamekazana Israel anasaidiwa as if kuna vita ambayo ishawahi pigwa nchi ikakosa ally wake, wanasahau hata Kagera war tu, Tz ilisaidiwa na Mozambique.

Ukirudi kwenye hii vita, kama lengo la Iran ilikuwa ni kushambulia maeneo ya kiraia basi wamefanikiwa ila kama lengo ni kushambulia sehemu nyeti basi Israel ni wazi kafanikiwa zaidi.
Sasa wewe ndio unaleta hoja za vijiwe vya kahawa.
 
Ndio ashakubali sasa. Vinu vya nyuklia chakari, wakuu wa majeshi wawili wamefyekwa, mkuu wa Airforce kauwawa, mkuu wa Intelligence kauwawa.

Baada ya hapo anasaini kuacha vita. Kisha wanamgambo wa JF wanakwambia eti Iran kashinda 😂
Vinu vya Nuclear vipo salama kabisa, na vyombo mbali mbali vimelipoti na hata Jana Israel kashambuli Tena huko kuzuia access ya wairani huko. Nadhani Israel angekataa ceasefire kama anavyokataa na Hamas mpaka Regime change ifanyike na ndio lilikua lengo lake kubwa. Maana alisema bila Regime change basi wairani wataendelea kufadhili makundi ya kigaidi hivyo bila Regime change Bado hajafikia malengo yote.
 
Unasema hakuna mshindi alafu wakati huo unasema Israel ametimiza malengo yake basi tuseme Israel ndo imeshinda maana kushinda vita huwa kutimiza malengo.
Netanyau kipindi ana anzisha mashambuli alienda na malengo mawili kusambaratisha mpango wa nyukilia wa Iran na kubadilisha utawala nchini Iran na hakuna kilicho timia.
Mpango wa nyuklia Iran ina vinu 8 vya nyuklia vilivyo pigwa ni vitatu hata hivyo vilivyo pigwa hakuna uhakika iwapo vimeharibiwa kabisa, kuhusu mabadiliko ndo wameferi kwa aibu kubwa.

Kuhusu Israel kutawala anga ta Iran si bora Iran watasingizia hujuma zilizo fanywa dhidi ya mifumo ya ulinzi kutoka ndani, vipi kuhusu Israel ambaye mifumo yake yote ya anga ilikuwa ina fanya kazi na bado makombora ya Iran yakawa wanatawala anga lake na kufanya uharibifu?
Azimio la Umoja wa Mataifa namba 2231 lilowekwa mwaka 2015 litafikia ukomo wake tarehe 1 October 2025.

Azimio hilo linoitwa JCPOA (Joint Comprehensive Plan of Action lilifikwa makubaliano kati ya China, Russia, UK, Marekani, France, Germany, Mwakilishi wa EU na Iran yenyewe.

Azimio hilo liliwekwa kwa makusudi kuizuia Iran kupata uwezo wa kiuchumi na kijeshi na kuilazimisha kufungua mlango wa rasilimali zake.

Hivyo, ikifika tarehe 1 October azimio hilo litakufa na huenda mashambulizi ya Israel na Marekani yamefanywa mapema kwa kuangazia kufa kwa azimio hilo ambapo litapokufika ukomo, Iran itakuwa na uwezo wa kujitoa AIEA na pia kkuza ushirikiano na nchi marafiki katika nyanja zote usalama, ulinzi na biashara.

Soma hapa kuhusu Azimio la UN 2231 : Resolution 2231 (2015) on Iran Nuclear Issue | Security Council
 
Back
Top Bottom